Burudani


KAJALA BADO
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili Msanii wa Filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo jana ulishindwa kuleta hati ya mashtaka iliyofanyiwa marekebisho kama ulivyoamriwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wiki iliyopita kwa madai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi juzi hakuweza kupatikana ofisini kwake ili aweze kutoa kibali.
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mussa Hussein,  aliikumbusha mahakama hiyo kuwa, kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya upande wa jamhuri kuleta hati ya mashtaka iliyofanyiwa marekebisho, lakini ameshindwa kufanya hivyo kwa sababu juzi, DDP Dk. Feleshi hakuwepo ofisini kwake ili aweze kutoa kibali cha kuletwa hati hiyo mahakamani, kwa hiyo wanaomba wapewe siku moja waweze kutekeleza hilo.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, alikataa hati hiyo isiletwe leo na badala yake, hati hiyo iletwe Machi 26 mwaka huu kwa ajili wa washtakiwa kusomewa upya mashtaka hayo na akaamuru mshtakiwa arudishwe rumande, uamuzi ambao ulikubaliwa na wakili huyo wa Takukuru na wakili wa Kajala, Alex Mgongolwa.
Machi 15 mwaka huu, Kajala na mumewe, ambaye pia yupo gerezani anakabiliwa na kosa la utakatishaji fedha haramu katika kesi nyingine, ambako kwa mujibu wa sheria, kosa hilo halina dhamana.







MISS WORLD YABADILISHIWA RATIBA 
 
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu shindano la Miss tanzania Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mabadiliko ya mashindano hayo, kushoto ni mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye na kulia ni Mshauri wa kamati hiyo, Dk.Ramesh Shah



PRESS RELEASE


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

15 MACHI 2012
MABADILIKO YA KALENDA YA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA:


Katika mkutano wa mawakala wa wanaoandaa mashindano ya urembo kutoka nchi mbalimbali duniani uliofanyika London Uingereza mwezi Novemba 2011, Tulijulishwa mabadiliko ya Kalenda ya mashindano ya urembo ya dunia. [Miss World.]

Mashindano ya urembo ya Dunia yanatarajia kufanyika mwezi August 2012 nchini China, badala ya mwezi Novemba/ Desemba kama ilivyozoeleka, ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali watatakiwa wawe wamefika nchini China mwezi Julai 2012.

Kutokana na hali hiyo tunalazimika kubadilisha kalenda ya mashindano yetu kama ifuatavyo:-


1. Tutatuma Mwakilishi atakayeshiriki mashindano ya urembo ya Dunia Miss World 2012.

2. Mwakilishi huyo atapatikana kwa njia ya usaili. Ambapo warembo watakaojitokeza

katika usaili huo watafanyiwa mchujo na kupatikana idadi ya warembo 10 watakao

panda jukwaani katika tafrija ndogo ili kumpata Mwakilishi ambaye atabeba Bendera ya

Tanzania katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia 2012.

3. Tunaomba warembo wote wenye sifa na nia ya kushiriki katika mchujo wa usaili

wawasiliane na ofisi zetu au Mawakala wete popote Tanzania kupata maelezo zaidi.


Mchakato wa mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida na Mshindi wa Redds Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi yetu katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, akiwa na muda wa miezi [7] saba ya maandalizi.

Hii inakidhi haja na maoni ya Wadau wa fani ya urembo ya kumpa muda wa kutosha Mrembo wa Taifa kujiandaa vya kutosha kabla ya kushiriki Fainali za dunia.

Lundenga

HASHIM LUNDENGA.

MKURUGENZI.



KILI MUSIC AWARD ZATANGAZWA
Dar es Salaam, Leo Jumatano 08 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia

yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania

(BASATA) leo wametangaza rasmi wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tuzo za Muziki



Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya

Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na

kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri na

zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2011”.



Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX

ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George Kavishe aliongeza

“Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo zitaendeshwa kisasa na

kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki

nchini. Tunaendeleza ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi

hili la Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.”



Kura za wana Academy ni siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro

hubaki siri ya INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi

za washindi.

Hatua zifwatazo:

1. Semina ya Wasanii:

Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina elekezi kuhusu tuzo hizi na

kupata nafasi kuuliza maswali juu ya mchakato mzima wa kupata wateule na

taratibu zitakazofwata.



2. Kura.

Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb - 06/ Apr Maelekezo

ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro www.kilitimetz.com na

mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya magazeti na vipindi mbali

mbali ya redio na TV.



3. Usiku wa utoaji Tuzo.

Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012

katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na

TV mbali mbali.



Walioteuliwa majina na kundi la Mtumbuizaji Bora wa Kike Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Queen Darleen, Dayna na Shaa.Mtumbuizaji Bora wa Kiume, Diamond, Ally Kiba, Bob Junior, Dully Sykes na Mzee Yussuf.

Mwimbaji Bora wa Kiume Ally Kiba, Diamond ,Barnaba, Belle 9 na Mzee Yussuf. Mwimbaji Bora wa Kike Lady Jaydee, Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Dayna na Linah.



Wimbo Bora wa Taarab Full Stop ulioimbwa na Khadija Kopa, Mamaa Mashauzi wa Isha Mashauzi,Hakuna Mkamilifu wa Jahazi, Nilijua Mtasema, Wimbo Bora wa Mwaka jina na aliyeucheza katika mabano ni Hakuna (Suma Lee), Dushelele (Ally Kiba), Moyo Wangu (Diamond), Mathematics (Roma), Nilipe Nisepe (Belle 9) na Riz One (Izzo B).



Katika kundi la kuwania tuzo ya Wimbo Bora ya Kiswahili uliopigwa na bendi waniwa na Dunia Daraja (The Africa Stars), Hukumu ya Mnafiki (Mashujaa Band), Falsafa ya Mapenzi na Mtenda zote (Extra Bongo) na Usia wa Babu (Mapacha Watatu).



Wimbo Bora wa R&B unawaniwa na nyimbo za My Number One Fan (Ben Pol), Maumivu (Ben Pol ft One), Nilipe Nisepe(Belle 9), Napta Raha (Jux) na Usiniache (Hemed). Wimbo Bora wa Hip Hop wanaowania ni Famous (Jay Mo ft P Funk), King Zila (Godzilla ft Marco Chali), Mathematics (Roma), Riz One (Izzo B), Kilimanjaro (Joh Makini ft Lady Jaydee, G Nako),Wimbo Bora wa Reggae Mazingira (Malfred ft Lutan Fyah),Arusha Gold (Worrior from the East), Give it Up to me(Delyla Princess), Nia Yao (20%), Ni Wewe (Nakaaya).



Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall unawania wan a Goo Look (A.Y ft Miss Trinity), Maneno Maneno (Queen Darleen ft Dully Sykes), Ganja Man (Dabo), Kudadeki na Poyoyo (Malfred). Rapa Bora wa mwaka bendi wamo Kalidjo Kitokololo, Khalid Chokoraa, Msafiri Diouf na Totoo Ze Bingwa, Msanii Bora wa Hip Hop ni Godzilla, Roma, Izzo B, Joh Makini na Fid Q.



Kwa upande wa tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki inawaniwa na Kigeugeu (Jaguar)Chokoza (Avrill na Marya), Mulika Mwizi (Kidumu ft Sana), Coming Home (Nameless) , 4sho4shizzle (Prezzo) na Valuvalu (Jose Chameleon).



Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka inawaniwa na Diamond, Ali Kiba, Mzee Yussuf, Barnaba na Belle 9.Huku tuzo ya Mtayarishaji Bora (Producer) wa mwaka inawaniwa na Marco Chali,Pancho Latino, Bob Junior Maneck na Man Walter.



Video Bora ya Muziki ya Mwaka zinazochuana ni Moyo Wangu (Diamond), Hakunaga (Suma Lee), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Ndoa Ndoana (Kassim Mganga ft Mr. Blue) na Bongo Fleva (Dully Sykes).



Wimbo Bora wa Afro PopHakunaga (Suma Lee),Bongo Fleva (Dully Sykes), Moyo Wangu na Mawazo (Diamond) na Nai Nai (Ommy Dimples).Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba Daima Milele (Barbanaba), Dushelele (Ally Kiba), Nivute Kwako (Dyna ft Barbanaba),Wangu Lady Jaydee ft Mr. Blue) na Kizunguzungu (Recho).



Wimbo Bora wenye vionjo vya Kiasili unawaniwa na Bao la Kete (AT),Kidudu Mtu (Offside Trick ft Baby J), Vifuu Tundu (A.T ft Mwanne), Mwanadamu (Ashimba) na Tunapeta (Young Dee ft Kitokololo na Mataluma).Msanii Bora Anayechipukia Ommy Dimpoz, Darasa, Recho, Abdul Kiba na Beatrice a.k.a Nabisha. Wimbo Bora wa Kushirikiana ni Famous (Jay Moe ft P-Funk Majani), King Zilla (Godzilla ft Marco Chali), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Kama ni Ganster (Chegge, Tembaft Ferouz) na Nai Nai (Ommy Dimpoz ft Ally Kiba).








FUNIKO BASE; 
by
Kamafa 4ever

Tamasha la Majahazi na ujio wa 2012 waiva
Lile tamasha la filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) imeandaa MINI ZIFF RED CARPET katika ukumbi wa New Maisha Club siku ya Jumapili tarehe 22 Januari 2012. Wasanii mbali mbali maarufu wa filamu za Kitanzania (Bongo Movies), wasanii maarufu wa Bongo Fleva na wadau mbali mbali wa sanaa nchini wataalikwa kupita katika Red Carpet.
Wasanii wote maarufu wa Bongo Movies na Bongo Fleva watahudhuria katika RED CARPET jumapili hii pale New Maisha Club na baada ya hapo kutakua na onesho maalum ambapo kwa mara ya kwanza ZIFF imeweza kuwaweka wasanii AT na Offside Trick katika jukwaa moja.
MINI ZIFF RED CARPET inaandaliwa kufungua kampeni ya “ Nunua kazi halisi ya msanii wa nyumbani ili kukuza tasnia ya sanaa nchini/Buy Original Product of our Artists to support the Development of Arts in Tanzania". ZIFF imeona umuhimu wa kuanzisha kampeni hii ili kusaidia kusambaza ujumbe huu na uwafikie watanzania wote ambao wengi wao wamekua wakinunua kazi zisizo halisi (Pirated Copies) na hivyo kuwanyima mapato wasanii ambao wamekua wakijitahidi katika kujikwamua kimaisha na kukuza tasnia nzima ya sanaa hapa nchini.

Katika Red Carpet ZIFF itatoa tuzo maalum (Nishani- Medal) kwa Kampuni bora iliyotoa mchango mkubwa kwa sanaa ya filamu Tanzania kwa mwaka 2011, Muigizaji bora wa kiume kwa 2011, mwigizaji Bora wa kike kwa 2011, filamu bora kwa mwaka 2011 na muugizaji bora anayechipukia. Tuzo hizi zitatolewa katika RED CARPET siku hiyo baada ya Kamati maalum (Panel) ya watu kumi watakaoteuliwa kufanya zoezi maalum la kuchagua watakopata tuzo hizo kutokana na kufanya kazi zao vizuri. Kamati (Panel) hiyo itaundwa na wadau wa karibu wa Bongo movies na watatoka katika vitengo au mashirika mbali mbali.
Pia MINI ZIFF itaendelea Ngome Kongwe Zanzibar tarehe 27 na 28 Januari, 2012, tutaonesha filamu za Kiswahili (Bongo Movies) sita katika screen kubwa ya Amphitheatre kuanzia saa moja usiku na filamu zitakazo oneshwa ni Mr.President ya Steve Nyerere, Big Daddy ya Kanumba, Pamoja ya Pastor Myamba, Dj Ben ya J.B, na filamu mpya toka CL& CY production.
Filamu zitaoneshwa bure siku ya Ijumaa ya tarehe 27, tarehe 28 Jumamosi itaoneshwa filamu moja na kufuatiwa na maonesho ya mavazi kutoka kwa Lucky Creation na Mgece Makory baada ya hapo tamasha hili dogo litafungwa na burudani kutoka kwa AT na Offside Trick kwa kiingilio cha shilingi 3,000/= tu.
==================================================================================


50 CENT ATANGAZA KUTOA ALBUM MBILI MPIGO NDANI YA MWAKA HUU 2012
Rapa kutoka pande za Obama land mtumzima 50 Cent  ametangaza kureleas albam mbili kwa mpigo ndani ya mwaka huu wa 2012, 50 amesema mashabiki wake waliokuwa wanasubiri ujio wa albam moja ya 50 sasa wakae tayari kwa ujio wa album mbili kwa mpigo, 50 ambaye hajatoa album kwa miaka mitatu mfululizo bado hajasema anazitoa lini album hizo, 50 aliyasema hayo katika interview na forbes nakuongezea kuwa kazi zote hizo atazifanya chini ya lebo yake mwenyewe ya interscope recods


===================================================================

RAPA RICK AKATAA MTOTO
Rapa muazilishi na kiongozi wa lebo ya Mybach Music Group (MMG) mtumzima Rick Ross amepata tuhuma nzito kutoka kwa mwanadada Tyrisha ambaye anadai kuzaa na rick, Mwana mama huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka pande za Georgia amesema  mtoto huyo mwenye umri wa miaka 3 hajawahi kupata kitu chochote kutoka kwa babake rick ross hivyo mwana mama huyo amemtaka rick kutoa kiasi cha dolla za kimarekani  $694  ambazo ni sawa na milion moja na elfu arobaini na moja (1041000) za kibongo, kwa upande wa Rick amesema hayuko tayari kuanza uduma kwa mtoto huyo mpaka pale vipimo vya DNA vitakapo thibitisha kuwa kweli ni mtoto wake











.................................................................................................................................................................









SIONDOKI TWANGA 
Kupaza



MWANAMUZIKI nguli wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Saleh Kupaza 'Mwana Tanga' amesema kuwa hana mpango wa kuihama bendi hiyo. Kupaza ambaye ni Kiongozi Msaidizi wa Twanga Pepeta akimsaidia Luiza Mbutu, amesema kamwe hawezi kurubuniwa akaiacha Twanga Pepeta na kuhamia bendi yoyote nchini. Akizungumza Dar es Salaam leo, Kupaza alikanusha uvumi kwamba ana mpango wa kufuata nyayo za mwenzake, Charles Gabriel 'Chaz Baba', aliyetua Mashujaa Musica kwa dau la sh. milioni 10 na gari aina ya Noah. "Nimekuwa nikisikia uvumi kwamba mimi na wenzangu, Miraji Shakashia 'Shakazulu' na James Kibosho tunatakiwa Mashujaa... lakini hakuhakikishia miongoni mwetu hakuna mwenye mpango huo. "Nipo Twanga Pepeta kwa ajili ya kulinda heshima ya bendi nikishirikiana na wenzangu... hao wanaosema Twanga itakufa wanajidanganya, tumejipanga vizuri sana," alisema Kupaza ambaye ni mtunzi hodari na mwenye sauti ya kipekee isiyoigika kirahisi. Mbali ya Kupaza kuhusishwa na mipango ya kudaiwa kusakwa na Mashujaa, pia kuna minong'ono kuwa anawaniwa na bendi ya TOT Plus iliyo chini ya Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, huku kila moja ikimtaka kwa dau kati ya sh. milioni 15 na sh. milioni 20. Hata hivyo, Kupaza alisema yeye bado ana mkataba aliosaini wa miaka mitatu na Twanga Pepeta, na kwamba anauheshimu, na hata isingekuwa hivyo, hana fikra za kuhama, kwa vile anatambua umuhimu wake katika bendi hiyo inayotambulika kama 'Kisima cha Burudani'. Kupaza alisema kwa kushirikiana na wenzake kama Mwinjuma Muumin, Hamis Kayumbu 'Amigolas', Luiza Mbutu, Ramadhan Athuman 'Dogo Rama', Venance Mgori, Jumanne Said, Haji Ramadhan (mshindi wa BSS 2011), Janeth Isinika, Khadija Mnoga 'Kimobitel', Grayson Semsekwa, Msafiri Said 'Diouf' na wengine, wataendelea kuipeperusha vyema bendera ya Twanga. Alisema pia wakiwepo wapiga vyombo, Shakazulu, Jojoo Jumanne, Godfrey Kanuti, Selemani Shaibu, Victor Nkambi, Hassan Kado, MCD, wanenguaji Asha Said 'Sharapova', Maria Soloma, Betty Johnson 'Baby Tall', Mary Khamis na wengineo, wataendelea kutamba. Twanga Pepeta hivi sasa inatamba na albamu yake ya 11 ya Dunia Daraja yenye nyimbo za Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji. Albamu zilizopita za bendi hiyo ni Kisa cha Mpemba (1999), Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari 2005 (2005), Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007) na Mwana Dar es Salaam (2009).


...........................................................................................................
 

DIAMOND  NA  J.MARTIN MZIGONI
J.martin  na Diamond



Baada ya nyota yake kung'aa vyema mwaka jana nikimaanisha mwaka 2011, msanii Diamond, amesema kuwa mwaka huu anatarajia kwenda kimataifa zaidi.

Akifunguka mwishoni mwa wiki, Diamond anasema anatarajia kugonga ngoma akimshirikisha J.Martins kutoka Nigeria kazi ambayo ataenda kuifanyia nchini humo.

Hata hivyo Diamond alisema wimbo huo hawezi kuutaja jina kwa sasa kwani utakua ni zawadi kwa mashabiki wake.

Diamond alisema kuwa mbali na kufanya kazi hiyo, pia wasanii wengine ambao atafanya nao kazi mwaka huu, ni kutoka Marekani, Kenya na Uganda

...........................................................................................................


MCHAKATO WA KILI MUSIC AWARD WAANZA.
George Kavishe meneja wa kilimanjaro





Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:

1. ACADEMY:

ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Jan 2012.

2. Majaji:

Hatua ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).

3. KURA:

Hii ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa kura :

  • Njia ya ujumbe mfupi (sms).
  • Njia ya barua pepe (Email).
  • Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
  • Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)

Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee Luhaja amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya tunzo za Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga za muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

Alisema msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao kupitia tungo zake



...............................................................................................................



Charlz baba arejea nnchini       


Charlz baba!!!muimbaji mpya wa mashujaa mara baada ya kutua uwanja wa ndege jana akitokea dubai alipokuwa amekwenda kupumzika....mwimbaji huyo atatambulishwa leo.






................................................................................................................










Mzee Kipara azikwa


 Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki mh.Samwel Sita,Akiwa na rais wa ahirikisho la filamu nchini Simon mwakifamba  na muigizaji Hashim Kambi, katika mazishi ya mzee kipara

....................................................................................................................................................................


Pembe na Senga nao walikuwepo kumsndikiza mzee kipara katika safari yake ya mwisho.ambapo Rais Jakaya kikwete ametoa salam za rambirambi kwa kundi la kaole.






..............................................................................................................



TUTAKUWA TUNAKULETEA HISTORIA ZA WASNII WA
KIAFRIKA KILA  ALHAMISI'   KARIBUNI

...................................................................................................................................................................


JAMAA AKISUBIRI HUKUMU


 Msanii wa bongo fleva  Diamond akiwa katika mahakama ya mwanzo ya iringa kabla ya hukumu yake ambapo alilipa faini na kuachiwa.....kwa undani wa sakata hilo fuatilia afrika ngoma ya radio 5
.....................................................................................................................................




Huku Dude kule Ndikumana

 Msanii wa filamu nchini  Kulwa Kikumba maarufu kama Dude,amekanusha vikali kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa msanii wa kike mwenye  mvuto Irene Uwoya.
....................................................................................................................................................................


MALI YA MASHUJAA

Huyu ndo Charlz Baba ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na bendi ya mashujaa...Kila la kheri chalz baba.

''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''



CHARLZ BABA AJIUNGA NA MASHUJAA MUSICA
Baada ya sekeseke la muda wa wiki nzima hatimaye imegundulika kuwa jamaa amejiunga na mashuja musica..pichani meneja wake akionesha mkataba wake.




MZEE KIPARA HATUNAYE TENA.....
Mzee kipara  amefariki nyumbani kwake...................Fani ya uigizaji imepatwa na pigo kubwa sana Rest in piece baba.