Friday, January 20, 2012

SUMARI KUZIKWA JUMATATU

Mwili wa mbunge na aliyewahi kuwa naibu waziri wa fedha Jeremia Sumari,Unatarajiwa kuzikwa Arusha siku ya Jumatatu,Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana,Mwili huo utaagwa siku ya jumamosi katika ukumbi wa karim jee na kusafirishwa  siku ya jumapili kwenda Arusha kwa ajili ya kuupumzisha siku ya jumatatu.Endelea kusikiliza Radio5 na kutembelea blog yetu kwa taarifa zaidi.  Chini ni picha za viongozi wa serikali walipokwenda kuwapa pole wafiwa.




 Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisaini kitabu cha maombolezo alipofika kwenye msiba wa Mbunge wa Jeremiah Sumari nyumbani kwake.Pembeni yake ni spika wa bunge na waziri mkuu mstaafu Mh.Edward  Lowasa.


Rais Jakaya Kikwete akiwafariji wafiwa katika msiba huo.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Spika wa bunge Anne Makinda na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa Nyumbani kwa marehemu  Mbezi beach jana.
 Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal,akisaini ktabu cha waombolezaji jana alipokwenda kuwafariji wafiwa.
 Makamu wa rais akisalimiana na watoto wa marehemu jana nyumbani kwao.
Makamu wa rais akiongea na mke wa marehemu mama Miriam Sumari nyumbani kwake jana. Mwili wa mbunge Jeremia Sumari aliyefariki usiku wa kuamkia jana utazikwa jumatatu Arumeru mkoani Arusha.

No comments: