Sunday, January 22, 2012

TASWIRA KATIKA TAIFA

Vyoo ndio kipimo cha umasikini
By
       David Rwenyagira



Kitika maisha ya kawaida ya binadamu vitu vikuu muhimu ni chakula, matibu na makazi ambayo kwa kiqasi kikubwa upimwa na ubora wa choo. Niliopita katika baadhi ya makazi nje kidogo ya mjiwa Dodoma na kusikitshwa na aina ya vyooo nilivyokuta ambavyo kwa mtazamo wangu vina dhalilisha utu nwa tumiaji.
Urefu vyoo hivyo hauzidi mita moja ya kina chake na minyaa na mifuko ya plastiki ndio uzio unaotengeza sitili ya mtumiaji.hii niafadhali kwa watumiaji wa kiume kuliko dada na mamazetu kim- singi ni aibu tupu.

Kuona vyoo peke yake  hakutoshi nikaanza kujiuliza hivi suala la kujenga choo bora ni wajibu wa nani serikali au mtumiaji?
Lakini  je inaweza kuwa ni uzembe tu wa mtumiaji kwa nia ya kuonyesha uma kwamba serikali imewasahau watu wake?
Hivi kweli kile kikundi cha watu wanaolipwa mishahara kwa kazi ya afya kipo?
Ni kwa namna gani mtuimiaji wa choo ya namana hii anaweza kuepuka maradhi ya miripuko kama kipindupindu lakini mamlaka na kitego cha maafa pengine wanasubiri yatokee ili wanunuea maturubai kwa ajili ya kuhifadhi wahanga.
Nafikiri umefika wakati wa viongozi kuona kwamba wanawajibika na hasa katika mpango wa udhibithi na usimamiaji wa masula ya afya.
Kama vyoo vya namna hii vinaweza kupatikana  Dodoma ambapo wabunge wote ufanya kusanyiko na viogozi wote ufika wakiongozwa na waziri mkuu basi sehemu zingine ambazo kwa mwaka mzima mgeni rasmi wa sherehe zao ni mkuu wa wilaya kwa vyovyote hali itakuwa mbaya sana.
Narudia tena ukitaka kupima viwango vya umasini tafadhari kanuni ya msingi ni kuangalia ujenzi wa vyoo ukiona vyoo kama hivi ujue kimeisha waka  na hafadhari serikali ikatafuta njia mbadala  ama ya kualazisha wajenge vyoo bora au iwajengee kama wanafuzi kabala haijawaweka kwenye kambi ya kipindupindu ambako kwa namna yoyote ghalama zitaku kubwa sana.       


No comments: