RAIS Jakaya
Kikwete, ameagiza mahakama nchini kuhakikisha unatoa elimu kuhusu adhabu
mbadala ya kifungo katika kesi za jinai.
Hatua hiyo
imeelezwa kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa wafungwa na
mahabusu magerezani.
Rais Kikwete, ametoa wito huo jana katika
sherehe za Siku ya Sheria Nchini, iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam.
Siku ya
sheria ni ishara ya ufunguzi rasmi wa shughuli za mhimili huo kwa mwaka huu,
chini ya kauli mbiu ya ‘Adhabu mbadala ya kifungo katika kesi za jinai faida
kwa jamii’.
Rais amesema mbali na kupunguza msongamano, pia
kutawafanya wahalifu waliofungwa vifungo vya nje kuwa karibu na jamii na
kufanya shughuli nyingine za jamii, hivyo kujirudi kitabia.

No comments:
Post a Comment