Kamati kuu ya
chama cha mapinduzi CCM imetangaza kurejewa kwa kura ya maoni ili
kumpata mwakilishi wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa bunge katika jimbo
la ARUMERU MASHARIKI.
Katibu wa itikadi na uenzi wa CCM NAPE
N’NAUYE ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kikao cha
kamati kuu ,na kuwataja watakaohusika katika kura hiyo ya maoni hapo march mosi
,kuwa ni Sioi Sumari pamoja na Wiliam Sarakikya.
Kwa mujibu wa NAPE ,kamati kuu imeamua kuchukua uamuzi huo wa
kurejelewa kwa kura ya maoni kutokana na wagombea wote waliojitokeza katika
kinyang’anyiro hicho kutofikia zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
Hatua kama hii imekuwa ikitumika pindi
kunapotokea upinzani mkali baina ya wagombea huku idadi kubwa ya wajumbe
wakionekana kutomkubali mgombea
aliyeshinda.
Uamuzi huo uliwahi kutumika kuamua mgombea wa
nafasi ya urahisi kwa mwaka 1995 baina ya mwanasiasa mkongwe nchini CLEOPA
MSUYA ,rais wa awamu ya tatu BENJAMINI WILIAM MKAPA na rais wa sasa mh: dakta
JAKAYA MRISHO KIKWETE.
No comments:
Post a Comment