Tuesday, February 7, 2012

NKAMIA APANIA KUNYANYUA ELIMU


Mbunge wa jimbo la kondoa kusini Juma Nnkamia amesema kuwa Moja ya mikakati aliyojiwekea katika kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda ni kuhakikisha kuwa kila mwaka anasomesha watotoI 20 ambao wazazi wao hawana uwezo wa kifedha wa kuwapatia elimu.

Akizungumza na mwandishi wa habari jijini Arusha Nnkamia amesema kuwa idadi hiyo sio ndogo kwa kuwa ukiwa na uhakikia wa kupata wapiga kura walioelimika ni faida kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa kutokana na uhaba wa walimu katika jimbo lake pindi anapokuwa jimboni hulazimika kuingia darasani kufundisha kama mwalimu kwa kuwa anataaluma hiyo ya ualimu.

Amefafanua kuwa watoto hao ambao anawafadhili ana wasomesha anampango wa kuwapatia kompyuta ili waweze kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

Nnkamia amesema kuwa msaada huo wa elimu ni pamoja na sare ya shule,ada,viatu,madaftari ambavyo ni vifaa muhimu vya shule na lengo likiwa ni kuwa na jamii iliyoelimika.

Katika hatua nyingine amefafanua kuwa uhaba wa walimu unachangiwa na mazingira magumu kwa kuwa kuna baadhi ya maeneo ni magumu kufikika na hilo sio tatizo la jimbo lake tu bali ni nchi nzima.

''uhaba wa walimu unatokana na mazingira magumu kwa mfano kuna baadhi ya maeneo kufikika si chini ya kilometa 210 kama vile shule ya Birise hiyo nayo inachangia tatizo hili''alisema Nnkamia

Hata hivyo maesema kuna baadhi ya shule kuna mwalimu mmoja hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuinua kiwango cha elimu katika jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakiki mwalimu kwa kumuona na sio uhakiki wa maandishi kwa kuwa utagundua mapungufu mengine pamoja na kuwa na uhakika zaidi.
Na Ashura Mohamed

No comments: