JAJI wa Mahakama Kuu, Aloyce Mujulizi jana alijitoa
kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini ,Godbless
Lema (Chadema) baada ya upande wa utetezi kuwasilisha notisi ya kutokuwa
na imani naye kutokana na Kampuni ya Uwakili ya Imma aliyokuwa akifanya kazi ,
kutuhumiwa na ufisadi kwa kusaidia kuchotwa fedha Benki Kuu (BOT) fedha
ambazo zilidaiwa kusaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.
Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliwasilisha notisi hiyo ya kuendelea kutokuwa na imani na jaji huyo Januari 31 mwaka huu na jana, aliendelea kusisitiza kuwa mteja wake (Lema) hana imani na Jaji huyo kwani chama chake cha Chadema kilishiriki kuituhumu kampuni ya Imma kwa kusaidia Kampuni ya Deep Green Ltd kuchota fedha BOT.
“Kwa kuwa maneno haya yalitamkwa na Chadema na yalitolewa pia bungeni na Kampuni ya Imma haikuwahi kukanusha kama ni kweli au la, mteja wangu anaamini, wewe wakati huo ulikuwa mmoja ya wanahisa katika kampuni hiyo, hivyo anahofu hautamtendea haki katika kesi hii hivyo tunaomba kwa busara ujitoe,” alisema Kimomogoro.
Alisema mteja wake yupo tayari kutoa ushahidi juu ya kutuhumiwa kampuni ya Imma, kuhusika na ufisadi huo ambao ulielezwa fedha zake hizo ndizo ambazo zilisaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.
Jaji Mujulizi alitangaza uamuzi wa kujitoa baada ya mawakili wa pande zote kutoa hoja zao kwa zaidi ya saa mbili huku wakili wa utetezi, Alute Mungwai, akieleza kupinga notisi hiyo ya kutokuwa na imani na jaji kwa maelezo imewasilishwa kinyume cha sheria, haina ukweli, imejaa majungu, inashusha heshma na hadhi ya mahakama na jaji huyo kwani tuhuma za Imma hazijathibitishwa
Jaji
Akitoa uamuzi wake, Jaji Mujulizi alisema anachukua uamuzi wa kujitoa kwa kuzingatia heshima na maslahi ya haki hasa kutokana na mlalamikiwa kueleza kutokuwa na imani naye.
Jaji Mujulizi alisema amechukua uamuzi huo pia ili kuhakikisha kesi hiyo isiendelee kupigwa danadana na lazima ifike kikomo kwani ushahidi unaonyesha upande wa walalamikiwa una lengo la kuchelewesha kesi hiyo.
Akinukuu kesi mbalimbali zilizowahi kufikiwa uamuzi kama huo, Jaji Mujulizi alisema kimsingi shauri lililopo mbele yake linahusiana na kesi ya uchaguzi ambayo inapangiwa muda maalumu kumalizika na sasa imebaki miezi minne pekee kufikia mwisho.
“Notisi iliyowasilishwa kuwa hawana imani na mimi , imekiuka kila aina ya utaratibu na ni dhahiri wanachokifanya ni kuchelewesha tu usikilizaji wa kesi hii”, alisema Jaji Mujulizi.
Hata hivyo, Jaji Mujulizi alitoa siku tano kwa Lema kuwasilisha mahakamani hapo na nakala kumpatia yeye ambapo pia alisema maelezo ya kutokuwa na imani naye, yanatilia shaka uwezo wake na mahakama hiyo, wanapaswa Chadema kuleta mahakamani tuhuma hizo kuwa Kampuni ya Imma ilihusika na fedha za EPA ndani ya siku tano.
Alisema pia chadema wanaweza kuchukua hatua za kikatiba kuwasilisha maombi rasmi kwa Rais Jakaya Kikwete aunde tume kuchunguza sakata hilo na pia kama yeye hastahili kukalia ofisi ya jaji na wafanye hivyo kwa kuzingatia Katiba.
“Hatuwezi kukaa kila mtu akae na kuchafua wengine kwa kurudia rudia na hadi kuamini kuwa ni ukweli,” alisema Jaji Mujulizi.
Awali, Wakili Mungwai alitoa hoja mbali mbali za kisheria kupinga notisi ya kumtaka jaji huyo kutojitoa na kueleza kuwa kama akikubali kujitoa itaonyesha amekubali kuhusika na tuhuma za ufisadi na hivyo itaathiri heshima na hadhi yake na mahakama kwa ujumla.
Lema atamba
Mara baada ya uamuzi huo, nje ya Mahakama akizungumza na waandishi wa habari, Lema alisema ndani ya siku tano watawasilisha ushahidi wa tuhuma zao bila ya matatizo.
“Tuna ushahidi wa kutosha juu ya kampuni ya ImmaAdvocate na hatuna shaka juu ya hili”, alisema Lema.
Wafuasi wachache wa Chadema ambao jana walifika mahakamani, walipokea uamuzi ya Jaji Mujulizi kwa shangwe na mmoja nusura ajikute akitiwa nguvuni baada ya kupiga makofi mahakamani mara baada ya jaji kusema anajitoa

Mwananchi.
No comments:
Post a Comment