Friday, February 3, 2012

WANAFUNZI WAJERUHIWA KATIKA MAHAFALI

WANAFUNZI saba wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Korogwe Girls  pamoja na mp gapicha wa kujitegemea wamejeruhiwa vibaya kwa kugongwa na gari lilolkuwa likichezewa na mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakisubiri kushiriki katika mahafali ya kuhitimu kidato cha sita cha shule hiyo.

Ajali hiyo ilisababisha vilio, majonzi na huzuni kutawala katika viwanja vya shule hiyo iliyopo Wilayani Korogwe na hivyo kuvuruga mwenendo mzima wa sherehe za mahafali  ya wahitimu wa kidato cha sita shuleni hapo.

Ajali hiyo  ililotokea  saa 4:20 asubuhi katika shule hilo, baada ya mwanafunzi mmoja Kibibi Mmasa anayesoma kidato cha sita shuleni hapo , kuingia katika gari la kaka yake lenye namba za usajili T489 AGJ ambaye alifika kushuhudia mahafali hayo, aliweka gia hiyo kisha gari hilo kurudi nyuma kwa mwendo kasi wa kilomita 120 kwa saa na kuwaparamia wahitimu hao waliokuwa wamejikusanya vikundi.

Wanafunzi waliojeruhiwa na hali zao kuelezwa zipo katika hali mbaya ni Zahra Jumanne (19) na mpiga picha wa siku nyingi. Elias Ngole 'Ngoswe', wengine ni Renata Renatus (25), Sophia Godfrey (19), Victoria Mtwale (19), Nancy James (19) na Mwanamkonda Kapunda (19) ambao wote wanasoma kidato cha sita na ambao walikuwa wakitarajia kufanya mahafali ya kumaliza shule.

Watu waliokuwa katika shule hiyo wamesema walishuhudia gari hilo likiendeshwa na mwanafunzi huyo likichomoka  kwa kasi kurudi nyuma na kuanza kumgonga mpiga picha huyo ambaye alikuwa akizungumza na mwenzake ambaye baada ya kuliona gari hilo aliruka pembeni lakini mwenzake alishindwa na badala yake gari hilo lilimgonga kisha kunasa chini yake na kuburuzwa hadi kiasi cha mita 30 gari hilo lililopogonga mti na kusimama.

Baada ya kugongwa mpiga picha gari hilo liligonga wanafunzi wengine ambao walikuwa wamejikusanya wakibadilishana mawazo namna watakavyosherehekea mahafali yao ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta nchini, Sabasaba Moshingi.

 Mmoja wa wanafunzui hao, Zahra aligongwa vibaya na kunasa chini ya gari hilo ambapo gari hilo lilipinduliwa ili kumnasua huko chini akiwa amevunjika miguu na kupata jeraha kubwa kichwani.

"Kaka alinituma mle ndani ya gari wakati nikichukua mzigo aliyonituma ghafla nikaona gari linakwenda, nikawa sijui kinachoendelea nikasikia makelele wenzangu wanapiga huko nje huku nikiwa nimekanyaga mafuta," alisema Kibibi huku akisihi viongozi wamweche kaka yake ambaye alishikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo. Kaka yake ni Hussein Mmasa

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Erasto Sima ambaye alifika kwenye eneo hilo na baadaye kwenda hospitali kufuatilia matibabu ya majeruhui hao, alisema tukio hilo ni la kusikitisha na alishawahi kutoa taadhali kuhusu magari yanayokwenda kwenye sherehe kama hizo shuleni kwamba magari yaegeshwe kwenye maeneo maalum kuliko kuwekwa katika maeneo kama hayo ambayo yanaweza kutokea ajali kama hizo.

Wanafunzi hao, wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Korogwe iujlikanayo Magunga  wakiendelea kupatiwa matibabu huku mmoja wao Zahra akiwekewa mashine ya  kupumulia Oksijeni na wengine hali zao zinaendelea vizuri. Mahafali yaliendelea lakini hayakuwa na furaha kutokana na tukio hilo.

No comments: