Waziri wa afya Dk.Hajji Mponda na naibu wake Dk Lucy Nkya
DAR ES SALAAM
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk
Haji Mponda amewataka madaktari walioko kwenye mgomo kurejea kazini ili kuoko
maisha ya watanzania wakati hoja zao
zikifanyiwa kazi na serikali.
Waziri Mponda ameyasema hayo jijini Dar
es salaam na kuwasihi madktari kufanya mpango wa kufika ofisi ya waziri mkuu
kwa ajili ya majadiliano,huku pia akisisitiza kwamba kanuni za utumishi
zinamtaka mtumishi kudai haki yake huku akiwa anaendelea na majukumu yake kama
kawaida.
Mgomo huo wa madaktari ambao unaingia
siku ya nne hii leo,tayari umesambaa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo
mikoa ya mwanza,na mbeya.
Kwa upande wao madaktari wameitaka
serikali kutumia njia sahihi kujibu hoja zao za msingi ili kuleta suluhu ya
suala hilo.
Mwenyekitiwa madaktari hao Dk Steven Ulimboka ameitaka serikali kuchukua
hatua za haraka katika kuhakikisha kwamba madai yao yanafanyiwa kazi kabla ya
kutokea kwa athari kubwa zaidi.
Katika hatua nyingine,wakati serikali
ikiwataka madaktari kurejea kazini ili kuokoa maisha ya watanzania wanaotegemea
huduma zao, Mkoani Kilimanjaro madaktari zaidi ya 100 katika hospitali ya rufaa
ya KCMC wamekubaliana kuanza mgomo wao
hii leo asubuhi kuunga mkono wenzao ambao wako katika mgomo.
Madaktari hao wamefikia maamuzi hayo
hapo jana jioni katika kikao walichofanya katika ukumbi wa hospitali hiyo kujadilia
madai yanayodaiwa na wenzao walioanza mgomo jijini dare s salaam.
Wakizungumza mara baada ya kikao hicho
, wamesema madai ya wenzao ambao wako
katika mgomo ni ya msingi ,na kwamba hayapaswi kupuuzwa kwa namna yoyote .
Wamesisistiza kwamba wataingia katika
mgomo na kuwaunga mkono wenzao hadi pale serikali itakapochukua hatua mahususi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza na
kuyatafutia ufumbuzi madai yao.
......................................................................................................................................................................
DAR ES SALAM
SERIKALI imesema imefanikiwa kukusanya mapato
yanayotokana na kodi mbalimbali kwa zaidi ya asilimia 100 kutokana na
ushirikiano mzuri baina ya wananchi serikali na ,idara mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda wakati akijibu maswaliya waandishi
wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo wa mwaka
kuhusu Sera ya Taifa unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Waziri mkuu PINDA amesema katika kipindi cha
miezi 3 seriklai imefanikiwa kukusanya
mapato ya kodi kwa zaidi ya asilimia 100 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali
vya mapato nchini.
Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Waziri Mkuu,
amesema lengo kubwa ni kufanya tathimini na kuangalia mipango mbalimbali ya
maendeleo ikiwa imetekelezwa au la.
Waziri mkuu akiwa na mabalozi na mawaziri katika mkutano huo.
.........................................................................................................................................................................
ARUSHA
Jeshi la polisi mkoani Arusha limeombwa
kukidhibiti kikundi kinachojiita jeshi la kimila kilichoundwa wilayani Arumeru
ili kuepusha kutokea kwa ghasia baina ya wananchi na kikundi hicho.
Wakizungumza na kituo hiki wananchi
wilayani arumeru wamesema kikundi hicho
hufanya shughuli zake nyakati za usiku ikiwemo kuwakamata wananchi kuwapiga na
kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji.
Kiongozi wa wananchi hao SAIBOKO NGOISO
ameliomba jeshi la polisi kudhibiti kikundi hicho haraka kabala ya wananchi
kuamua kujichukulia sheria mikononi hali mabnbayo inaweza kusababisha umwagaji
damu.
Malalamiko ya wananchi hao yanajuka siku chache mara
baada ya viongozi mbalimali wa serikali
akiwemo naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi GOODLUCK OLE
MEDEYE kusema kwamba kwa serikali
inaendelea kushughulikia suala hilo ,huku pia akiwataka wananchi walioyakimbia
makazi yao kurejea nyumbani.




No comments:
Post a Comment