Kimataifa

UPINZANI WASHIKA HATAMU SENEGAL
RAIS wa Senegal Abdoulaye Wade (85), ameangushwa vibaya na mpinzani wake, Macky Sall (50) katika duru ya pili ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.
Matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na wananchi wa Senegal na hata hapa nchini wengi wakisema anguko hilo la Wade ni somo kwa viongozi ving’ang’anizi wa madaraka barani Afrika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wanasiasa, wasomi na wanaharakati nchini wamesema, anguko la Wade, linapaswa kuwa funzo kwa viongozi wanaokandamiza demokrasia katika nchi kadhaa barani Afrika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya alisema watawala wa Afrika wanapaswa kuheshimu uamuzi wa raia wanaotoa kupitia sanduku la kura.
“Wakati wa kuiba kura na kufanya hila nyingine ili mtu ashinde umepitwa na wakati. Kinachotakiwa ni kuheshimiwa kwa matakwa ya wananchi,” alisema na kuongeza: “Kilichotokea Senegal kinabainisha kuwa waliochaguliwa watakwenda kuwatumikia wananchi kwa kuwa hawakununua kura.”
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid alisema nchini kumekuwa na dhana kwamba upinzani una vurugu jambo ambalo alisema siyo la kweli isipokua hali hiyo inachangiwa na walio madarakani kutaka kuendelea kubaki hapo hata kama wananchi wanawakataa.
“Matokeo ya Senegal yanatufundisha kukubali kushindwa na kuwataka wanasiasa kuheshimu katiba,” alisema na kuongeza kuwa tume za uchaguzi zinapaswa kuacha demokrasia ikapata nafasi yake bila kuwafanya wengine kulazimika kutumia nguvu.
Mwenyekiti wa Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema alisema wananchi wamechoshwa na vyama vilivyokaa madarakani muda mrefu hivyo wanahitaji mabadiliko hata kama hayawapeleki wanapotaka.
Alisema watu wamechoshwa na vyama vya siasa vikongwe madarakani na wanapenda kuona mabadiliko hivyo ni wakati wa vyama vya namna hiyo ama kuachia ngazi au kuacha kura za wananchi zikaamua kwa kufuata misingi ya haki na demokrasia.
“Watu wamechoshwa na wapo tayari kwenda kwingine hata kama ni gizani,” alisema na kuongeza kuwa wale ambao wanahisi kuwa mfumo umewachoka ni vizuri wakakaa pembeni kwa heshima kuliko kusubiri kuondolewa kupitia masanduku ya kura.
Historia ya Wade
Kabla ya kuangushwa, Wade wa Chama Senegalese Democratic (PDS), tayari aliiongoza nchi hiyo kwa vipindi viwili mfufulizo tangu mwaka 2000 alipoingia madarakani na mwaka jana alibadili katiba ili aweze kugombea muhula wa tatu.
Senegal ambayo tayari ilikuwa ikinyemelewa na ghasia kutokana na Wade kubadili katiba, juzi ilipata Rais huyo mpya kutoka Chama cha Alliance for the Republic, baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 60 huku mkongwe huyo akiambulia kiasi cha asilimia 30.
Awali, taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Senegal zilisema  kulikuwa na jumla ya wapigakura zaidi ya milioni tano ambao waliandikishwa.
Ushindi huo wa Sall ambaye aliwahi kuwa mshirika kubwa kisiasa wa Wade ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya mkongwe huyo na Meneja wa kampeni iliyomuingiza madarakani kiongozi huyo mwaka 2000, umepokewa kwa nderemo na vifijo katika viunga vya jiji la Dakar na maeneo mengine nchini humo.
Hata hivyo, hadi jana jioni hakukuwa na taarifa rasmi za idadi ya wapigakura walioshirika katika duru hilo la pili la uchaguzi lililomng’oa Wade. Shirika la Habari la Serikali la Senegal (APS) lilitangaza kuwa Wade amekubali kushindwa na mpinzani wake huyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Wade alimpigia simu mpizani wake Sall na kumwambia kuwa amekubali kushindwa. Taarifa hizo za APS zilisema Sall aliripotiwa kukubali kuzungumza mara tu baada ya mpinzani wake kukubali kuwa ameshindwa.

Kabla na baada ya duru ya pili
Katika duru ya kwanza, uchaguzi ulifanyika baada ya maandamano na vurugu katika kampeni za uchaguzi baada ya Wade kutumia mamlaka yake kutaka kuendelea kuwepo madarakani kwa kipindi kingine.
Wananchi hao walianza kujikusanya na kufanya maandamano kwa lengo la kumtoa Wade madarakani. Baada ya matokeo ya juzi, maelfu ya wafuasi wa Sall walijitokeza katika barabara za Dakar wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao.
Miongoni mwa waliokuwa wakisherehekea ni Seynabou Seck ambaye alipohojiwa alisema: “Nimefurahi sana , Macky bado ni kijana na tena ni mtu mpole sana na ana heshima! Kwa hakika anastahili ushindi huu. Kila mtu alikuwa akimuombea ashinde.”
Akizungumzia ushindi wake, Sall alisema ni mwamko mpya kwa raia wa Senegal.
Katiba ya Senegal inaweka muda wa mihula miwili kwa rais kubaki madarakani na jaribio la Wade kuwania muhula wa tatu lilizusha maandamano na ghasia zilizosababisha vifo.
Wafuatiliaji wa kimataifa walisema uchaguzi huo ulifanyika kwa uhuru na amani ingawa polisi walirusha mabomu ya kutoa machozi nje ya kituo kimoja jijini Dakar.












 
WANAJESHI WATANGAZA MAPINDUZI MALI
 
Wanajeshi waasi wametangaza katika televisheni ya taifa ya Mali kuwa wamechukua udhibiti wa nchi, saa kadha baada ya kuvamia kasri ya rais.
Wanajeshi walioasi wanasema kuna marufuku ya kutotoka nje katika nchi nzima na kwamba katiba haitatumika kwa sasa

Siku ya Jumatano wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu kwa serikali.

Wanasema serikali haijawapa silaha za kutosha kukabiliana na waasi wa jamii ya Tuareg.

Tayari walikuwa wamechukua udhibiti wa kituo cha taifa cha redio na televisheni na kusitisha matangazo.

Baada ya saa kadha ya kuonyesha picha za nyimbo za wanamuziki wa Mali, kundi la wanajeshi likaonekana kwenye televisheni mapema siku ya Alhamisi, wakitambulishwa kama "Kamati itakayorudisha Demokrasia na kutuliza hali katika nchi".

Msemaji wa waasi hao, aliyetajwa kwa jina la Luteni Amadou Konare, alisema sasa wamemaliza "utawala usio thabiti" wa Rais Amadou Toumani Toure.
 



WAFANYAKAZI WATIMULIWA




Kenya’s public healthcare system was paralysed on Thursday after the government sacked the 25,000 striking health workers, including nurses.

They will be replaced by retired nurses and other health workers and interns, according to a government statement.

The blanket sacking was the culmination of seven days of protests by nurses, laboratory technicians, pharmacists and other health workers in government service demanding better terms of employment and working conditions.

In response to the announcement of their sackings, the nurses maintained that their strike was still on and that the government move was ill advised.

They held demonstrations in major towns and vowed to continue doing so until their demands were met.

The nurses want their extraneous allowance increased from the current Sh7,500 to Sh50,000 to be at par with doctors.

They also want non-practice allowance of Sh50,000, car allowance (night duty) of Sh40,000 and their uniform allowance increased from Sh10,000 to Sh40,000.

Announcing the sackings on Thursday, government spokesman Alfred Mutua said their names were removed from the payroll on Thursday and they will receive their dismissal letters soon.

“All illegal striking health professionals who defied the directive by Medical Services minister (Prof Anyang Nyong’o) to report to work have been dismissed,” Dr Mutua said in his address to the nation on Thursday.

“All qualified health professionals who are unemployed or retired are advised to report to the nearest health facility for interviews and deployment starting tomorrow (March 9, 2012),” Dr Mutua said.

He added: “The government has taken this firm action to alleviate further suffering of innocent Kenyans.”

“It is wrong, regardless of any disagreement, for a health professional to abscond duty and lead to loss of life or suffering.

“The government and indeed the people of Kenya will not tolerate this,” the government spokesman said.

Medical Services minister Peter Nyong’o confirmed that the health workers had been sacked for deserting work.

“They have absconded their duties leading to the suffering of Kenyans and the ministry could not tolerate it,” the minister said.



BRUSSELS                 
Viongozi wa Iran wamelaani vikali hatua ya umoja wa ulaya kupitisha azimio la kupiga marufuku nchi hiyo kusafirisha mafuta nje ya nje mpaka itakapoachana na mpango wake wa nyuklia.
Viongozi hao wameiita hatua hiyo kuwa ni vita vya kisaikolojia na wameimarisha vitisho vya kuufunga mlango bahari wa Hormuz.
Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa mjini Brussels amefafanua hatua hiyo ya umoja wa ulaya kupiga marufuku mafuta ya Iran akisema Iran hadi wakati huu inapinga kushirikiana na jumuiya ya kimataifa.
Naye Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa ulaya Bi Catherine Ashton amesema hatua hiyo inaitaka Iran irejee kwenye meza ya mazungumzo.
Wataalam wa kijeshi wameibua maswali ikiwa Iran ina uwezo wa kujaribu kuufunga mlango bahari wa Hormuz huku Marekani na washirika wake wakisema watachukua hatua ya haraka dhidi ya hatua zozote za Iran kuufunga mlango huo.

 .............................................................................


TRIPOLI               

Wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, marehemu Moammar Gadhafi wamefanya msururu wa mashambulizi katika miji kadhaa nchini humo.
Wapiganaji saba waliosaidia kuuangusha utawala wa Gaddafi waliuwawa ambapo mashambulizi yamefanywa katika maeneo tofauti ya mji wa kaskazini wa Benghazi, mji wa magharibi wa Bani Walid na mji mkuu Tripoli.
Msemaji wa kikosi cha mapinduzi amesema zaidi ya wapiganaji 150 waliomuunga mkono Gaddafi waliingia katika mapigano ya barabarani, wakitumia maguruneti ya kurushwa na roketi pamoja na bunduki aina ya AK 47.
Viongozi wapya wa Libya wangali wakijaribu kuondoa upinzani kutoka kwa wanajeshi waliomuunga mkono Gaddafi na wanajaribu kuiunganisha nchi hiyo baada ya miezi minane ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.


By Philip Magese


............................................................................


MELI YAZAMA ITALIA



Meli ya Costa Concordia imezama jana katika bahari ya pasifiki na kupoteza maisha ya watu watatu...bado waokoaji wanaendelea na shghuli za uokoaji,,,Taarifa zaidi sikiliza habari ya radio 5


..........................................................................................................................................................



 


Baada ya miaka saba ya uvamizi wa Marekani nchini Iraq, rais wa Barack Obama amethibitisha kuwa vikosi vyote vya marekani vitaondoka nchini humo mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa mujibu wa rais Obama, hatua hii itatimiza ahadi yake aliyoitoa baada ya kuingia mamlakani.
Hata hivyo wanajeshi elfu hamsini watasalia iraq kutoa mafunzo kwa vikosi nchini humo na kuwaelimisha kuhusu nyenzo za kupambana na ugaidi.
Taarifa zinaelza kwamba  baadhi ya wananchi wanahofia huenda mashambulizi yanayofanywa na makundi ya wapigajani yakaongezeka iwapo wanajeshi wa Marekani wataondoka.

Hata hivyo kuna  wasiwasi zaidi kuhusu ukosefu wa kuunda serikali miezi mitano baada ya uchaguzi kufanyika.
.................................................................................................................................................................




WASHINGTON;              


ABIDJAN;         
Televisheni ya taifa ya Ivory Coast imetangaza kuwa chama cha Rais Alassane Ouattara wa nchi hiyo kinaelekea kupata ushindi mutlaki katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika Jumapili iliyopita.
Matokeo hayo yanahitimisha rasmi mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast ulioibuka baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Rais mwishoni mwa mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa matokeo ya awalia ,,chama cha Rally of the Republicans kimepata viti 123 katika matokeo ya viti 228 yaliyotangazwa hadi hivi sasa katia ya viti 255 vya bunge.
Chama hicho kinafuatiwa na kile cha Democratic Party of Cote d'Ivoire ambacho kimepata viti 93, na wagombea huru wamepata viti 12.
Chama cha Rais wa zamani wa nchi hiyo anayeshikiliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai huko The Hague Uholanzi kimesusia uchaguzi huo.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS imesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki licha ya zoezi hilo kuhudhuriwa na idadi ndogo ya watu.
......................................................................................................................................................................



KINSHASA;                         
Marekani imeonya kwamba Uchaguzi wa hivi karibuni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulikuwa na dosari nyingi  na kusisitiza umuhimu wa  mchakato huo kutathminiwa tena upya.
Balozi wa Marekani nchini humo anasema kumekuwa na dosari kadhaa na kwamba  zoezi zima la uchaguzi lilikuwa na  ulikuwa na kasoro.
Balozi huyo amesisitiza kwamba  Marekani na wafadhili wengine kutoka nchi za Magharibi wanatoa msaada wa kiufundi kwa Congo ili kuchunguza kwa makini dosari zilizotambuliwa na waangalizi wa uchaguzi.
Matokeo rasmi yamempa Rais Joseph Kabila ushindi wa asilimia 49% dhidi ya asilimia 32% ya kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi.
...............................................................................................................................................................

KAMPALA;                        

Viongozi wa Kanda ya Maziwa Makuu wanaokutana mjini Kampala Uganda, wanatarajiwa kujadili tuhuma za uhalifu uliosababisha mauaji ya watu wengi katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini, mpakani mwa Sudan.
Mkurugenzi mtendaji wa mkutano wa kimataifa kuhusu Kanda ya Maziwa Makuu Bi. Liberata Mulamula, amewaambia waandishi wa habari kuwa wakuu hao watajadili uzito wa tuhuma hizo kuona kama ipohaja ya kupeleka tume ya kutafuta ukweli nchini Sudan.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton, ametangaza kuunga mkono mpango wa maendeleo wa nchi hiyo, akisema Marekani na washirika wake wako tayari kusaidia kudumisha na kukamilisha amani nchini Sudan Kusini
Majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile yameshuhudia mapambano ya kutumia silaha kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa kundi la SPLA kutoka Sudan Kusini.
.....................................................................................................................................................................
NEW YORK;       DESEMBA15, 2011     

       

Wakati  kuna  ripoti  za  majeshi  ya  Syria  kushambulia mji  wa  kati  wa  Hama,  katibu  mkuu  wa  umoja  wa mataifa  Ban Ki-moon  ameyataka  mataifa  yenye  nguvu duniani  kuchukua  hatua  kwa  ajili  ya  ubinadamu  dhidi ya  ukandamizaji   unaofanywa  na  utawala   wa  rais Bashar al-Assad.
Ban  amezungumza  mjini  New York wakati  alipolitumia  baraza  la  usalama  la  umoja  wa mataifa  taarifa  ya   baraza  la  umoja  wa  mataifa  la  haki za  binadamu  ambayo  inasema  kuwa  zaidi  ya  watu elfu 5,  wameuwawa  tangu  March  mwaka huu.
Hadi  sasa , Urusi  na  China  zimezuwia  juhudi  za mataifa  ya  magharibi  kwa  baraza  hilo  kutoa  shutuma dhidi  ya  Syria. 
Kundi  la  wanaharakati  wa  Syria wanaongalia   haki  za  binadamu  nchini  Syria   lenye makao  yake  nchini  Uingereza  limesema  kuwa  raia  21 wamepigwa  risasi  na  kufariki  na  majeshi  ya  serikali nchini  Syria  jana, ikiwa  ni  pamoja  na  watu  11  katika mji  wa  Hama.
......................................................................................................................................................................

ABUJA;               DESEMBA 14, 2011                   SAA 6 MCHANA

Watu kumi wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, katika mapigano yaliyotokea katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu waliokuwa na silaha wamevamia askari waliokuwa mjini humo ambapo wakazi wa mji huo walisikia milipuko na milio ya risasi.
Taarifa kutoka hospitali moja mjini humo imesema, watu waliokuwa na majeraha ya risasi wamepelekwa hospitali humo kwa matibabu.
Wiki iliyopita, watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha walimuua Inspekta wa Polisi wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, ambamo katika miezi iliyopita, milipuko ya mabomu na aina nyingine za mauaji imekuwa ikitokea mara kwa mara .
Mapema mwezi Novemba mwaka huu, wapiganaji wa kundi la kiislamu lenye itikadi kali la Boko Haram lilidai kuhusika na mashambulizi katika miji ya kaskazini ya Damaturu na Maiduguri na kuua zaidi ya watu mia moja.
......................................................................................................................................................................







GENEVA:              

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa licha ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria kupungua kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, lakini mtikisiko wa kiuchumi duniani huenda ukadumaza juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

WHO imesema katika ripoti yake ya kila mwaka kwamba takriban watu laki 6 na 55 elfu wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa malaria mwaka jana 2010.

Ripoti hiyo ya Shirika la Afya Duniani imebaini kuwa, asilimia 86 ya vifo hivyo vilivyosababishwa na malaria ni watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka 5.

Imeongeza kuwa, watu zaidi ya milioni 570 wapo katika hatari ya ugonjwa huo katika nchi za chini ya jangwa la Sahara barani Afrika.
Hata hivyo, WHO imepongeza kupungua kwa asilimia 50 maambukizi na vifo vinavyosababishwa na malaria katika nchi 11 za Afrika.



 ..............................................................................................................................................................


NAIROBI;    DESEMBA 13,2011   

           
Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametoa mwito kwa wananchi kuimarisha   utulivu na mshikamano ,ili kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao unafanyika bila matatizo.
Akiongea kwenye Maadhimisho ya miaka 48 ya uhuru wa Kenya, Rais Kibaki amesema Kenya itafanya mkutano wa taifa wa mshikamano na maafikiano kabla ya uchaguzi huo.
Ameongeza kwamba maandalizi mbalimbali ya uchaguzi yameanza kwa utaratibu, na ana matumaini kuwa serikali na wananchi watashirikiana ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uhuru, haki na kwa utulivu.
Amesisitiza kwamba, mwaka huu maendeleo makubwa yamepatikana katika kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa Kenya.
Rais kibaki pia amesema  Kenya itaendelea kusukuma mbele mageuzi na maendeleo katika kuhimiza masuala  ya siasa, uchumi na jamii nchini humo.

TUNIS:                     DESEMBA 13,2011              
Bunge la mpito la Tunisia limemchagua  daktari na mwanaharakati wa haki za binadamu Moncef Marzouki kushika wadhfa wa urais nchini humo.
Marzouki ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa seriklai iliyoondolewa madarakani ,alifungwa 1994 baada ya kumkosoa rais Ben Ali katika uchaguzi wa rais na kisha kuachiwa huru miezi minne baadae na kulazimishwa  kuishi uhamishoni Ufaransa.
Waangalizi wa nchi za magharibi wanamuelezea Marzouki kama asiyekuwa na msimamo wa kidini na kuweka mambo sawa katika chama chenye itikadi ya kiislamu ambacho kwa hivi sasa kinatawala nguvu ya kisiasa nchini humo.
Kiongozi huyo atahudumu mwaka mmoja, mpaka pale ambapo katiba mpya itaandikwa na uchaguzi mpya utafanyika.

NEW YORK:              DESEMBA 13,2011               
Umoja wa Mataifa hivi sasa unakadiria kwamba karibu watu elfu 5, wameuwawa nchini Syria tangu kuanza kwa vuguvugu la kupinga serikali ya nchi hiyo hapo Machi.
Akihutubia baraza la usalama la umoja huo Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametaja kiwango hicho kuwa  kisichovumilika .
Pillay ameongeza kwamba Zaidi ya watu elfu 14,  wanakadiriwa kuwekwa kizuizini, na wengine elfu 12na mia 4  wamekimbilia nchi jirani.
Wakati huohuo Wasyria wamefanya uchaguzi wa ngazi ya manispaa, ambao uligubigwa na vurugu hali iliyopelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wapiga kura.
Majeshi ya serikali yamekuwa yakipambana na makundi ya wanajeshi waasi, na kuongeza hofu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.