DAR ES SALAAM; DESEMBA15,2011
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imezindua mradi wa kimtandao utakaofanya kazi ya kudhibiti na kulinda ubora wa vifaa anuai kwenye maabara yake ambayo hutumika kuchunguza na kubaini maradhi ya binadamu.
Akizindua mradi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya amesema mradi huo utasaidia kugundua kwa usahihi vifaa na hata kumuelekeza daktari kutoa tiba kwa usahihi kwa wagonjwa.
Naibu Waziri pia amepata fursa ya kutembelea maabara ya TFDA ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kufuatilia kwa umakini na kulinda afya za Watanzania hususani katika dawa za vyakula.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Dawa na Vipodozi, Mitangu Fimbo amesema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa kipindi cha kukamata dawa bandia.
...................................................................................................................................................................
IRINGA; DESEMBA15,2011
Hali ya simanzi na majonzi imetawala kwa wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi mkoani iringa mara baada ya baraza la mitihani la taiafa kufuta matokeo yote ya watahiniwa 737 waliobainika kujihusisha navitendo vya udanganyifu.
Taarifa ya afisa elimu wa mkoa wa IRINGA imeeleza kwamba baraza limebaini kuwepo kwa mfanano usio wakwaida katika majibu ya watahiniwa hao,hali ambayo inaashiria kuwepo kwa udanganyifu.
Kufutia hali hiyo waziri wa nchi sera uratibu na bunge WILIUM LUKUVI ameagiza kuundwa mara moja tume itakayochunguza na kuwawajibisha wote watakaobainika kusababisha hali hiyo.
Halikadhalika amezisihi halmshauri mbalimbali nchini zilizofanya vizuzi katika matokeo hayo kutobweteka na badala yake kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea kuinu sekta ya elimu.
Hapo jana baraza la mitihani la taifa limetangza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika mwezi September kote nchini ambapo kiwango cha ufaulu kimeongezaka kutoka asilimia 53.52 kwa mwaka jana hadi asilimia 58.28.
.......................................................................................................................................................................
ARUSHA: DESEMBA15,2011
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema masuala ya ugavi na manunuzi bado yanakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba usimamizi zaidi unahitajika ili Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 iweze kufanya kazi kwa asilimia 100.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Pili wa wataalamu wa masuala ya ugavi na manunuzi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).
PINDA amesema asilimia 80 ya bajeti ya maendeleo inatumika katika manunuzi ya Serikali kupitia huduma pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu
Ameongeza kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kutosha kumetoa mianya mingi ya utoaji rushwa na uagizaji wa bidhaa bandia hali mabayop inasababisha hasara kubwa kwa serikali.
Kwa upande mwingine waziri mkuu ameziagiza halmashauri ambazo zimepata hati chafu kuhakikisha zinafanyia marekebisho maeneo muhimu kabla ya serikali kuzichukulia hatua.
...................................................................................................................................................................ZANZIBAR: DESEMBA15,2011
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar HAMAD MASUD amema serikali imechoshwa na kuona kesi nyingi za usalama barabarani zikiachwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kukosekana kwa ushahidi .
Amesema hayo wakati alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar Dk Shein katika uzinduzi wa muongo wa Taifa wa usalama barabarani huko kati Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
MASUD amewataka askari wa usalama barabarni wabadilike ili kuona kesi za ajali za barabarani zinachukuliwa hatua madhubuti za kisheria ili aliye fanya kosa ahukumiwa kwa mujibu wa sheri.
Hata hivyo amesema kuwa wananchi wa Zanzibar wamechoshwa kuona uvunjwaji wa sheria za barabarni na vifo vinavyo tokana na ajali hizo.
...............................................................................................................................................................PRODUCED BY;
MONICA NANGU
CHRISTIAN SUMARY.
No comments:
Post a Comment