ASEMA SH 1.7 TRILIONI ZINAZOTUMIKA KWA MWAKA ZINATOSHA KUTANDAZA
BOMBA LA GESI NA KUMALIZA KABISA TATIZO
Muheza
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema miradi ya umeme wa dharura inayoigharimu Serikali Sh1.7 trilioni kwa mwaka ni kichaka cha ufisadi.

Akizungumza na wakazi wa Muheza katika mkutano wa hadhara juzi, Zitto
alisema: “Umeme wa dharura unapendwa kwa kuwa ni eneo lililojaa ufisadi. Ni
rahisi kufanya mikataba ya wizi katika eneo hilo. Si tumesikia wizi wa mafuta
ya kuendeshea mitambo ya IPTL? Dola za Marekani 56 milioni zinadaiwa kupotea,
Takukuru wanachunguza.”
Kauli hiyo ya Zitto imekuja wakati tayari Bunge limeidhinisha kiasi cha
Sh1.6 trilioni kwa Serikali kwa ajili ya mpango wa dharura wa kutatua tatizo la
mgawo wa umeme kuanzia Agosti mwaka jana hadi Desemba mwaka huu.
“Nilimwandikia Spika mwaka jana kumuomba aiambie kamati ya Makamba (Januari)
(ya Nishati na Madini) kuchunguza ufisadi katika ununuzi wa mafuta ya IPTL
lakini, mwaka unapita hakuna hatua iliyochukuliwa. Nimemkumbusha tena Spika
katika mkutano uliopita lakini hajajibu. Mimi sitachoka, nitaendelea
kumbughudhi Spika hadi ufisadi huo ufichuliwe.”
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alipotafutwa jana kuthibitisha kama
amepata barua ya Zitto iliyomwomba achunguze wizi kwenye baadhi ya miradi hiyo
hakupatikana kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila ya kupokewa.
Alisema hakuna sababu nyingine ya miradi hiyo zaidi ya mwendelezo wa ufisadi. Alisema fedha hizo zingetosha kama zingetumika kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuondoa kabisa tatizo la umeme badala ya kutegemea umeme wa dharura.
“Pia sehemu ya fedha hizo zingeweza kutumika katika ujenzi wa bomba jingine la gesi kutoka Kiwira hadi Dar es Salaam ambalo kwa pamoja, umeme huo ungeingizwa kwenye gridi ya taifa na kumaliza kabisa tatizo hilo.”
Alisema Serikali imewagawa Watanzania katika matabaka kwani umeme ukikatika Dar es Salaam na watu wakapiga kelele, inatikisika na kushughulikia matatizo yao haraka, lakini vijijini hata watu wakipiga kelele vipi, hawasikilizwi.
Serikali imeamua kukalia ripoti inayothibitisha namna ufisadi unavyoliangamiza taifa: “Serikali inatakiwa kutoa ripoti hiyo ili wananchi wajue nchi yao inakoelekea na waweze kuchukua hatua haraka kuinusuru.”

Zitto alisema ni lazima wananchi wasimame kidete ili kulinda maslahi yao
dhidi ya mafisadi kwa kuwa Serikali imeshindwa kufanya hivyo na kuwasababishia
wananchi umasikini wa kutupwa.
Katika mkutano huo, Zitto alisema maisha ya wananchi wa Tanzania yako
hatarini kwa kuwa wale ambao ni masikini wanaotegemea kilimo wamekata tamaa kwa
kukosa msaada katika sekta hiyo.
“Kila siku mnaambiwa kilimo kimekua kwa asilimia nne, mbona haibadiliki na nyie hamshangai? Ni lazima muwe mnahoji hao wanaofaidika na kilimo ni kina nani hasa kama siyo mafisadi? Umaskini tulio nao nasisitiza wao ndiyo chanzo,” alisema Zitto.
Januari Makamba
Makamba alipoulizwa kuhusu madai ya Zitto kumwandikia barua Spika alisema amepata nakala lakini kamati yake haijapewa maelekezo rasmi kuchunguza suala hilo.

Alisema suala la ununuzi wa mafuta ya umeme linatakiwa kufanyiwa uchunguzi
wa kibunge kwa kuwa haliko wazi katika mchakato wake.
“Tatizo ni kwamba zoezi zima haliko wazi, mimi naunga mkono kuwa uchunguzi
wa kibunge ufanyike na ieleweke wazi masuala ya ugavi na nani amepataje
zabuni,” alisema Makamba.
Kwa upande wa gharama za kukodi mitambo ya dharura, alisema hawezi
kushangazwa na matumizi ya kiasi hicho lakini akasema hana uhakika na kiasi cha
fedha kwani mchakato umekuwa kwa zaidi ya miezi sita tokea Agosti 8, mwaka
jana.
UCHAGUZI ARUMERU
WAKATI Kamati Kuu ya Chadema inatarajiwa kukutana Machi 3, mwaka huu
kumpitisha Mgombea wa Ubunge Arumeru Mashariki, Chama cha Tanzania Labour (TLP)
na Sauti ya Umma (Sau), vimetangaza wagombea wao kwenye kinyang’anyiro hicho.Kamati Kuu ya Chama cha Sau, katika kikao chake kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, kilimtangaza Shaaban Kirita na TLP wamemsimamisha Abraham Chipaka.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Uenezi wa Sau, Johnson Mwangosi, alisema uamuzi wa kumsimamisha Kirita kuwania nafasi hiyo, umefikiwa katika kikao cha kamati kuu kilichofanyika Jumamosi iliyopita.
“Tunamsimamisha Kirita ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la chama chetu,” alisema Mwangosi na kwamba, amepata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wanachama wengine ambao ni Mohamed Mgate na Susan Maro.
Alisema Kirita amechaguliwa kutokana na mchuano mkali uliokuwapo baina ya wagombea ambao wana vigezo, ambavyo vinakaribiana na baada ya vuta nikuvute hatimaye wajumbe walipitisha jina lake.
Mwangosi alisema mgombea huyo ni mpambanaji msomi, mfanyabiashara na ana uzoefu wa kutosha katika masuala ya siasa na uchaguzi na kwamba, alikuwa ‘mwiba mkali’ kwa wanaharakati wa vyama vingine vya siasa uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga.
Alisema wanampeleka Kirita Arumeru Mashariki kutwaa kiti siyo kushiriki uchaguzi, kwa sababu mgombea huyo ni mwenyeji na anazijua changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo.
Katika tukio lingine, Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa Arusha, Leonard Makanzo, alisema Abraham Chipaka alipatikana baada ya kumshinda katika kura za maoni, Fanuel Palangyo.
“Wajumbe wa mkutano wa jimbo walimchagua Chipaka hivyo kamati yetu ya utendaji mkoa pia imempitisha,” alisema Makanzo.
Makanzo alisema ili kuhakikisha upinzani unashinda kiti hicho, wanaomba Chadema wawaunge mkono kama walivyofanya wao Jimbo la Igunga.“Tuliwaachia Igunga sasa tunaomba watuachie Arumeru na watuunge mkono ili tuing'oe CCM,” alisema Makanzo.
Chadema wachukua fomu
Katibu wa Chadema Jimbo la Arumeru Mashariki, Totinan Ndonde, alisema hadi jana ni wanachama sita waliokuwa wamechukua fomu na hakuna alikuwa amerejesha.
Ndonde alisema kikao cha kamati kuu, kitatanguliwa na Mkutano wa Baraza Kuu Chadema katika jimbo hilo, Kamati ya Utendaji Wilaya ya Arumeru na Sekretarieti ya chama wilaya.
“Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Februari 25, tunatarajia mgombea wetu atajulikana Mach 3, baada ya kikao cha kamati kuu,” alisema Ndonde.Alisema waliochukua fomu hadi jana ni Joshua Nasari, Godlove Temba, Yohane Kimuto, Rebecca Mugwisha, Samwel Shami na Anna Mughwira.
Walioshindwa CCM wasubiri
huruma ya vikao vya juu.
Waliokuwa wanawania kuteuliwa na CCM kuwania ubunge Arumeru Mashariki na kubwagwa na Sioi Sumari, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari, wameeleza kusubiri uamuzi wa vikao vya juu.
Wakizungumza baada kinyang'anyiro cha kura za maoni, baadhi ya wagombea hao, walisema kilichotokea katika upigaji kura kimeonekana na wao wanasubiri chama hicho kutoa uamuzi.
Elirehema Kaaya, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Nyangamana, mkoani Mwanza, alisema zoezi la kura za maoni limekwisha na sasa wanasubiri uamuzi wa chama.
“Sina maoni kama unavyojua kura za maoni ni hatua za mwanzo za mchakato, nadhani tusubiri uamuzi wa vikao vya juu,” alisema Kaaya ambaye alishika nafasi ya tatu kwa kura 205.
Maoni hayo ya Kaaya yalionekana kuungwa mkono na wagombea wengine, walioangushwa na Sumari aliyepata kura 316, akifuatiwa na William Sarakikya (259), Elishiria Kaaya ambaye ni mjumbe wa Nec (176), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11).
Mgogoro CCM
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Arusha, wametaka viongozi wa juu wa CCM kuwakemea tena wenzao mkoani hapa wenye njama za kumdhoofisha kisiasa Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige.
Wakizungumza ofisi za UVCCM Mkoa Arusha juzi, baadhi ya viongozi wa UVCCM Arusha, walisema kuna njama za kumhujumu mbunge huyo kutokana na siasa za makundi zinazokinafuna chama hicho.
Katibu wa UVCCM KaTa ya Lemara, Masoud Rajabu na Katibu wa UVCCM Kata ya Sombetini, Rabia Abdallah, walisema kama CCM haitakemea njama chafu za kuchafuana, kunaweza kuibuka mpasuko mkubwa ndani ya chama.
“Kwa mfano hizi taarifa za UVCCM kugomea posho za mbunge, siyo za kweli kwani aliyetoa taarifa siyo kiongozi na hakuwapo hata huko kwenye hafla ya mbunge,” alisema Rajab.
Naye Rabia akizungumzia tukio hilo, alisema baada ya mbunge huyo kwenda kutoa msaada wa baiskeli za walemavu Kijiji cha Olsonyosambu na kurejea, hakukuwa na ahadi za kulipwa posho ya Sh5,000 au zaidi.
SAMAKI WA MAGUFULI
MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa hukumu ya washtakiwa
katika kesi ya uvuvi haramu, Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania
(Exlussive Economic Zone- EEZ), maarufu kesi ya ‘Samaki wa Magufuli’.
Awali katika kesi hiyo ilikuwa na washtakiwa 37, 35 kati yao wakiwa ni raia wa mataifa mbalimbali katika Bara la Asia na wawili wakiwa raia wa Kenya.Katika hukumu ya leo kuna uwezekano mkubwa kushuhudia machozi ya aina mbili, moja ni machozi ya furaha kwa watu ambao hawatapatikana na hatia na kuachiwa huru na machozi ya huzuni kwa watakaopatikana na hatia.
Mshtakiwa wa tisa Hsu Sheng Pao anayedaiwa kuwa mmoja wa mawakala wa meli hiyo, washtakiwa wa 33, Cai Dong Li na wa 34, Cheng Rui Hai huwenda leo wakaamuliwa kwenda kuungana tena na familia zao kwao.
Wengine ni wahandisi wawili wa meli hiyo, mshtakiwa wa 33 na Hai wa 34; na mawakala wawili wa meli hiyo, mshtakiwa wa saba, Zhao Hanquing na mshtakiwa wa tisa Pao.
Pia kuna matumani kwa washtakiwa hao kuachiwa huru baada ya wazee washauri wa Mahakama katika kesi hiyo Magreth Mosi na Bernard Ntumba kuishauri mahakama iwaone hawana hatia na kwamba waachiwe huru.
Wakichambua ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa wakati wakitoa maoni yao ya majumuisho ya kesi hiyo, wazee hao walisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Walisema washtakiwa wa 33 na 34 hawahusiki na mashtaka hayo kwa kuwa wao walikwa ni wahandisi tu wa meli hiyo na kwamba kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha meli inafanya kazi.
Kuhusu mshtakiwa wa tisa Pao walisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushiriki wake zaidi, mbali kuambatana na mshtakiwa wa saba kuja Dar es Salaam hadi kwa Ofisa wa Polisi.
Lakini mshatakiwa wa kwanza, Hsu Chin Tai ( Nahodha) na mshtakiwa saba, Zhao Hanquing (wakala) wanaonekana kuwa na nafasi finyu ya kuchomoka katika mashtaka hayo.
Pia kuna matumaini hafifu kutokana na wazee washauri wa mahakama kushauri mahakama iwatie hatiani.
Maoni yao kwa mshtakiwa wa kwanza walieleza kuridhika kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi yake kuwa alikuwa akivua katika eneo la Tanzania na bila kuwa na kibali.
“Mshtakiwa wa kwanza alitoa kivuli cha ‘fax’ tena cha meli ya Tawaliq 2 na si Tawaliq1. Wakati akihojiwa na PW8 alikiri kwamba taarifa zilizochukuliwa kwenye GPS zilipokelewa na mtaalamu wa alama,” alisema Mosi.
Kwa upande wake Ntumba alisema ushahidi wa mazingira wa shahidi wa tatu, Msimamizi wa Shughuli za Uvuvi na Sheria za Uvuvi Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Nahodha Ernest Bupamba aliyewakamata washtakiwa hao, unathibitisha mashtaka hayo.
“Pia mshtakiwa Ali Mkotya alikiri kuwa walikuwa wakivua katika eneo la Tanzania bila kibali.
Hata hivyo Jaji hafungwi na maoni ya wazee washauri bali hutoa hukumu kutokana na uzito wa ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi ambao huchambua kwa kuzingatia misingi ya kisheria.
Kutokana na hali hiyo matokeo ya hukumu ya leo yanaweza kuwa tofauti na mtizamo huu.Washtakiwa hao na wenzao walikamatwa Machi 8, 2009 wakiwa samaki tani 293 aina ya Jodari.Mpaka sasa washtakiwa hao wamesota rumande kwa muda wa miaka miwili miezi 11 na siku 15 tangu wakituhumiwa kutenda makosa yanayowakabili.
Washtakiwa hao wamesota rumande kwa muda wote huo baada ya kukosa dhamana licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na mawakili wao wanaowatetea Kapteni Ibrahim Bendera na Johna Mapinduzi kuwaombea dhamana mara kadhaabila mafanikio.

DAWA YA BABU
WATAFITI wa kimataifa wa masuala ya
tiba na wanahabari kutoka Japan wamefika Samunge kuendelea kutafiti dawa
inayotolewana Mchungaji Ambilikile Masapila.
Mmoja wa wasaidizi wa Mchungaji Masapila, Paulo Dudui, alisema Wajapani hao wamefika hivi karibuni na watafiti wengine tokanchi za ulay ikiwepo Ujeremani na Uingereza .
“Wanakuja watafiti wanachukua dawa wanasema wamepata taarifa za dawa hizo wakiwa nchi kwao,” alisema Dudui.
Akizungumzia tiba hiyo, Dudui alisema bado inatolewa ingawa ni watu wachache wanaofika.
“Watu wanakuja na babu bado anasema kuna miujiza mingine itakuja na anaendelea na ujenzi wa kituo kipya cha tiba,” alisema Dudui.
Kampuni ya Simu ya Vodacom haitafunga huduma zake Kijiji cha Samunge , wilayani Ngorongoro, ambako maelfu ya watu walikuwa wakifika kupata kikombe cha tiba kwa Mchungaji Masapila licha ya sasa watu kupungua na wanaofika wengi ni watafiti.
Kampuni kadhaa ya simu zilifikisha huduma zake Samunge kuanzia Mei mwaka jana kutokana na kufurika kwa watu kupata kikombe cha tiba, lakini sasa baadhi ya kampuni zimesitisha huduma eneo hilo.
Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando, alisema wakazi wa Samunge wataendelea kupata huduma zote za kampuni hiyo.
“Ni kweli kuwa hivi sasa kuna wateja wachache Samunge na ni gharama kuendesha mtambo kule, lakini Vodacom hatutafunga mawasiliano kwani kuna wateja wetu wengi eneo hilo,” alisema Kamando.
Alisema wateja hao na wengine wa Mkoa wa Arusha na maeneo mengine, wamekuwa wakinufaika na huduma za kampuni hiyo, ikiwapo ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao.
Awali, Meneja wa Vodacom Arusha, Jerome Munishi, alisema kampuni hiyo mkoani hapa ina mawakala 600 ambao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali.

No comments:
Post a Comment