FA KURUDI MSIMU UJAO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limerejesha tena mashindano ya Kombe
la FA (TFF) kuanzia msimu ujao 2012/2013 ambapo bingwa wa michuano hiyo
ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Timu
zinazotakiwa kushiriki michuano hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa
mtoano ni zilizosajiliwa ambapo katika maombi yao ni lazima
ziambatanishe nakala ya hati ya usajili wa klabu ambayo itatakiwa
kuidhinishwa na chama cha mpira wa miguu cha wilaya.
Ada
ya fomu ya maombi ya kushiriki ni sh. 20,000 wakati ada ya mashindano
ni sh. 200,000. Usajili wa wachezaji katika Kombe la FA ni ule ule
mmoja wa kalenda ya usajili ya TFF ambapo unaanza Juni Mosi nakumalizika Septemba 10.
S IMBA KUJICHIMBIA EGYPT
KATIKA kuhakikisha
wanashinda mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya
ES Setif ya Algeria wiki ijayo, kikosi cha Simba kimepanga kwenda
kuweka kambi nchini Misri siku tano kabla kuelekea Algeria
katika mchezo wa marudiano.
Mwenyekiti wa Simba
Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa wanalazima kwenda mapema huko ili
kuweza kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kwa sasa Algeri kuna baridi
kali hivyo kwa kuwa Misri haitofautiani sana itakuwa ni vizuri kwa
kikosi chao.
Alisema kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida kujiandaa na michezo yake ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Katika mchezo wa kwanza
uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili, Simba iliwabanjua waarabu hao
mabao 2-0, huku mechi ya marudiano ikitaraji kupigwa ugenini kati ya
Aprili 5-8 mwaka huu.
KATIKA kuhakikisha
wanashinda mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya
ES Setif ya Algeria wiki ijayo, kikosi cha Simba kimepanga kwenda
kuweka kambi nchini Misri siku tano kabla kuelekea Algeria
katika mchezo wa marudiano.
Mwenyekiti wa Simba
Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa wanalazima kwenda mapema huko ili
kuweza kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kwa sasa Algeri kuna baridi
kali hivyo kwa kuwa Misri haitofautiani sana itakuwa ni vizuri kwa
kikosi chao.
Alisema kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida kujiandaa na michezo yake ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Katika mchezo wa kwanza
uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili, Simba iliwabanjua waarabu hao
mabao 2-0, huku mechi ya marudiano ikitaraji kupigwa ugenini kati ya
Aprili 5-8 mwaka huu.
MAN CITY OUT
MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City ya England imetolewa katika Europa League kwa hasara ya mabao ya ugenini licha ya ushindi wake wa jana usiku wa mabao 3-2 dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.
Matias Fernandez alifunga dakika ya 33 kwa mpira wa adhabu na Ricky van Wolfswinkel akafunga tena dakika ya 40 kuunenepesha ushindi wa Wareno wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza.
Ikihitaji mabao manne ili kusonga mbele, City ilionekana kama kuzinduka kwa mabao ya Sergio Aguero dakika ya 60 na 82, yaliyofuatiwa na bao la Mario Balotelli dakika ya 75 na kufanya sare ya jumla ya mabao 3-3.
Lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa uwezo wao kwenye Uwanja wa Eithad na mwanzo wa safari ya kuiaga michuano ya Ulaya mwaka huu.
“Ninajivunia kiwango, (lakini) nimestaajabishwa na mechi hizi mbili, kwa sababu nafikiri kwa mechi zote mbili, hatustahili kusonga mbele,” alisema kocha wa City, Roberto Mancini.
Matokeo hayo yanamaanisha England hawatakuwa na timu hata moja kwenye Robo Fainali ya michuano hiyo, kufuatia Manchester United kutolewa na Athletic Bilbao mapema jana.
BILBAO, Hispania
KLABU ya Athletic Bilbao imeishughulikia tena Manchester United na kuonyesha kwamba wanastahili ubingwa wa Europa League kufuatia ushindi mwingine wa mabao 2-1 usiku wa jana na kutinga Robo Fainali.
Kikosi cha makinda wa Basque, walianzia pale walipoishia kwenye ushindi wa 3-2 katika mechi ya kwanza kwa Fernando Llorente na Oscar de Marcos kufunga mabao mengine jana.
Wayne Rooney alifunga la kufutia machozi dakika ya 81 na kuiacha klabu hiyo ya Hispania isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-3.
“Sifikirii kama tutalalamikia matokeo haya,” alisema Ferguson. “Najaribu kuuchambua msimu huu (kwa Ulaya) kuufananisha na misimu mingine ni mgumu mno. Umekuwa ni mwaka wa maajabu.”
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wamejiimaarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Simba sasa wana pointi 44, baada ya kucheza mechi 20 wakati Azam ipo nafasi ya pili kwa pointi zake 41 baada ya kucheza mechi 20 pia, wakati Yanga iliyoifunga African Lyon 1-0 inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 40, ingawa imecheza mechi 19.
Bao pekee la Simba kwenye mchezo huo, lilitiwa kimiani na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Mutesa Patrick Mafisango. Bao la Yanga lilikuwa kama la kujifunga, kwani beki Hamisi Yussuf aliokoa mpira ukambabatiza kiungo Kiggi Makassy na kutinga nyavuni.
Azam itashuka dimbani Jumapili kucheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam, Chamazi, siku ambayo Simba watakuwa wakimenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
YANGA WAKIONA
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Dar es Salaam jana (Machi 12 mwaka huu) imetoa adhabu kwa klabu mbalimbali na wachezaji sita wakiwemo watano wa Yanga.
Villa Squad imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 122 dhidi ya Azam iliyochezwa Februari 15 mwaka huu Uwanja wa Chamazi.
Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa uwanjani kwenye mechi namba 129 dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Februari 19 mwaka huu Uwanja wa Manungu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 8(13) ya ligi hiyo.
Nayo Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi namba 132 dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu. Pia klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 25(d) baada ya kuoneshwa kadi kuanzia tano kwenye mechi hiyo.
Mchezaji Juma Mohamed wa Polisi Dodoma amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuwashambulia watazamaji kwa chupa ya maji katika mchezo namba 114 kati ya timu yake na Villa Squad uliochezwa Februari 11 mwaka huu.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga amefungiwa mechi sita za Ligi Kuu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi hiyo namba 132.
Wachezaji wengine wa Yanga walioadhibiwa kutokana na mechi hiyo ni Nurdin Bakari amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Omega Seme amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000, Jerryson Tegete amefungiwa miezi sita na faini ya sh. 500,000.
Stephano Mwasika amefungiwa mwaka mmoja na faini ya sh. milioni moja kwa kumpiga mwamuzi Nkongo. Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu.
Kamati ya Ligi imempongeza nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na mshambuliaji wa timu hiyo Hamis Kiiza kwa kuwa mstari wa mbele kuzuia wenzao kumshambulia mwamuzi. Pia imempongeza kocha Kostadin Papic wa Yanga kwa kukemea vurugu zilizofanywa na wachezaji wake.
Pia Kamati ya Ligi imeiagiza Sekretarieti kutoa waraka kwa makamishna wote wa ligi juu ya utaratibu wa wageni rasmi wakati wa mechi za ligi.
LIVER KUONDOA MKOSI LEO?
NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard amewataka wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Anfield kujituma haswa baada ya kupokea kipigo cha tatu mfululizo kutoka kwa Sunderland Jumamosi.
Wekundu hao hawajawahi kufungwa mechi tatu mfululizo tangu mwaka 2003, na kipigo hicho kinamuacha kocha Kenny Dalglish katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, pointi mbili tu dhidi ya wapinzani wao Everton watakaomenyana nao katika Merseyside derby Uwanja wa Anfield.
"Wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa hapa tulipo kwenye ligi," alisema Gerrard said. Si nzuri kiasi cha kutosha kwa klabu kama yetu kuwa huko. Tunatakiwa kutafuta kiwango kizuri na cha kudumu. Tunahitaji kufanya kweli na hakuna timu nzuri ya kuifanyia hivyo zaidi ya Everton.
Baada ya kutwaa Kombe la Ligi mwezi uliopita na kumaliza ukame wa mataji wa miaka sita, Liverpool imefufua matumaini ya kupigania Nne Bora katika Ligi ili icheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
MSHAMBULIAJI wa Schalke 04, Raul amechangia jezi yake na bao lake la 400 alilofunga katika kumbukumbu ya soka ya Ujerumani.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Raul alifunga bao hilo Februari 19 katika ushindi wa 4-0 kwenye Bundesliga dhidi ya Wolfsburg.
"Nimekuwa na wakati mzuri sana Bundesliga na ninajivunia sana heshima niliyopewa na mashabiki wa Ujerumani," alisema Raul, ambaye amefunga mabao 33 tangu ajiunge na Schalke majira ya joto 2010.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amefunga mabao 323 akiwa na Real Madrid, ambako alianzia soka ya kulipwa mwaka 1994, na alitwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Alifunga mengine 44 akiwa na timu ya taifa ya Hispania na 33 akiwa na Gelsenkirchen.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
KOCHA Jose Mourinho amepuuza madai kwamba anaweza kujiuzulu ukocha Real Madrid, iwapo timu hiyo haitafuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya CSKA Moscow ya Urusi.
Mchezo huo umekaa vibaya kufuatia matokeo ya sare ya 1-1 mjini Moscow, ingawa Real inapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano kesho kwenye Uwanja wa nyumbani, Santiago Bernabeu.
Mourinho amesema kwamba anahofia desturi ya mchezo kutobarika kuliko mustakabali wa kazi yake iwapo akifungwa.
"Mustakabali wangu hauwezi kuamuliwa na matokeo ya Jumatano, labda itokee klabu inifukuze tukishindwa kufuzu,"alisema Mreno huyo, ambaye klabu yake inaongoza Ligi Kuu Hispania ikiwazidi pointi 10, wapinzani wao na mabingwa watetezi, Barcelona.
"Lakini pointi yangu ya msingi ni kwamba, matokeo hayatabdili kitu. Mchezo wa kwanza ulikuwa na mkangayiko ambao unaacha nafasi wazi. Kuelekea kesho ninauhofia sana mchezo, ambao unaweza kutoa matokeo yoyote ya kustaajabisha."
Mourinho pia anaamini kupiga kwake kazi Chelsea na Inter Milan –aliowapa taji la Ligi ya Mabingwa na baadaye Bernabeu mwaka 2010 – itakuwa faida kwake kuelekea mchezo huo.
"Naifahamu CSKA tangu nikiwa Chelsea na Inter na ninafahamu ni timu inayokanganya kucheza nayo. Wanakufuata kwa kasi, wana mashambulizi makali ya kushitukiza na wana safu ngumu ya ulinzi. Lakini nafikiri tuna spana za kuwapiku."
Mourinho alipoulizwa kuhusu washambuliaji wake, Gonzalo Higuain aliyerudi kwenye fomu na Karim Benzema aliyekuwa majeruhi, alisema; "Nilikuwa nina matatizo wakati Higuain hakuwa kwenye fomu au Benzema alipokuwa majeruhi. Kwa sasa, tatizo hilo halipo tena," alisema Mourinho. "Kwa ujumla, kuwa nao wote ni jambo zuri linalowezekanaYANGA WAMD WAMDUNDA MWAMUZI YAADABISHWA 3-1
Wachzaji wa Yanga wakimpiga mwamuzi katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam Fc kwa taarifa zaidi fuatilia vi[pindi vyetu vya michezo hapa Radio 5
ZAMBIA WALIKUWA 22 UWANJANI

HAKUNA aliyekuwa akiipa nafasi Zambia kufanya vizuri katika Fainali za Afrika mwaka huu. Zambia ilikuwa ikicheza na Ivory Coast katika mechi ya fainali jana usiku.
Zambia iliingia fainali baada ya kuitoa Ghana iliyokuwa ikipewa nafasi kutwaa ubingwa kwa mara ya tano kwa kuilaza bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali katikati ya wiki iliyopita.
Lakini mwanzoni kabla ya kuanza fainali hizo, Zambia ilisema inakwenda Gabon ikiwa na mambo mawili. Kwanza kutaka ubingwa na pili kuwaenzi waliokufa katika mwambao wa Gabon 1993.
Wachezaji wote wa Zambia waliokuwa wanakwenda Senegal kucheza mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia, walikufa baada ya ndege yao kuanguka.
Ni miaka 19 imepita tangu Zambia kupata msiba mkubwa baada ya ajali ya ndege ya jeshi la nchi hiyo iliyotokea Pwani ya Gabon, kulikofanyika Fainali za Afrika zilizoandaliwa kwa pamoja na Guinea ya Ikweta.
Malengo ambayo kikosi cha sasa cha Zambia, Chipolopolo 'Risasi za Shaba' ni wazi imeyatimiza kwa kiasi kikubwa. Hakuna aliyetarajia kama wangeinia fainali zaidi ya Senegal, Mali, Ghana, Gabon na Ivory Coast.
Ni wazi kwamba wachezaji wa Zambia walikuwa na 'mizimu' ya wachezaji 23 waliokufa na walisema wanakwenda kuwaenzi. Wachezaji na viongozi wa timu hiyo waliweka mashada ya maua katika pwani ya Gabon mahali walipofariki wachezaji hao 23 katika ajali ile.
Katika ajali ile, abiria wote 30 ambao ni pamoja na watumishi watano wa ndege ile ya jeshi wakiwa safarini kwenda Dakar, Senegal kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani dhidi ya Simba wa Teranga (Senegal), walikufa.
Watumishi wa ndege:
Kanali Fenton Mhone, Luteni Kanali Victor Mubanga na Luteni Kanali James Sachika (wote ni marubani), Ofisa Mteule Edward Nambote (fundi) na Koplo Tomson Sakala ambaye ni mhudumu.
Wachezaji waliofariki, makipa: Efford Chabala na Richard Mwanza.
Mabeki; John Soko, Whiteson Changwe, Robert Watiyakeni, Samuel Chomba, Winter Mumba, Godfrey Kangwa na Kenan Simambe ambao ni mabeki.
Viungo ni Eston Mulenga, Derby Makinka, Moses Chikwalakwala, Wisdom Mumba Chansa na Numba Mwila.
Washambuliaji: Kelvin "Malaza" Mutale, Timothy Mwitwa, Moses Masuwa na
Patrick "Bomber" Banda.
Benchi la Ufundi liliundwa na Kocha: Godfrey "Ucar" Chitalu
Alex Chola, Wilson Mtonga (doctor) na Wilson Sakala
Wengi:Michael Mwape (Mwenyekiti FAZ), Nelson Zimba (mtumishi wa umma)
na Joseph Bwalya Salim (mwandishi wa habari).
Wachezaji wa Zambia waliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, kwamba mashindano ya mwaka huu ni kwa ajili ya kuwaenzi wenzao hao waliokuwa wanakwenda kutetea taifa la Zambia.
Wakizungumza kwenye ufukwe huo, walisema kuwa kuingia fainali, ni heshima pekee waliyoionyesha kwao kwani mataifa mengi yameshindwa kufuzu na hata kufikia hatua hiyo.
Zambia iliyomtimua kocha wake, Herve Renard kabla ya kumrudisha, ilikwenda India kujipanga kwa fainali hizo na ni wazi ilikuwa imejikamilisha kwa fainali za za mwaka huu.
Wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha mwaka huu cha Afcon ni makipa: Kalililo Kakonje na Kennedy Mweene (Free State Stars) na Joshua Titima wa Power Dynamos.
Mabeki: Kampamba Chintu (Bidvest Wits), Hichani Himonde, Stoppila Sunzu na Francis Kasonde (TP Mazembe), Christopher Katongo (Henan Jienye), Nyambe Mulenga (Zesco United), Joseph Musonda (Golden Arrows), Davies Nkausu wa SuperSport United.
Viungo: Isaac Chansa (Orlando Pirates), Noah Chivuta (Free State Stars),
Rainford Kalaba (TP Mazembe), Felix Katongo (Green Buffaloes), Chisamba Lungu (FC Ural), Clifford Mulenga (Bloemfontein Celtic), Jonas Sakuwaha (El Merreikh) na Nathan Sinkala wa Green Buffaloes.
Washambuliaji: Evans Kangwa (Nkana), James Chamanga, Dalian Shide
Emmanuel Mayuka (Zurich) na Collins Mbesuma wa Golden Arrows.
Ilitokea: Aprili 27, 1993
Chanzo: Kosa la rubani
Mahali: Bahari ya Atlantiki
Abiria: 25
Watumishi wa ndege: 5
Waliokufa: 30
Walionusurika: 0
Aina ya Ndege: De Havilland Canada DHC-5 Buffalo
Mmiliki: Jeshi la Anga Zambia
Namba yake: AF-319
Ilikoanzia safari: Lusaka, Zambia
Ilikotua awali: Brazzaville, Congo
Kituo kingine : Libreville, Gabon
Ilikokuwa ikienda: Dakar, Senegal
Watazamaji 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000.
Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh. 2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,861,000.
Gharama za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000, posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.
ZAMBIA NA IVORY COAST YASOGEZWA MBELE NUSU SAA
Muda wa kuanza kwa mchezo wa fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumapili utachelewa kuanza kwa nusu saaa kutokana na "matatizo ya kiufundi".
Mchezo wa fainali kati ya Zambia na Ivory Coast utakaochezwa mjini Libreville, uliokuwa uanze saa nne usiku saa za Afrika Mashariki, sasa utaanza nusu saa baadaye- saa nne na nusu usiku.
Shirikisho la Soka Barani Afrika Caf, halijatoa sababu yoyote zaidi kuhusiana na mabadiliko hayo.
Tiketi za mchezo wa fainali hazijafanikiwa kuuzwa zote kama ilivyotarajiwa, huku robo tatu ya tiketi hizo zikiwa hazijanunuliwa.
Waandaaji wamesema siku ya Jumatano kuwa asilimia 70 ya tiketi, zimeuzwa kwa ajili ya mchezo huo katika mji mkuu wa Gabon siku ya Jumapili.
Zambia itacheza mechi ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya tatu kwenye uwanja wa de l'Amitie, wakiwa wanatafuta kunyakua kombe la Afrika kwa mara ya kwanza.
Ivory Coast itakuwa ikitafuta ushindi kwa mara ya pili, miaka 20, baada ya kucheza na kushinda mechi ya fainali dhidi Ghana.
Timu hizo mbili zinakutana baada ya Chipolopolo kutoka Zambia kuichapa Ghana 1-0 mjini Bata, huku Ivory Coast wakiichapa Mali 1-0 mjini Libreville siku ya Jumatano.Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa jana Mali imeifunga Ghana 2-0
EVRA NA SUAREZ WAZUA GUMZO TENA
Luis Suarez kukataa kumpa mkono Patrice Evra kabla ya mechi kati ya Manchester United na Liverpool ndio jambo ambalo mashabiki wengi watalikumbuka katika mechi iliyochezwa Jumamosi uwanja wa Old Trafford, na ambayo wenyeji walipata ushindi wa magoli 2-1.
Suarez na Evra walikutana kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo ya ligi ya Premier, mara ya mwisho wakiwa uwanjani Anfield mwezi Oktoba, katika mechi ambayo mchezaji Suarez, kutoka Uruguay, alitamka maneno ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa ulinzi Evra, na ambayo yalisababisha kupewa adhabu ya kutocheza katika mechi nane.
Katika shughuli za kiutaratibu za wachezaji kupeana mkono, Suarez aliupuuza mkono wa Evra.
Evra alijitahidi kumsogezea mkono wake, lakini kabisa Suarez alikataa kabisa kuunyosha mkono wake.
Kutokana na hayo, mlinzi Rio Ferdinand naye alikataa kumpa mkono mshambulizi huyo wa Liverpool.
Lakini licha ya Suarez kuelekea kuonyesha utovu wa nidhamu, uwanjani Wayne Rooney aliweza kuifungia Manchester United magoli mawili katika muda wa dakika nne, kipindi cha pili.
Suarez alikuwa anaonekana wazi anakerwa na kukosa kupata bao, lakini Liverpool walipata nafasi ya kuondoka na bao moja, wakati Michael Carrick alipoadhibiwa kwa kucheza vibaya, na kufuatia mkwaju wa Charlie Adam kudunda baada ya kumgonga Ferdinand, Suarez alifunga bao.
Mchango wa Rooney katika mechi hiyo sasa umeiwezesha Manchester United kuwa kileleni katika ligi kuu ya Premier, huku jirani Manchester City ikisubiri kucheza na Aston Villa siku ya Jumamosi, na pengine kuweza tena kuendelea kuongoza ligi.
YANGA YAPIGWA BITI NA FIFA
Njoroge
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu.
Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu.
Njoroge ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake FIFA kupinga Yanga kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano. Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa Kenya.
Yanga ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo. Klabu hiyo inatakiwa iwe imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo. Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa mwaka ya fedha hizo.
Ikiwa Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi.
......................................................................................................................................................................
VIINGILIO MECHI YA TWIGA VYATANGAZWA
Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Pia kutakuwa na kiingilio cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 ambacho ni sh. 1,000. Watoto watakaotumia tiketi hizo wanatakiwa kuingia uwanjani wakiwa na wazazi au walezi wao.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 5,000 kwa VIP B na C n ash. 10,000 kwa VIP A.
Namibia inatarajia kuwasili nchini Ijumaa (Januari 27 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
...............................................................................................................................................................
YANGA YAZINDUKA
Mabingwa wa soka Tanzania Jana walifanikiwa kuwafunga Sofapaka ya Kenya 2-1 katika maaandalizi ya ligi ya mabingwa barani Afika,,Magoli ya Yanga yalifungwa na Hamis Kiiza Diego....kwa habari zaidi sikiliza sports ya radio5
...................................................................................................................................................................
Azam bingwa mapinduzi
Azam FC imefanikiwa kuchukua ubingwa wa mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba 3-1 katika mchezo wa fainali ya kombe la mpinduzi ilyopigwa uwanja wa Aman zazibar,Mabao ya Azam yamefungwa na John Boko ambaye pia alikosa penati,Said Morad na Mrisho Ngasa.
.................................................................................................................................................................
| TANZANIA FOOTBALL FEDERATION | |||||||||||
| Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA | |||||||||||
| Karume Memorial Stadium, Uhuru/ Shaurimoyo Rd – Ilala | |||||||||||
| P.O. Box 1574, Dar Es Salaam, Tanzania | |||||||||||
| Telefax: +255 22 2861815, Email: tfftz@yahoo.com, Website: www.tfftanzania.com | |||||||||||
| SECOND ROUND VODACOM PRIMIER LEAGUE | |||||||||||
| FIXTURE 2011/2012 | |||||||||||
| 21st JAN. 2012 - 05th MAY, 2012 | |||||||||||
| NO | DATE | No. | TEAMS | STADIUM | |||||||
| 14 | 21 Jan. 2012 | 92 | MORO UNITED Vs YANGA SC | U/Taifa | |||||||
| 21 Jan. 2012 | 95 | MTIBWA SUGAR Vs OLJORO | Manungu | ||||||||
| 21 Jan. 2012 | 94 | RUVU SHOOTING Vs TOTO AFRICAN | Mlandizi | ||||||||
| 21 Jan. 2012 | 95 | VILLA SQUAD Vs KAGERA SUGAR | Chamazi | ||||||||
| 22 Jan. 2012 | 96 | JKT RUVU Vs POLISI DODOMA | Chamazi | ||||||||
| 25 Jan. 2012 | 97 | AFRICAN LYON Vs AZAM FC | Chamazi | ||||||||
| 25 Jan. 2012 | 98 | SIMBA SC Vs COASTAL UNION | U/Taifa | ||||||||
| 15 | 28 Jan. 2012 | 99 | VILLA SQUAD Vs TOTO AFRICAN | Chamazi | |||||||
| 28 Jan. 2012 | 100 | JKT RUVU Vs YANGA SC | U/Taifa | ||||||||
| 28 Jan. 2012 | 101 | RUVU SHOOTING Vs KAGERA SUGAR | Mlandizi | ||||||||
| 29 Jan. 2012 | 102 | MORO UNITED Vs AZAM FC | Chamazi | ||||||||
| 29 Jan. 2012 | 103 | MTIBWA SUGAR Vs COASTAL UNION | Manungu | ||||||||
| 01 Feb. 2012 | 104 | AFRICAN LYON Vs POLISI DODOMA | Chamazi | ||||||||
| 01 Feb. 2012 | 105 | SIMBA SC Vs OLJORO | U/Taifa | ||||||||
| 16 | 04 Feb. 2012 | 106 | MORO UNITED Vs COASTAL UNION | Chamazi | |||||||
| 04 Feb. 2012 | 107 | VILLA SQUAD Vs SIMBA SC | U/Taifa | ||||||||
| 04 Feb. 2012 | 108 | RUVU SHOOTING Vs POLISI DODOMA | Mlandizi | ||||||||
| 05 Feb. 2012 | 109 | AZAM FC Vs OLJORO | Chamazi | ||||||||
| 05 Feb. 2012 | 110 | KAGERA SUGAR Vs JKT RUVU | Kaitaba | ||||||||
| 05 Feb. 2012 | 111 | TOTO AFRICAN Vs AFRICAN LYON | CCM Kirumba | ||||||||
| 08 Feb. 2012 | 112 | YANGA SC Vs MTIBWA SUGAR | U/Taifa | ||||||||
| 17 | 11 Feb. 2012 | 113 | TOTO AFRICAN Vs MORO UNITED | CCM Kirumba | |||||||
| 11 Feb. 2012 | 114 | POLISI DODOMA Vs VILLA SQUAD | Jamhuri | ||||||||
| 11 Feb. 2012 | 115 | COASTAL UNION Vs AFRICAN LYON | Mkwakwani | ||||||||
| 11 Feb. 2012 | 116 | OLJORO Vs JKT RUVU | Sh. Amri Abeid | ||||||||
| 11 Feb. 2012 | 117 | SIMBA SC Vs AZAM FC | U/Taifa | ||||||||
| 12 Feb. 2012 | 118 | KAGERA SUGAR Vs MTIBWA SUGAR | Kaitaba | ||||||||
| 12 Feb. 2012 | 119 | YANGA SC Vs RUVU SHOOTING | Chamazi | ||||||||
| 17-19 Feb. 2012 | CL & CC PRELIMINARY ROUND FIRST LEG | ||||||||||
| 18 | 15 Feb. 2012 | 120 | OLJORO Vs RUVU SHOOTING | Sh. Amri Abeid | |||||||
| 15 Feb. 2012 | 121 | TOTO AFRICAN Vs MTIBWA SUGAR | CCM Kirumba | ||||||||
| 15 Feb. 2012 | 122 | AZAM FC Vs VILLA SQUAD | Chamazi | ||||||||
| 15 Feb. 2012 | 123 | COASTAL UNION Vs JKT RUVU | Mkwakwani | ||||||||
| 15 Feb. 2012 | 124 | KAGERA SUGAR Vs MORO UNITED | Kaitaba | ||||||||
| 14 Mar. 2012 | 125 | POLISI DODOMA Vs SIMBA SC | Jamhuri | ||||||||
| 14 Mar. 2012 | 126 | YANGA SC Vs AFRICAN LYON | U/Taifa | ||||||||
| NO | DATE | No. | TEAMS | STADIUM | |||||||
| 19 | 19 Feb. 2012 | 127 | COASTAL UNION Vs RUVU SHOOTING | Mkwakwani | |||||||
| 19 Feb. 2012 | 128 | AFRICAN LYON Vs OLJORO | Chamazi | ||||||||
| 19 Feb. 2012 | 129 | MTIBWA SUGAR Vs VILLA SQUAD | Manungu | ||||||||
| 19 Feb. 2012 | 130 | POLISI DODOMA Vs MORO UNITED | Jamhuri | ||||||||
| 19 Feb. 2012 | 131 | JKT RUVU Vs TOTO AFRICAN | Chamazi | ||||||||
| 22 Feb. 2012 | 132 | YANGA SC Vs AZAM FC | U/Taifa | ||||||||
| 22 Feb. 2012 | 133 | OLJORO Vs KAGERA SUGAR | Sh. Amri Abeid | ||||||||
| 20 | 25 Feb. 2012 | 134 | POLISI DODOMA Vs KAGERA SUGAR | Jamhuri | |||||||
| 25 Feb. 2012 | 135 | MORO UNITED Vs JKT RUVU | Chamazi | ||||||||
| 26 Feb. 2012 | 136 | AFRICAN LYON Vs RUVU SHOOTING | Chamazi | ||||||||
| 26 Feb. 2012 | 137 | OLJORO Vs TOTO AFRICAN | Sh. Amri Abeid | ||||||||
| 03 Mar. 2012 | 138 | MTIBWA SUGAR Vs POLISI DODOMA | Manungu | ||||||||
| 29 Feb. 2012 | NATIONAL TEAM TAIFA STARS Vs MOZAMBIQ | U/Taifa | |||||||||
| 2-4 Mar.2012 | CL & CC PRELIMINARY ROUND SECOND LEG | ||||||||||
| 07 Mar. 2012 | 139 | SIMBA SC Vs KAGERA SUGAR | U/Taifa | ||||||||
| 07 Mar. 2012 | 140 | AZAM FC Vs COASTAL UNION | Chamazi | ||||||||
| 21 | 11 Mar. 2012 | 141 | SIMBA SC Vs TOTO AFRICAN | U/Taifa | |||||||
| 17 Mar. 2012 | 142 | VILLA SQUAD Vs YANGA SC | Chamazi | ||||||||
| 18 Mar. 2012 | 143 | TOTO AFRICAN Vs POLISI DODOMA | CC Kirumba | ||||||||
| 17 Mar. 2012 | 144 | COASTAL UNION Vs OLJORO | Mkwakwani | ||||||||
| 18 Mar. 2012 | 145 | AZAM FC Vs RUVU SHOOTING | Chamazi | ||||||||
| 18 Mar. 2012 | 146 | SIMBA SC Vs MTIBWA SUGAR | U/Taifa | ||||||||
| 21 Mar. 2012 | 147 | VILLA SQUAD Vs JKT RUVU | Chamazi | ||||||||
| 23-25 Mar.2012 | CL & CC 1/16TH FINAL FIRST LEG | ||||||||||
| 22 | 31 Mar. 2012 | 148 | COASTAL UNION Vs YANGA SC | Mkwakwani | |||||||
| 28 Mar. 2012 | 149 | MORO UNITED Vs AFRICAN LYON | Chamazi | ||||||||
| 28 Mar. 2012 | 150 | RUVU SHOOTING Vs MTIBWA SUGAR | Mlandizi | ||||||||
| 31 Mar. 2012 | 151 | AFRICAN LYON Vs SIMBA SC | U/Taifa | ||||||||
| 18 Apr. 2012 | 152 | KAGERA SUGAR Vs YANGA SC | Kaitaba | ||||||||
| 28 Mar. 2012 | 153 | MORO UNITED Vs VILLA SQUAD | Chamazi | ||||||||
| 01 Apr. 2012 | 154 | AZAM FC Vs RUVU JKT | Chamazi | ||||||||
| 06-08 Apr.2012 | CL & CC 1/16TH FINAL SECOND LEG | ||||||||||
| 23 | 15 Apr. 2012 | 155 | TOTO AFRICAN Vs YANGA SC | CCM Kirumba | |||||||
| 15 Apr. 2012 | 156 | RUVU SHOOTING Vs SIMBA SC | U/Taifa | ||||||||
| 14 Apr. 2012 | 157 | POLISI DODOMA Vs AZAM FC | Jamhuri | ||||||||
| 14 Apr. 2012 | 158 | MTIBWA SUGAR Vs JKT RUVU | Manungu | ||||||||
| 14 Apr. 2012 | 159 | KAGERA SUGAR Vs AFRICAN LYON | Kaitaba | ||||||||
| 14 Apr. 2012 | 160 | MORO UNITED Vs OLJORO | Chamazi | ||||||||
| 15 Apr. 2012 | 161 | VILLA SQUAD Vs COASTAL UNION | Chamazi | ||||||||
| 24 | 21 Apr. 2012 | 162 | AZAM FC Vs MTIBWA SUGAR | Chamazi | |||||||
| 18 Apr. 2012 | 163 | RUVU SHOOTING Vs MORO UNITED | Mlandizi | ||||||||
| 25 Apr. 2012 | 164 | OLJORO Vs YANGA SC | Sh. Amri Abeid | ||||||||
| 18 Apr. 2012 | 165 | JKT RUVU Vs SIMBA SC | U/Taifa | ||||||||
| 21 Apr. 2012 | 166 | KAGERA SUGAR Vs TOTO AFRICAN | Kaitaba | ||||||||
| 18 Apr. 2012 | 167 | POLISI DODOMA Vs COASTAL UNION | Jamhuri | ||||||||
| 18 Apr. 2012 | 168 | VILLA SQUAD Vs AFRICAN LYON | Chamazi | ||||||||
| NO | DATE | No. | TEAMS | VENUE | |||||||
| 25 | 22 Apr. 2012 | 169 | YANGA SC Vs POLISI DODOMA | U/Taifa | |||||||
| 29 Apr. 2012 | 170 | AZAM FC Vs TOTO AFRICAN | Chamazi | ||||||||
| 25 Apr. 2012 | 171 | SIMBA SC Vs MORO UNITED | U/Taifa | ||||||||
| 29 Apr. 2012 | 172 | COASTAL UNION Vs KAGERA SUGAR | Mkwakwani | ||||||||
| 25 Apr. 2012 | 173 | JKT RUVU Vs RUVU SHOOTING | Chamazi | ||||||||
| 28 Apr. 2012 | 174 | AFRICAN LYON Vs MTIBWA SUGAR | Chamazi | ||||||||
| 29 Apr. 2012 | 175 | VILLA SQUAD Vs OLJORO | Chamazi | ||||||||
| 26 | 05 May. 2012 | 176 | SIMBA SC Vs YANGA SC | U/Taifa | |||||||
| 05 May. 2012 | 177 | OLJORO Vs POLISI DODOMA | Sh. Amri Abeid | ||||||||
| 05 May. 2012 | 178 | RUVU SHOOTING Vs VILLA SQUAD | Mlandizi | ||||||||
| 05 May. 2012 | 179 | COASTAL UNION Vs TOTO AFRICAN | Mkwakwani | ||||||||
| 05 May. 2012 | 180 | AFRICAN LYON Vs JKT RUVU | Manungu | ||||||||
| 05 May. 2012 | 181 | AZAM FC Vs KAGERA SUGAR | Chamazi | ||||||||
| 05 May. 2012 | 182 | MORO UNITED Vs MTIBWA SUGAR | Jamhuri | ||||||||
| * Endapo timu za Yanga na Simba hazitafanikiwa kuvuka mzunguko w awali wa mashindano ya CL & | |||||||||||
| CC Orange 2012 ratiba itafanyiwamarekebisho. | |||||||||||
..................................................................................................................................................................
MESI MFALME WA SOKA KWA MARA YA TATU
Mchezaji wa Barcelona lionel Messi akiwa na Tuzo yake ya mwanasoka bora wa dunia.Mesi ametwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo sawa na raisi wa UEFA Michael Platini.....Sherehe hizo zilifanyika jijini Zurich Uswis ambapo kocha bora alikuwa Pep Guardiola wa Barcelona na goli bora likimuangukia Neymar wa Santos ya Brasil.
DOGO NENDA ULAYA
![]() |
Mwanasoka bora mara tatu duniani Ronaldo luiz Nazario de lima akiwa na mshindi wa goli bora la mwaka Neymar....Ronaldo amemwambia kinda huyo kuwa kama anataka kuwika kuliko Messi basi aende Ulaya
| ||||||||||||||||||||||||
MAN CITY YAIUA LIVERPOOL
LEO NI MAN UNITED vs NEW CASTLE
Yaya Toure pamoja na David Silva wakishangilia goli la pili katika mchezo ulioisha kwa the citizens kushinda 3-0.
USHINDI WA KWANZA
David Vaughan wa Sunderland akishangilia ushindi wa kwanza kwa Sunderland katika uwanja wa DW ambapo The cats walishinda 4-1.
HATUJISUMBUI
Ungozi wa liverpool umesema hautakata rufaa juu ya adhabu aliyepewa nyota wao Luis Suarez..Sarez anayechukiwa na waafrika wengi anakabiliwa na adhabu ya kutocheza mech 8 kwa kumuita mchezaji wa manchester united Patrice Evra ... "Nigrito"akimaanisha mweusi.
RATIBA INABANA
Kipa wa Arsenal Wojiech Schzeny amesem akufungwa kwao na Fullham kunatokana na ratiba ya ligi hiyo kuwa ngumu hivyo wao kucheza wakiwa wamechoka.....Wakati huo huo kipa huyo amedai kuwa nguli wa zamani wa timu hiyo Thiery Henry bado ni moto wa kuota mbali na bado anajua kufunga.
Hapa Thiery Henry akiwa na Theo Walcot na kinda wa kijapani Ryo Miyaichai aliyekuwa kwa mkopo FC Feynood ya uholanzi msimu uliopita katika mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Colney.
............................................................................................................................................................
Meneja wa Tottenham Harry Redknapp hana nia ya kuchukua nafasi ya umeneja wa timu ya taifa England "kwa wakati huu", kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy.
"Harry bado ana miezi 18 kabla mkataba wake haujamalizika. Kwa ninavyomfahamu Harry, hana tatizo hapa na hataki hata kufikiria kwa wakati huu kazi ya kuifundisha England," alisema Levy.
"Tutakuwa na wasiwasi iwapo suala hili litajitokeza wakati wa msimu ujao wa usajili."
Meneja wa sasa wa England Fabio Capello atamaliza mkataba wake mwishoni mwa fainali za michuano ya Euro mwaka 2012.
Redknapp awali aliwahi kusema kazi ya umeneja wa England "itakuwa vigumu kuikataa" na kuielezea kazi hiyo kama ni "lulu kwa atakayeipata".
Redknapp mwenye umri wa miaka 64 alichukua hatamu za kuifundisha Tottenham mwezi wa Oktoba mwaka 2008 wakati huo timu hiyo ikiwa na pointi nne kutoka eneo la kushuka daraja kwa msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England baada ya kuwa na wakati mgumu mwanzoni walipokuwa chini ya meneja kutoka Hispania Juande Ramos.
Amejitahidi kuinyanyua Spurs hadi kuweza kucheza michuano ya Ubingwa wa Ulaya msimu wa 2009-10.
Wakati huo huo meneja huyo wa Tottenham ameonywa achunge kauli zake siku zijazo kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Chris Foy walipofungwa na Stoke.
Redknapp alisema alikuwa na wasiwasi Foy "alikuwa akifurahia kutotupatia chochote" walipolazwa mabao 2-1.
........................................................................................................................................................
Kocha wa Barcelona Pep Guardiola amekanusha taarifa kuwa timu hiyo inatarajia kumuuza mshambuliaji wake David Villa katika kipindi cha uhamisho wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka ujao.
Gazeti la Marca limeripoti leo kuwa Barca ipo katika mipango ya kumuuza mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania kwa dau kubwa kutoka katika moja ya timu inayoshiriki ligi kuu ya England.
Marca limeripoti kuwa klabu za Liverpool na Chelsea zimeonesha nia ya kuihitaji saini ya nyota huyo,ambapo jioni hii Gurdiola amekanusha taarifa hiyo na kusema kuwa huo ni uzushi mtupu.
Villa(30)alijiunga na Barcelona akitokea Valencia kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 40 katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazimwaka 2010,na kwa muda mfupi ameweza kuwa kati ya wachezaji muhimu katika klabu yake.
Hata hivyo,Villa anapigania namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika kipindi cha msimu wa 2011-2012,hasa baada ya kuja kwa akina Alexis Sanchez na Cesc Fabregas.
Akiongea kwa hasira Guardiola amesema kuwa waliotoa taarifa za Villa wameupotosha umma,na kuongeza kuwa mkataba wa nyota huyo unamalizika 2014.
..................................................................................................................................
Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta amesema kuwa Catalan wana kila sababu ya kushinda Kombe la Vilabu Bingwa vya Mabara Duniani,huku akijinasabu kuwa kazi ya kwanza wanaianza kesho katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Al Sadd huko Japan.
Barcelona waliwasili Japan jumapili ya baada ya kutoka kumwadhibu hasimu wake Real Madrid katika mchezo wa La Liga ambapo waliibuka na ushindi wa goli 3-1.
Iniesta amesema kuwa tangu wawasili Japan mambo yanakwenda sawa sawa ikiwa ni pamoja na kuzoea hali ya hewa ya huko,ambayo ni tofauti na ile ya Hispania.
Amesema kuwa wapo tayari ingawa hali ya hewa ya Japan haizoeleki kwa haraka,na kuongeza kuwa kila kitu wanachokitumia huko ni tofauti kabisa na Hispania,ila wanajitahidi kuishi kulingana na hali ya mazingira yalivyo ikiwemo kulala mapema.
Ameongeza kuwa kwa sasa wameelekeza zaidi akili zao kwenye mchezo wa nusu fainali kesho dhidi ya Al Sadd,ambapo kila mchezaji ari kubwa na mchezo huo,na kila kitu kinakwenda sawa sawa.
Wamepanga kufanya vizuri katika kinyang`anyiro hicho ili waweze kuwa Mabingwa wa Kombe hilo lenye heshima kubwa kwa upande wa vilabu bingwa wa Mabara.
Mpaka sasa Barca wana pointi 37 katika msimamo wa La Liga wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Real Madrid huku wao wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen, anaetoka Nchini Denmark, ameliponda Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kwa kutomkabidhi Timu ya Tanzania Bara iliyocheza CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP na hivyo kumvurugia programu zake kwa ajili ya michuano ya Kimataifa Mwakani na pia kuwalaumu Mashabiki wa Tanzania kwa kuzomea Wachezaji wa Kilimanjaro Stars.
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, ilikuwa chini ya Makocha Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwenye michuano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP ambayo walipoteza Ubingwa wao na kumaliza nafasi ya 4.
Poulsen amesema kuwa kazi yake itakuwa ngumu zadi maana walitaka kujitayarisha mapema zaidi.
Inadaiwa TFF iliamua Timu ya Kilimanjaro Stars wapewe Makocha wengine kwa vile Jan Poulsen anafundisha Timu ambayo hujumuisha Wachezaji wa Zanzibar na kwa vile Kili Stars haikuwa na Wachezaji hao basi waliona bora kuwapa Wazalendo nafasi hiyo.
Kuhusu uchezaji wa Kili Stars kwenye Chalenji, Poulsen amesema kuwa walianza kwa udhaifu na hawakucheza vizuri kwenye Kundi lao na Robo Fainali ilikuwa poa, kwani walicheza kwa bidii dhidi ya Malawi na hata na Uganda lakini Uganda ni Timu bora.’
Kuhusu Mashabiki, Poulsen amesema kuwa ni makosa makubwa kuzomea Wachezaji kwa mashabiki siku zote lazima watoe sapoti kwa Wachezaji hata kama wanakuvunja moyo,ni wajibu kuwasapoti. Kama wewe ni Mtanzania lazima uisapoti Timu yako katika hali njema au mbaya! Huu haukuwa wakati mzuri kwa Soka la Tanzania lakini Mashabiki lazima waiunge mkono Timu yao!’
LONDON;
SPORTS 13/12/2011
Ule msemo wa muosha huoshwa,umejidhihirisha jana pale,Ile rekodi yao ya kutofungwa Msimu huu na majigambo yote yalikufa ndani ya Stamford Bridge licha ya wao Manchester City, vinara wa Ligi Kuu England, kuanza vizuri sana mechi ya jana usiku kwa kufunga bao Dakika 1 Sekunde 40 tu tangu mechi ianze kwa pasi ya Sergio Aguero kumkuta Mario Balotelli aliyepachika bao.
Lakini Chelsea wakajiinua na kujitutumua na kusawazisha bao Dakika ya 34 baada ya kazi nzuri ya Daniel Sturridge kwenye Winga ya kulia na krosi yake kuunganishwa vyema na Raul Meireles.
Kipindi cha Pili, huku Man City wakififia, Chelsea walikuja juu na presha yao iliwafanya Man City kucheza rafu bila mpango na hizo ndio zilisababisha Gael Clichy kula Kadi za Njano mbili na hatimaye kuwashwa Kadi Nyekundu Dakika ya 57.
Katika Dakika ya 82, Frank Lampard, alieingizwa Kipindi cha Pili, alitoa pasi safi kwa Daniel Sturridge ambae shuti lake lilizuiawa kwa mkono na Joleon Lescott na Refa Mark Clattenburg hakusita na kuashiria penati ambayo Lampard alipachika wavuni kwa shuti kali na kuwapa ushindi Chelsea wa bao 2-1.
Huo ukawa ndio mwisho wa majigambo ya Man City ya kuwa Timu pekee Ligi Kuu ambayo haijafungwa Msimu huu na pia kupunguza pengo lao la kuongoza kileleni kuwa pointi mbili tu mbele ya Mabingwa Manchester United.
Refa wa mchezo huo alikuwa Mark Clattenburg
MILAN 13/12/2011
Clarence Seedorf amesema kuwa hafikirii kama Carlos Tevez anaweza kujiunga na AC Milan kwasababu nyota huyo anapenda kujiunga na klabu ambayo itamwahidi kitita kikubwa cha ngawira.
Manchester City wamepanga kumtoa Tevez katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi Januari,kwa vilabu kati ya AC Milan na Paris Saint Germain ambazo kwa pamoja zimeonesha nia ya kuihitaji saini ya nyota huyo.
City imeonekana kutoridhishwa na deal la AC Milan ya Italia ambayo inamtaka nyota huyo kwa mkopo,zaidi imevutiwa na ofa ya PSG ya Ufaransa ambayo imeahidi kumlipa mshahara mnono tofauti na ule alioahidiwa AC Milan.
Seedorf amesema kuwa kamwe hatarajii kama Tevez ambaye yupo nyumbani kwao nchini Argentina anaweza kujiunga San Siro mwezi Januari.
Ameliambia Sky Sport Italia kuwa hofu zaidin ya kuinasa saini ny nyota huyo inaongezeka zaidi kutokana na wakala wa mchezaji huyo ambaye aanaonekana kuweka masharti magumu ikiwemosuala la mshahara mkubwa kwa timu ambayo inamwitaji nyota huyo.
Seedorf ameongeza kuwa hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya maisha ya Milan kumhitaji mchezaji kwa mkopo bila ya kumwaga mbumba,na kusema kuwa kwa sasa wanasubiri nini kitakachotokea.
SPORTS 13/12/2011
Tayari Timu 15 zina uhakika wa kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI na bado zipo Timu 19 zenye matumaini ya kunyakua nafasi 9 zilizobaki ikiwa zitapata matokeo mazuri kwenye mechi za mwisho za Makundi zitakazochezwa Jumatano Desemba 14 na Alhamisi Desemba 15.
Timu hizo 24 toka Makundi ya EUROPA LIGI zitajumuika na Timu 8 zilizomaliza nafasi ya 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ili kufanya idadi ya Timu za Raundi ya Pili ya Mtoano ya EUROPA LIGI kuwa 32.
Timu 3 za England tayari zimeshajijua kama ziko kwenye Raundi hiyo ya Pili na nazo ni Stoke City iliyofuzu kutoka Makundi ya EUROPA LIGI na zile Klabu za Manchester, Manchester United na Manchester City, ambazo zilitupwa kutoka UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kumaliza katika nafasi za 3 za Makundi yao na hivyo kutumbukizwa EUROPA LIGI.
Timu hizo 8 kutoka UEFA CHAMPIONZ LIGI ni:
-FC Porto [ambao ni pia ni Mabingwa Watetezi wa EUROPA LIGI]
-Manchester City FC
-Trabzonspor AŞ
-Manchester United FC
-AFC Ajax
-Valencia CF
-Olympiacos FC
-FC Viktoria Plzeň.
Droo ya kupanga mechi za Raundi ya Pili ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI pamoja na Raundi ya Tatu ya Timu 16 itafanyika Makao Makuu ya UEFA huko Nyon, Uswisi hapo Ijumaa Desemba 16.
SPORTS 13/12/2011
Klabu ya Celtic ya nchini Uskochi imesema kuwa haitarajii kukata rufaa ya kupinga faini waliyopewa na UEFA mwezi uliopita katika mchezo wa ligi ndogo ya UEFA dhidi ya Rennes katika uwanja wake wa nyumbani wa Celtic Park.
UEFA imeitwanga rungu la kulipa euro 15,000 ambazo ni sawa na pauni 12,700 ikiwa ni kuipa nidhamu timu hiyo licha kuibuka mshindi wa goli 3-1 dhidi ya Rennes November 3.
Mkurugenzi Mtendaji wa Celtic,Peter Lawwell ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa licha ya adhabu hiyo kuwa kubwa,hii inaonesha kuwa UEFA wameamuamua kuwa serious katika mambo mbali mbali yasikuwa ya kiungwana michezoni.
ARSENAL YAPATA PIGO

Beki wa kushoto wa arsenal mbrazil Santos aliyeumia katika mechi ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Olimpacos ya Ugiriki atafanyiwa opereshen na hivyo kuwa nje kwa kipindi cha miezi mitatu.
Santos anaongeza idadi ya majeruhi ndani ya kikosi hicho kilicho katika fomu kwa sasa akiwafuatia Carl jecknson,Kieran Gibbs,Bacary Sagna pamoja na kiungo Jack Willshere.





















