Rais wa chama cha madaktari Tanzania ,bw .Mkopi.
Chama cha Madaktari nchini (MAT), kimetoa muda wa saa 72 kwa
serikali kuwarejesha kazini madaktari waliofukuzwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam wanarejeshwa kazini mara moja.
Taarifa ya chama hicho imesisitiza kwamba, ikiwa serikali haitotekeleza matakwa yao, basi
kitaitisha mkutano mwingine siku ya Jumatano wiki hii, kujadili mambo mbalimbali
likiwemo suala la kufukuzwa kwa madaktari hao.
Chama hicho pia kimemtaka
Rais Jakaya Kikwete, kumwajibisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni
kwa kuwa chanzo cha migogoro ya madaktari hapa nchini.
Mgogoro huo wa madakatari na serikali unafuatia kufukuzwa kwa
wenzao 229 baada ya kuitisha mgomo wa kudai posho zao ambapo walilipwa na
serikali lakini baadaye wakapewa barua za kufukuzwa kazi.

No comments:
Post a Comment