CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) vinaingia kwa mara nyingine katika mpambano wa kuchagua
mbunge wa Arumeru Mashariki.
Hali hiyo inatokana na jana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru na madiwani katika kata nane utakaofanyika Aprili mosi. Uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari (CCM) kilichotokea Januari 19 pamoja na vifo vya madiwani wa kata husika.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NEC, Damian Lubuva, uteuzi wa wagombea wa ubunge utafanyika Machi 8 na kampeni zitaanza Machi 9 hadi 31.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote, kuwa imepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye kuiarifu kuhusu nafasi wazi ya ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki,” ilisema sehemu ya taarifa ya Mwenyekiti wa NEC.
Kutangazwa kwa uchaguzi huo kunatoa fursa nyingine ya mpambano wa kisiasa baina ya vyama hivyo, ambavyo vilichuana katika kuwania jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu mwaka juzi na hatimaye Sumari kushinda kwa kura 34,661 sawa na asilimia 62.23.
Mgombea wa Chadema, Joshua Nasari alipata kura 19,123 sawa na asilimia 34.33, John Pallangyo wa CUF alipata kura 265, Linda wa Jahazi Asilia kura 176, Fanuel Pallangyo wa TLP kura 88 na Charles Msuya wa UPDP kura 88.
Kwa upande wa madiwani wa kata nane zilizoko katika halmashauri mbalimbali nchini, ratiba inaonesha uteuzi wa wagombea ni Machi 5 na kampeni zitaanza Machi 6 hadi 31. Kata hizo zipo wazi kutokana na vifo vya madiwani husika.
Alifafanua, kwamba hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo. Alisema Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, ndilo litakalotumika katika uchaguzi huo mdogo.
Vituo vitakavyotumika kupiga kura ni vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka juzi. Tume ilisema itaweka orodha ya wapiga kura katika vituo vya kupigia kura kwa siku saba kuanzia Machi 25 hadi 31.
Wananchi wa Arumeru Mashariki na kata zote ambazo uchaguzi utafanyika wameombwa kwenda katika vituo vyao vya kupigia kura kukagua majina yao. Aidha vyama vya siasa vimeaswa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume.
Hiki kitakuwa kipindi kingine cha wanasiasa kuelekeza macho, masikio, nguvu na kila aina ya mbinu za uchaguzi Arumeru ukiwa ni uchaguzi mdogo wa pili kutokea Tanzania baada ya ule wa Igunga, ambapo CCM kupitia kwa Dalaly Kafumu, iliibuka kidedea.
Tofauti na Arumeru Mashariki, uchaguzi wa Igunga ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wake, Rostam Aziz, kujiuzulu wadhifa huo na nyingine alizokuwa nazo CCM kwa alichokiita siasa chafu.

No comments:
Post a Comment