Watu
wasiopungua 37 wameuawa huko Sudan Kusini katika upiganaji risasi kwenye
mkutano wa amani unaolenga kumaliza ghasia katika eneo hilo, wamesema maafisa.
Maafisa
kutoka majimbo matatu walikutana katika mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa
Mataifa katika mji wa Mayendit, kwenye jimbo la Unity, katika jitihada za
kupunguza uhasama wa kikabila.
Kwa mujibu
wa Umoja wa Mataifa, mzozo ulizuka na magari manne kuwasili yakiwa yamejaa
polisi ambao mara moja walianza kufyatua risasi.
Miongoni mwa
waliokufa ni raia ambapo wanaharakati wa haki za binaadam wameshutumu ukosefu
wa nidhamu miongoni mwa majeshi ya usalama.
Mazungumzo
hayo yaliitishwa kufuatia mfululizo wa mapigano, yakiwemo mapigano ambayo watu
74 waliuawa mapema wiki hii.
No comments:
Post a Comment