Arusha

HATMA YA LEMA 

 HATMA mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (Chadema), itajulikana Aprili 5, mwaka huu baada ya  Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kutoa hukumu.

Uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya wakakili wa pande zote mbili kufanya mashauriano ya faragha na Jaji Gabriel Rwakibarila na kukubaliana kuwasilisha hoja zao za mwisho kwa njia ya maandishi Machi 30, mwaka huu kabla ya saa 3:00 asubuhi.
 “Mheshimiwa Jaji, baada ya kutathmini na kutafakari, tumeridhika na ushahidi wetu na tunaomba kuitaarifu mahakama yako tukufu kuwa tunafunga ushahidi wa mdaiwa wa kwanza kwa sababu hatutarajii kuita shahidi mwingine,” alisema Wakili Method Kimomogoro.

Naye wakili wa serikali, Juma Masanja anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo ambalo lilifunguliwa na wapiga kura watatu, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo aliieleza mahakama kuwa baada kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa wadai na mdaiwa wa kwanza, hawaoni haja ya kuita shahidi yeyote, badala yake watajikita zaidi kwenye hoja za mwisho.

Awali akihojiwa na wakili wa wadai katika shauri hilo, Alute Mughwai, shahidi
wanne upande wa utetezi, Samson Mwigamba alidai chama chake hakikuwa na imani na msimamizi mpya wa uchaguzi katika Jimbo la Arusha mjini, Estomih Chang’a tangu alipoteuliwa kuchukua nafasi ya Raphael Mbunda aliyekuwapo awali.

Mwagamba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Arusha alidai walikosa imani na msimamiza huyo kutokana na kitendo chake cha kutumia kamati yake ya maadili ya jimbo kumwadhibu aliyekuwa mgombea wao, Godbless Lema kutokana na barua ya malalamiko iliyoandikwa na Dk Batilda Burian aliyegombea kupitia CCM ambayo awali ilipuuzwa na mtangulizi.

Shahidi huyo alimweleza Jaji Rwakibarila kuwa Mbunda alihamishwa ghafla baada ya kupuuza malalamiko ya Dk Burian baada ya kukosa ushahidi.


Aliieleza mahakama kuwa baada ya kupokea barua ya mbunge wao Lema ya kutiwa hatiani na kutozwa faini ya Sh100,000, waliamua kulipa badala ya kukata rufaa licha ya kutokukubaliana na adhabu hiyo ili kuepuka kupoteza muda wa kampeni.

Mwigamba alidai kwamba alifika mahakamani kusema ukweli na kuithibitishia mahakama kuwa madai yote yaliyowasilishwa na wadai ni uongo.

Katika madai yao, wadai ambao wote ni wana CCM wanaoimba mahakama kutengua ushindi wa Lema kwa madai kuwa alitumia lugha za kashfa, matusi na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian wakati wa mikutano ya kampeni na waliita mashahidi 14 mahakamani kujenga hoja zao.

Madai hayo yamekanushwa na Lema aliyekuwa shahidi wa kwanza upande wa utetezi pamoja mashahidi wengine watatu awaliowaita mahakamani hapo.









MGOGORO UVCCM



MGOGORO  unaofukuta ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Arumeru mkoani Arusha, umeingia katika sura mpya baada ya uongozi wa jumuiya hiyo kuitisha kikao cha dharura na kutoa tamko la kumpiga marufuku mjumbe wa umoja huo, Kennedy Mpumilwa kutoshiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wilayani humo.

Pia, uongozi huo umemtaka Mpumilwa kutovaa sare za chama hicho huku wakimtuhum kwamba amekuwa akikivuruga chama cha CCM wilayani humo kwa kutumiwa na wapinzani hususani Chadema.

“Kennedy siku zote amekuwa mjenga hoja wa kubomoa hoja za CCM Arumeru, asionekane amevaa sare za CCM na wala asishiriki kampeni za CCM wakati mchakato utakapoanza,” alisema Pallangyo ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM kata ya King'ori wilayani Arumeru.

Katika kikao hicho waliohudhuria ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, James Ole Millya, mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, Esther Maleko pamoja na wenyeviti 17 wa UVCCM wa kata 17 za wilayani humo.

Tamko hilo limetolewa baada ya Mpumilwa ambaye ni mjumbe wa Baraza la Vijana mkoani Arusha kupinga vikali matokeo ya uchaguzi wa kumtafuta mwakilishi atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa ubunge wilayani humo, mtoto wa marehemu Sumari,Sioi Sumari kwa madai kwamba ulijaa rushwa.

Akitoa tamko hilo katika ofisi za CCM zilizopo eneo la Kikatiti wilayani humo kwa niaba ya wenyeviti 17  wa kata wa UVCCM wilayani Arumeru aliokuwa ameambatana nao, mwenyekiti wa UVCCM kata ya King”ori, Pallangyo alisema kwamba taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba hali si shwari ndani ya jumuiya yao si za kweli.

Pallangyo, alisema kwamba mara baada ya uchaguzi wa awali wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM kumekuwa na taarifa kwamba hali ya kisiasa ndani ya umoja wao si shwari kwa kuwa kuna mgawanyiko, kitendo ambacho alidai kinapotoshwa na watu wachache.

Alisema kwamba kumekuwa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na Mpumilwa kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa na mizengwe kitendo ambacho si sahihi huku akisisitiza kwamba kada huyo ametumwa na wapinzani kuvuruga umoja na chama chao.

Alimtuhumu kada huyo ya kwamba mara kwa mara amekuwa akijichukulia madaraka wakati si yake kwa kutoa matamko mbalimbali wakati yeye si msemaji wa chama wala jumuiya ya vijana wa chama hicho wilayani Arumeru.

“Ifahamike ya kwamba msemaji wa jumuiya yetu ni mwenyekiti, katibu na katibu hamasa,Mpumilwa sio msemaji wa chama, siku zote amekuwa akijichukulia madaraka ambayo si yake,” alisisitiza Pallangyo.

Hata hivyo, aliutaka uongozi wa CCM ngazi ya mkoa na taifa kwa ujumla kumwajibisha Mpumilwa kwa kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba ya CCM kwa kuwa amekuwa akikiuka maadili ya chama hicho.

Wakati huo huo, Milya ndani ya kikao hicho alisema kwamba chama chao kina uhakika wa kushinda uchaguzi katika jimbo la Arumeru Mashariki huku akisema kwa mafumbo kwamba  hata katika harusi mbalimbali nchini  wamekuwa wakiingia watu walioalikwa na wazamiaji.

Bila kuwataja wazamiaji na waalikwa ni akina nani, Milya alisema kwamba UVCCM imejipanga kikamilifu kupambana kwa lengo la kunyakua jimbo hilo kwa kuwa wanajiamini watashinda.

Hatahivyo, Mpumilwa amekaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akijibu mapigo kuhusina na tamko hilo la umoja huo huku akisema kwamba hatishiki kwa kuwa kikao kilichofanyika sio halali  kwani hata yeye hakuitwa kupewa nafasi ya kujibu madai yake



NJAA KALI


WANANCHI zaidi ya 5000 kutoka kata za Nduruma ,Mlangarini na Moshono katika Wilaya ya Arumeru na Moshono manispaa ya Arusha wanakabiliwa na njaa kali kufuatia kitendo cha Jeshi la Wananchi kuwazuia kufanya shughuli zozote katika ardhi wanayodai kuimiliki toka mwaka 1930. Katika Matangazo hayo wananchi hao hawaruhusiwi kulima ,kujenga nyumba na wala kuokota kitu chochote ndani ya maeneo hayo ambayo ni ya vijiji vilivyosajiliwa kisheria Hali kadhalika wananchi hao wamedai kunyimwa kuzika maiti za jamaa zao katika eneo hilo huku wengine wakishindwa kukarabati nyumba zao kutokana na hofu ya kuadhibiwa na askari wanaofanya doria katika eneo hilo ili kuhakikisha kuwa maagizo yao yanafuatwa. Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao walisema kuwa wametoa vilio vyao kwa muda mrefu kwa viongozi ambao walihidi kulifuatilia haraka lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika . “Tumeonewa na kudhulumiwa kwa kiwango cha kutisha,serikali yetu imetutendea vibaya kwa kushindwa hata kusikia kilio chetu katika muda wote tuliyopiga kelele za kuomba msaada ,haiwezekani jambo linalohusu maisha ya watu wengi namana hii likapuuzwa kwa kiwango hiki kwa sasa tunaomba mahala pa kuzika ndugu zetu katika vijiji vya jirani”alisema George Mollel mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiserian. Alisema kuwa baadhi ya wazazi wameshindwa kupeleka watoto wao shule kutoakana na kukosa fedha za kulipam karo ya shule . Kauli hiyo inaumgwa mkono na Mzee wa Nyangusi Laanyuni ambaye alisema kuwa watoto wake wamelazimika kuacha masomo kutokana na njaa na hali kuwa ngumu. “Mimi naiomba serikali iangalie kilio chetu, hawa watoto wasiposoma tutawapeleka wapi katika Dunia ya leo,wengi tumekosa karo. Naye mmoja wa watu waliochaguliwa katika kamati ya kufuatilia sula hilo Moses Loningo Kivuyo alisema kuwa hali ni mbaya na kwa sasa kitakachofuatia ni wananchi kuchukua sheria mikononi mwao kwa kukadi matangazo ya Jeshi na kungia katika mashamba yao na kufanya kazi za kilimo na uifugaji. “Kwa hali ilivyo kwa sasa tunapa serikali siku thelathini itoe tamkoa kuhusu mgogoro huu ,Jeshi letu la wananachi tunalipenda na kuliheshimu ,tunajua wanaotuvuruga ni baadhi ya viongozi wa serikali na Jeshi ambao wana masilahi na eneo hili kwa kjuwa Barbra ya reli inapita na kuna mabaki ya kiwanda cha nyama cha Tanganyika Packers”alisema. Alieleza kuwa jamii zao zimeshi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka zaidi ya zaidi ya temanini na kwamba jeshi lilifika katika maeneo hayo na kujenga ghala la kuhifadhi vifaa vyao katika eneo hilo katika miaka ya sabini. “Ndugu mwandishi cha kushangaza zaidi ni kwamba vijiji vyetu vimesajiliwa na kuandikishwa kisheria sasa leo badala ya serikali kuwataka wanajeshi wakae mbali ana ardhi yao wanakubali nguzo za matangazo ya kutunyima kufanya lolote tutaishije kama wanaitaka hii ardhi si wafuate taratibu na kutupa haki zetu kwa mujibu wa sheria “alihoji Kivuyo. Aidha Mollel alisema jambo la kusikitisha ni hatua ya halmashauri ya Arusha kufika katika maeneo yao kwa njia ya ulaghai na kufanya tathmini ya mali zao kwa njia ya hila. Alisema kuwa hakuna kiongozi yeyote wa kijiji wala kitongoji aliyeshirikishwa katika zoezi hilo lililofanyika oktoba 2010. Mwananchi mwingine Elias Ndakusa alisema kuwa watoto wake wameacha masomo kufuatia kushindwa kulipa karo ya shu le huku akisema lishe imekuwa ngumu kutokana na kuzuiwa kulima katika shamba lake. “Mimi nimezaliwa hapa mwaka 1953 niliwakuta babu zangu wnajeshi walifika hapa mwaka 1975 kujenmga maghala ya silaha lakini eneo hili sii mali yao kuna wakubwa ambao wanhitaji hili eneo kutokana na umuhimu wake kiuchumi”alisema Ndakusa. Mikael Meibaku alisema kuwa kwa sasa wamefika mwisho na kitakachofuata baad ya siku thelathini ni kuingia katika mashamba yao na kuanza kulima. “Ni afadhali hawa wanajeshi watuue tufe kuliko mateso haya





MILA POTOFU

Tabia ya kuwavalisha watu mifuko ya salphet (magunia) na mabati shingoni kwa madai kuwa wamekiuka Mila na Desturi za kabila la Kimaasai imechukuwa sura mpya tena baada ya Mzee wa boma Bw.Robert Elias pamoja na kijana wake Amani Robert kuvalishwa Magunia na kutembezwa usiku kucha huku wakiimbiwa nyimbo za matusi pamoja na kipigo wakidai kuwa wamekiuka Mila na taratibu za kabila hilo. Hayo yamejiri leo katika mtaa wa shams kata ya Elerai jijini hapa ambapo zaidi ya Vijana wa kimasai almaarufu (Koriyanga) Morani zaidi ya 30 walivamia boma la mzee Robert Elias na kumkamata kijana wake Amani Robert na kumvalisha magunia, huku wakimuimbia nyimbo mbalimbali za matusi za kabila hilo na baadae ndipo walifanikiwa kumkamata baba mzazi wa kijana huyo Baada ya vijana hao kumkamata baba huyo walimvalisha Magunia na kumtembeza mtaa mzima, akiwa amepakwa oili na kipigo juu akishurutishwa kulipa faini ya dume la ngombe na vipozeo vyake kwa madai kuwa wamekiuka mila na desturi za kabila hili Naye kijana mdogo wa mzee huo Emmanuel Robert alisema kuwa kutokana na imani yao ya kanisa la PEFA ambalo waumini wake ni walokole ndio maana wao wanafuata taratibu za imani yao ya dini hivyo wasihukumiwe kwani katiba ya jamuhuri inawapa watu uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria za nchi Aliendelea kusema kuwa anawashangaa sana watu wa kabila lao kwa kukiuka katiba na uhuru wa mtu kuabudu kwa visingizio vya mila na desturi jambo ambolo linahatarisha na kuwanyima fursa za kuishi na uhuru wa kuabudu "Baba yangu na familia yetu kwa ujumla ni walokole wa kanisa la PEFA na tunafuata mahubiri ya kanisa letu kama muongozo wa maisha yetu, tumeshangazwa na vitendo walivyofanyiwa familia yetu kwani vipo nje ya imani yetu"tuliona kaka yetu mnamo saa 7 mchana akivamiwa na baadae mnamo saa 2 usiku baba yetu naye alikamatwa na vijana wa kimila"alisema Emmanuel huku akitokwa na machozi Aliongeza kuwa wamewadhalilisha baba na kaka yake na kwa hili tunaomba serikali ichukue hatua za kisheria kwa vijana hao kwani wakiendelea kunaweza kutokea uvunjifu wa amani kwa jamii Tulipo mtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Bw.Thobias Andengenye kuzungumzia juu ya matukio haya ambayo yamechukuwa nafasi kubwa sana kwa watu kudhalilishwa utu wao na huku watuhumiwa wakikamatwa kutochukuliwa hatua zozote na kuachiwa huru na jeshi la polisi. Kamanda Andengenye alipopigiwa simu ya kiganjani alishindwa kupokea na hatimaye kutuma ujumbe mfupi kuwa yupo nje ya Mkoa Hata hivyo polisi walikuwepo eneo la Burka baada ya waliokiuka mila na desturi kutembezwa usiku kucha na asubuhi kufikishwa eneo hilo na ndipo vijana hao waliitwa na wazee wa kimila na kuzungumzia tukio hilo, ambapo jeshi la polisi walishuhudiwa wakituliza ghasia katika eneo hilo.







AJALI YAPOTEZA MAISHA 





ARUSHA                       JAN 24, 2012                       SAA 2 USIKU



Mtu mmoja aliyefahamika  kama Kombola Ngoyoo mkazi wa osterbay jijini Arusha  amefariki dunia papo hapo  mara baada ya kugongwa na gari  wakati akivuka barabara.

Kamanda wa polisi mkoa wa arusha kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Thobias Andengenye  amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa kumi na mbili jioni katika barabara ya Dodoma.

Kamanda ameongeza kuwa gari lenye namba za usajili T 780 AUN ambalo lilikuwa linaendeshwa na JOSEPH THOMAS MAKUMPA mkazi wa njiro lilikuwa likitokea maeneo ya kona Nairobi kuelekea Mbauda ndilo lililomganga marehemu.

Mara baada ya ajali hiyo dereva alikamatwa na na anaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani ambapo kamanda Andengenye amemtaja marehemu kuwa alikuwa mwalimu katika shule ya msingi Mecksons



................................................................................................................................................................... 



AJIUA KISA DOLA 1500








Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la John Justine(17) mkazi wa makao mapya amefariki dunia jana katika hospitali ya mount meru wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi. Akizungumza na wandishi wa habari kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa arusha Thobias Andeng'enye amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu jioni ambapo siku hiyo mama wa marehemu aitwaye Betty John alikuwa akitoka kwenye sherehe mara baada ya kufika nyumbani alikuta geti limefungwa ndipo alipowaomba majirani kumsaidia kufungua. Andeng'enye amesema kuwa mama huyo amesema kuwa mara baada ya kuingia ndani akiwa na mtoto wa jirani alimkuta mtoto wake akiwa chini amelala chini huku akihema kwa tabu huku damu zikimtoka kifuani ndipo alipotoka nje na kuomba msaada kwa majirani. Aidha kamanda alisema kuwa mma huyo pamoja na majirani walisaidina kumkimbiza hospitali ya Dkt.Mohamed iliyopo eneo la Tank la maji Ilboru kwa matibabu ambapo ilishindikana na kumpeleka hospitali ya mkoa ya mount meru ambapo ailipatiwa msaada lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia. Hata hivyo andeng'enye amesema kuwa baada ya polisi kituo kikuu wilaya kupata taarifa walikwenda eneo la tukio kufanya ukakuzi ambapo walikuta bunduki aina ya shortgun Pump Action pamija na ujumbe unaosema"ANASIKITIKA KULAUMIWA NA WAZAZI WAKE PIA ANAWAPENDA SANA" Vilevile walikuta michirizi ya damu kutoka chumbani hadi alipoangukia. Kamanda ameongeza kuwa inasemekana kuwa marehemu alituhumiwa na baba yake mzazi Jastine Kaizer kuwa aliiba fedha kiasi cha dola za marekani 1500 hivyo polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kumhoji baba mzazi wa marehemu . Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha mount meru ukisubiri uchunguzi zaidi wa daktari.








........................................................................................................................................................................

ZA MWIZI AROBAINI.
Mganga wa kienyeji Anna Loshirali aliyekuwa amemhifadhi
nyumbani kwake jambazi sugu ,na kumtibu majeraha akiwa chini ya
ulinzikwenye gari la polisi baada ya kumtia mbaroni.
Mmoja wa madakitari katika hospital ya mounti meru akiufanyia
uchunguzi mwili wa jambazi huyo

 kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye akionyesha baadhi
ya silaha zilizokuwa zikitumia na jambazi huyo baada ya kuzikamata eneo
la Kijenge alipokuwa amezificha jambazi huyo.
Mwili wa jambazi Sugu aliyeuawa ,Elipokea kayaa(45)

No comments: