MAHAKAMA
Kuu Dar es Salaam imerejesha matumaini kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
baada ya kutupilia mbali pingamizi la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya
Dowans dhidi ya maombi yake ya kibali cha kukata rufaa.
Tanesco iliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka kibali cha kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya mahakama hiyo iliyoamuru kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans ya Sh94 bilioni, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).
Hata hivyo, Dowans nayo kupitia kwa wakili wake, Kennedy Fungamtama iliweka pingamizi dhidi ya Tanesco ikiiomba mahakama hiyo iinyime kibali hicho cha kukata rufaa kwa madai kuwa haina haki ya kisheria kupinga hukumu hiyo.
Lakini katika uamuzi wake jana, Jaji Dk Fauz Twaib alitupilia mbali pingamizi la Dowans akisema Tanesco inayo haki ya kukata rufaa.
Kwa mujibu wa taratibu za kesi ya migogoro ya kibiashara, kama mshindwa tuzo akitaka kukata rufaa kupinga tuzo iliyotolewa kwa mshinda tuzo, anawajibika kwanza kuomba kibali cha kukata rufaa hiyo kwa mahakama iliyotoa tuzo hiyo.
Hata hivyo, katika uamuzi wake, Jaji Dk Twaib alisema kwa mazingira ya kesi hiyo, Tanesco haikuwa na haja ya kuomba kibali mahakamani hapo ili kukata rufaa hiyo na kwamba ingeweza kutumia utaratibu wa kawaida tu.
Uamuzi huo unatoa matumaini kwa Tanesco kuanza harakati za kuzuia kisheria malipo ya Sh110 bilioni ambayo inapaswa kuilipa Dowans baada ya hukumu ya ICC.
Akizungumza baada ya uamuzi huo, Wakili anayeitetea Tanesco, Dk Alex Nguluma kutoka Kampuni ya Rex Attorneys alisema kutokana na uamuzi huo sasa watakwenda kukata rufaa moja kwa moja Mahakama ya Rufani kupinga hukumu hiyo.
Hukumu ya ICC
Novemba 15, 2010 AICC, chini ya Mwenyekiti, Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, ICC iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh94 bilioni, kwa kuvunja mkataba baina yao kinyume cha sheria.
Kutokana na uamuzi huo, Januari 25, 2011 Dowans iliwasilisha maombi mahakamani hapo ikiomba tuzo yake hiyo isajiliwe ili utaratibu wa ulipwaji wake uwe na nguvu ya kisheria.
Hata hivyo, Tanesco kupitia kwa mawakili wake, Rex Attorneys kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliwasilisha pingamizi la usajili wa tuzo hiyo Februari 9, 2011.
Lakini, Septemba 28, 2011, Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam aliamua tuzo hiyo ya Dowans ya Sh94 iliyotolewa na ICC isajiliwe na kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.
Katika uamuzi wake, Jaji Mushi alikubaliana na hoja za Dowans na kutupilia mbali pingamizi la Tanesco na kuamuru tuzo hiyo isajiliwe na kuwa hukumu halali ya mahakama hiyo.
Jaji Mushi alisema baada ya kupitia mwenendo na hoja za pande zote, alibaini kwamba si sawa kwa mahakama hiyo kuingilia uamuzi wa ICC.

wakati huohuo
SERIKALI imetiliani saini mkataba wa kutafuta mafuta na gesi
na kampuni ya Swala katika maeneo ya Kilosa Mkoani Morogoro na Pangani Mkoani
Tanga.
Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mktaba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana , Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja aliitaka kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yaliyomo kwenye mkataba kwa vitendo.
Ngeleja aliihakikisha kampuni ya Swala kuwa serikali na Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) itatekeleza makubaliano yaliyomo na kwamba itatoa ushirikiano kwa kila jambo litakalohitajika na kampuni hiyo wakati wowote.
“Mikataba huu wa leo ni muhimu katika suala la maendeleo ya utafutaji na uchimbaji gesi na mafuta kwa Tanzania na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa ukubwa wake nasema hivyo sababu kuna mambo mawili yenye manufaa makubwa kwa wananchi wa husuani walio katika eneo linalozunguka machimbo hayo”alisema Ngeleja na kuongeza,.
“Kampuni ya Swala, wao wanasema watatoa sehemu ya faida ya pato lao kwa ajili ya kuchangia shughuli za maendeleo katika eneo la uchimbaji na pia watauza hisa zao katika soko letu la ndani ili kuongeza wigo wa umiliki kwa wazalendo”alisema.
Ngeleja aliitaka TPDC Kutoa vipaumbele kwa kampuni za uwekezaji za aina hiyo pindi zinapoomba kuingia mikataba ya uwekezaji katika sekta hiyo ya uchimbaji mafuta.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPDC Yona Kilagane alisema tangu gesi ipatikane nchini Julai 2004 hadi 2011 serikali imeokoa Sh 3.3 bilioni zilizokuwa zitumike kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme.
Alisema hali hiyo imetokana na gesi hiyo kuchangia Megawati 416 sawa na asilimi 35 ya umeme unaotumika nchini.
“Kiasi hicho cha fedha kingetumika kununua mafuta mazito,disel na ya ndege kwa ajili ya kuendesha mitambo ya umeme,kiasi hicho kimeokolewa”alisema Kilagane na kuongeza kuwa pia kwa wafanya biashara viandani gesi hiyo imeokoa dola 200 milioni”alisema.
Kilagane aliitaka serikali kuangalia suala la miundombuni alilodai linakwamisha kasi ya usafirishaji gesi kutoka katika maeneo inakopatikana hadi jijini Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa masuala la biashara kwa Kampuni ya kutafua Mafuta na Gesi ya Swala Chiris Opperman alisema kampuni hiyo inatarajia kuwa miongoni mwa kampuni kubwa za kutafuta mafuta katika ukanda wa jangwa la Sahara.
Aliema kampuni hiyo ni ya kipekee sababu imeingia ubia na wawekezaji wa ndani katika suala zima la utafutaji mafuta na gesi.
“Tunaamini kuwa Tanzania itakuwa sehemu ya uaptikanaji wa mafuta na gesi na wawekezaji wa ndani wamepewa fursa ya kuwekeza katika kampuni hii,hadi sasa watu zaidi ya 12 ni wawekezaji wa ndani na tunahitaji kuonmgeza idadi yao”alisema Opperman.
Kampini ya utafutaji mafuta ya Swala ni kampuni Tanzu ya kampuni ya Otto Enregy Ltd ya Australia.

CHANJO YA UKIMWI YATOA MATUMAINI
SERIKALI imetoa tamko kuhusu utafiti wa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi
unaoendelea nchini, ikisema: “Matokeo yake yanatia matumaini.” Msemaji wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema jana kuwa chanjo
hiyo ni majaribio ya kimaabara yanayohusu wanyama (nyani) kabla ya matumizi kwa
binadamu. Alisema majaribio hayo yalifanywa na Taasisi ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza ya Marekani, Programu ya Utafiti wa Ukimwi ya Jeshi la Marekani yalionyesha kuwa, kima waliopata chanjo hiyo walikingwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi. “Pamoja na matokeo hayo mazuri ni vyema jamii ikaelewa kwamba majaribio kama haya hayajafanyika kwa binadamu,” alisema Mwamwaja.
Mwamwaja alisema bado wanaendelea na utafiti wa chanjo ya Ukimwi nchini na
kwamba mchakato wa kuainisha matokeo unaendelea. Alisema utafiti huo
unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS) na mtu wa
mwisho alichanjwa Januari mwaka huu.
Alisema majaribio hayo yanalenga kuainisha usalama na uwezo wa kujenga kinga ya binadamu dhidi ya Virusi vya Ukimwi. “Hata hivyo, jamii inapaswa kuelewa kwamba majaribio yanayoendelea nchini yapo katika hatua za awali hivyo tathmini ya uwezo wa kutoa kinga dhidi ya Virusi vya Ukimwi haijafanyika hadi sasa,” alisema Mwamwaja. Alisema majaribio ya awali yalifanywa Sweden kabla ya kuanza nchini na kwamba lengo ni kuendeleza tathmini ya usalama na ubora wa chanjo hiyo ya majaribio.
Aliitaka jamii kuendelea kutumia njia na mikakati ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kama wataalamu wa afya wanavyoshauri na kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna chanjo wala dawa ya kutibu ugonjwa huo iliyothibitishwa kitaalamu. Sera ya Ukimwi Katika hatua nyingine; Serikali imeunda jopo la wataalamu kuchunguza na kutengeneza sera itakayowezesha Tanzania kunufaika na matokeo ya tafiti za kutafuta chanjo na tiba ya Ukimwi.
Miongoni mwa matokeo hayo ni uwezo wa kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) bila kondomu, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba cha Johns Hopkins, Marekani.
Katika utafiti huo, chuo hicho kilibaini kuwa matumizi ya ARV yanaweza kutumika kama njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa waathirika kwenda kwa wapenzi wao ambao hawajaathirika kwa asilimia 95 wanaposhiriki ngono bila kondom. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda alisema Serikali tayari imepokea matokeo ya utafiti huo na kinachofanyika sasa ni wataalamu wake kufanya tathmini na kuunda sera.
“Tulipata taarifa hiyo wakati nikiwa Dodoma (Bungeni) kwa sasa nimerejea ninatarajia kukutana na wataalamu wangu kuona hatua za kuchukua,” alisema Dk Mponda mwishoni mwa wiki iliyopita... “Tunataka tufanye tathmini na tuwe na sera ya Taifa katika mpango huo.”

Alisema kuwapo kwa sera hiyo, kutaiwezesha Serikali kuwa na mpango wa
tathmini ya kiwango gani ambacho Tanzania imeweza kufanikiwa tangu mpango wa
matumizi ya ARV uanze nchini mwaka 2008 na nini kifanyike ili kupunguza zaidi
kasi ya maambukizi.
Afrika Kusini wajipanga
Serikali ya Afrika Kusini tayari imeweka mkakati wa kutumia matokeo ya utafiti huo, kukabiliana na maambukizi mapya katika taifa hilo lenye kasi kubwa ya maambukizo kuliko mengine duniani.
Mmoja wa wataalamu wa afya wa nchi hiyo, Dk Brian Williams alisema tayari wamefanya tathmini na kuona baada ya miaka mitano watakuwa wamefanikiwa kuyakabili maradhi hayo.
Dk Willams alisema Afrika Kusini ina waathirika milioni sita na kwamba ni asilimia 30 tu wanaopatiwa tiba ya ARV. “Ili kuwagharimia waathirika hao itabidi tutumie Dola za Marekani kati ya milioni mbili hadi tatu (Sh3.2 trilioni hadi 4.8 trilioni) kununua dawa za ARV kwa mwaka,” alisema Dk Williams akiwa Marekani, hivi karibuni.
Kutokana na uzoefu wake, Dk Williams alisema utafiti huo utawasaidia waathirika kuwa katika mazingira mazuri ya kupatiwa chanjo ambayo ipo mbioni kupatikana. Ugunduzi wa Hopkins Katika utafiti huo wa matumizi ya ARV, ilibainika kuwa mtu ambaye anatumia dawa hizo za kupunguza makali, anaweza kufanya tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana Ukimwi na asimwambukize kwa asilimia 95.
Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman alisema kwenye ripoti ya ugunduzi huo kuwa wamebaini kuwa ARV sasa zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi. “Huu ni ugunduzi wa kustajabisha,” alisema Profesa Eshleman:
“Matokeo haya yameleta mapambazuko mapya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya.”
Alisema utafiti huo walioupa jina la HPTN 052 waliufanya kupitia maeneo mbalimbali ya dunia hasa yenye kasi kubwa ya maambukizi kama vile Afrika, Brazili, India na Thailand. Kwenye ripoti hiyo ambayo pia ilichapishwa kwenye jarida maarufu la kisayansi linaloitwa Science, watafiti hao wanasema kwamba mtu anapotumia ARV, hufikia wakati fulani wingi wa virusi mwilini hupotea kiasi kwamba anakuwa karibu sawa na yule ambaye hajaambukizwa. “Jambo la msingi katika utafiti huu ni kwamba dawa hizi za ARV zinapotumiwa kikamilifu, hupunguza mzigo wa virusi mwilini kwa zaidi ya mara 200.
Ni sawa na kusema inapunguza hadi kufikia karibu na sifuri,” inaeleza ripoti hiyo. Onyo la utafiti Pamoja na kwamba njia hii imeonekana kuwa nzuri katika kuzuia maambukizi, wataalamu hao wanasema ni hatari pale inapotumika vibaya. Hatari wanayoizungumzia ni kwa muathirika iwapo atatembea na mpenzi ambaye ni pia ni muathirika, lakini akawa hajatumia ARV au ametumia lakini siyo kwa kiwango ambacho VVU vimepunguzwa hadi kufikia karibu na sifuri.
Wataalamu hao wanasema iwapo muathirika atapata maambukizi mapya, atajiweka katika hatari ya kupata usugu kwa aina ya dawa anayotumia. Hata hivyo, wataalamu na watafiti mbalimbali wameelezea utafiti huo kuwa ni mafanikio mazuri katika kurahisisha njia ya chanjo kutoa kinga kwa waathirika na wale ambao hawajaambukizwa.
Kwa sasa zipo aina nane za chanjo za Ukimwi duniani ambazo wataalamu wapo kwenye hatua mbalimbali za majaribio na wamekuwa wakizielezea kuwa zinatia matumaini.

No comments:
Post a Comment