MTANDAO wa kijamii wa Jamii Forum haujasajiliwa Tanzania,
Bunge limeelezwa.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, amewaeleza wabunge kuwa, mmiliki wa mtandao huo anaweza kuwa Mtanzania au si Mtanzania.
Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare (CCM).
Mbunge huyo amedai kuwa, Mtandao huo umekuwa ukisambaza habari za uongo kwa watu mbalimbali na haujachukuliwa hatua hivyo alitaka kumfahamu mmiliki wa mtandao huo.
Kitwanga amesema, uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha , na huanzishwa na mtu yeyote popote duniani.
“Kutokana na asili na miundo ya tovuti za kijamii, mamlaka haisajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoadikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni binafsi ya watu yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la” amesema Kitwanga.
Baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) kuuliza swali la nyongeza, wakati Kitwanga anajiandaa kumjibu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka kiongozi huyo wa Serikali, ajibu hasa swali kuhusu ‘ Jamii Forum na matatizo yake makubwa’
Ngoye amedai kuwa, baadhi ya mambo yanayoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forum yana madhara katika jamii yakiwemo matusi ya nguoni na ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.
Aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada , Bunge litunge sheria ili mtandao huo uache kuandika mambo ya maudhi na uchochezi.
Alitaka pia kufahamu kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada ili Bunge litunge sheria itakayozuia watoto kusoma ‘mambo machafu’ kwenye ‘internet cafĂ©’ vikiwemo vitendo vya ngono.

No comments:
Post a Comment