BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema,
uhakiki wa akaunti za wateja wa Benki nchini unaoendelea hivi sasa ni wa lazima
kwani unalenga kudhibiti fedha chafu, zinazoweza kuivuruga nchi.Hivi sasa benki
zote 47 zilizoko chini ya BoT zinafanya uhakiki wa akaunti za wateja wake kwa
kuchukua upya taarifa zao, kazi ambayo kwa mujibu wa taarifa za benki hiyo,
itafanyika kwa mwezi mmoja.Uamuzi huo wa BoT kuhakiki taarifa za wateja wa benki, umekuja siku chache tangu wabunge katika Mkutano wao wa Sita uliomalizika Ijumaa iliyopita, kuongeza makali katika Sheria ya Kudhibiti Fedha Chafu (Money Loundering Act) ya mwaka 2007.
“Ndiyo tumeagiza uhakiki huo wa akaunti zote za wateja wa benki nchini ambazo ziko chini yetu kuwa na rekodi za uhakika za wateja wao,” Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu alisema jana.
Hatua hiyo ya BoT pia imekuja kipindi ambacho baadhi ya benki zimetikiswa na wizi mkubwa wa mtandao wa kompyuta huku taarifa zikionyesha kuwa benki kubwa tatu za kimataifa, ziliwahi kuibiwa karibu Sh300 bilioni katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka juzi.
“Hata mimi (Gavana) nimeshatoa taarifa zangu kwa benki yangu. Huu ni utekelezaji wa Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu. Tunataka tupate urahisi wa kubaini mzunguko wa fedha chafu pale unapotokea.”
“Kwa mfano, kama fedha za Al Qaeda (mtandao wa ugaidi) zikipita kwenye akaunti yako (mwandishi), tukiwa na taarifa zako inaturahisishia sisi na vyombo vya dola kuzikamata kwa urahisi na kukuchukulia hatua za kisheria.”
Alisema wakati mwingine kukosekana kwa taarifa sahihi kwa wateja wa benki kunaweza kuwa tatizo kubwa katika kudhibiti fedha chafu, ndiyo maana kila benki inatakiwa kuhakiki hilo.
Mwaka 2007, Serikali ilipowasilisha Bungeni, kisha kutungwa kwa Sheria ya Kudhibiti Fedha Chafu, pia ilianzisha Kitengo cha Kudhibiti Fedha Chafu (Financial Intelligence Unit- FIU), ambacho kipo chini ya Hazina ambacho Profesa Ndulu alisema kimekuwa kikishirikiana na BoT na vyombo vingine vya dola kuhakikisha nchi haitikiswi na mzunguko wa fedha chafu.
“Sisi katika hili tunasaidiana na FIU na hazina, wajibu wetu ni usimamizi wa mabenki ndiyo maana tunataka kila moja litimize agizo letu. Kwa sababu wapo watu wanahama, wengine wanakufa na mambo mengi tu, sasa lazima kuwe na taarifa sahihi ili tuweze kujua nani yuko wapi,” alisema.
Gavana alisema katika mazingira ya sasa ambayo dunia imegubikwa na vitendo mbalimbali viovu ukiwamo ugaidi, ni vyema kukawa na mfumo salama wa kumbukumbu za fedha za wateja wote wa benki.
Alisema kuwepo kwa mfumo huo kutarahisisha mapambano dhidi ya fedha chafu ambazo zinaweza kutumika katika kutishia usalama wa nchi na hata vitendo vingine vya uhalifu.
Benki zatekeleza
Tayari benki nchini zimeanza utekelezaji wa agizo hilo la BoT kwa kutoa matangazo yenye kuhitaji taarifa za wateja wake ambazo ni pamoja na makazi yao kwa sasa, walikotoka kabla na hapo walipo wameishi kwa muda gani.
Katika utekelezaji huo, benki nchini pia zinamtaka kila mteja mwenye akaunti taarifa zake ziwe zinafahamika na kuthibitishwa na ofisa mtendaji wa kijiji, kata au mwajiri.
Pia wateja wanatakiwa kutoa taarifa zao mpya kwa kutaja vitu muhimu vilivyozunguka mahali wanakoishi kwa sasa, namba ya simu, barua pepe kwa wenye nazo, tarehe ya kuzaliwa na mwisho wa kujaza taarifa hizo ni Machi mwaka huu.
Adhabu
Alipowasilisha mabadiliko madogo ya Sheria ya Kudhibiti Fedha Chafu, Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema alisema adhabu ya kifungo inayopendekezwa katika makosa ya kukutwa na fedha za aina hiyo kisiwe chini ya miaka mitatu huku faini ikipendekezwa kuwa kati ya Sh100 milioni na isiyozidi Sh500 milioni.
Lakini, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alitaka adhabu itolewe kulingana na kiasi cha fedha alichokutwa nacho mhalifu huku akisema baadhi ya maghorofa Dar es Salaam pia yamejengwa kwa fedha chafu.
MWANACHAMA ATOKOMEA NA MICHANGO
MWENYEWE ALITOA SH2 MILIONI, SHEKIFU,
OLE SENDEKA NAO WALICHANGIA
Peter Saramba, Arusha
MMOJA wa wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, anadaiwa kutoroka na zaidi ya Sh26 milioni za jumuiya hiyo zilizochangwa kwenye harambee iliyofanyika Mei 9, mwaka juzi na kuongozwa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha. Akizungumza kwa simu kutoka Mererani, Simanjiro, Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Kiria Laizer alithibitisha kuwa fedha hizo zilizochangwa kwa lengo la kutunisha mfuko wa maendeleo ya vijana Simanjiro ziliyeyuka muda mfupi baada ya harambee hiyo.
Katika harambee hiyo, Nahodha ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alichanga fedha taslimu Sh2 milioni.
Ilielezwa kwamba wageni wawili waliohudhuria shughuli hiyo kwa mwaliko wa mtuhumiwa huyo ambao walitambulishwa ukumbini kuwa dada wa Rais Kikwete, walichangia 400,000.
Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za shughuli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu ambaye sasa ni Mbunge wa Lushoto (CCM), alichangia Sh500,000.
Viongozi wengine waliohudhuria na kiasi walichochanga kwenye mabano ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya (200,000), Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka (Sh1.5 milioni), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Ole Mukusi (Sh100,000).
Laizer alisema tukio la wizi huo limebaki kuwa kama mchezo wa kuigiza huku baadhi ya wanachama na viongozi wenzake wakimtuhumu hata yeye wakidhani alihusika kwa njia moja au nyingine.
“Baada ya mgeni rasmi (Nahodha) kunikabidhi mfuko wenye fedha usiku ule pale ukumbini, nilimwita (mtuhumiwa jina tunalo) na kumkabidhi mbele na wajumbe wawili wa kamati ya utekelezaji wilaya na tangu siku ile, sijawahi kumwona wala kupata mawasiliano naye,” alisema Laizer.
Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshuhudia makabidhiano hayo kuwa ni Bonny Shongo na Paul Sipitet.
“Siku tatu baadaye tulimtafuta (mtuhumiwa), bila mafanikio na tulipompata kwa njia ya simu alidai yuko Mjini Arusha kwa shughuli binafsi lakini baada ya muda mfupi alitutumia ujumbe mfupi wa simu akitutaka kutafuta mtu mwingine (wa kujaza nafasi yake) kwani yeye ameondoka,” alisema Sipitet.
Katibu wa UVCCM wilayani humo, Mwanakombo Amiri alisema kwa simu hakuna kumbukumbu yoyote kwenye majalada ya kiofisi inayohusu kikao cha maandalizi wala fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo.
“Hakuna chochote kwenye faili kuhusu jambo hilo unalouliza. Kikao kilichopita cha kamati ya utekelezaji kilizungumzia suala hilo ingawa haikuwa moja ya ajenda. Ila kikao kijacho ambacho siwezi kukutajia kitafanyika lini hilo ni moja ya ajenda muhimu na tutatoa uamuzi kulingana na kanuni zetu,” alisema Mwanakombo.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, ambaye ni miongoni mwa waliotafuniwa fedha zao walizochangia alithibitisha ofisi yake kupokea taarifa za fedha za kuyeyuka kwake na kusema tayari ameziagiza ngazi husika (UVCCM), kuchukua hatua kulingana na kanuni na taratibu zao na pia kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
“Sisi kama Serikali, chama kikichukua hatua na kuwasilisha taarifa, nitaagiza polisi wachukue hatua za kisheria kwa kuchunguza na kumtia mbaroni mtuhumiwa. Nakushauri pia uwasiliane na katibu wa CCM wilaya ambaye ndiye mlezi wa jumuiya zote za chama ngazi ya wilaya,” alisema Mandya.
Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya ofisi yake kutopata taarifa za utekelezaji wa amri yake ya mhusika kuchukuliwa hatua hadi sasa, ameamua kuuandikia barua rasmi uongozi wa UVCCM na chama wilaya kudai utekelezaji wa agizo lake kutokana na wahusika kuonekana wazito katika jambo hilo.
Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Jamila Mjungu alikataa kuzungumzia suala hilo akisema UVCCM ni jumuiya inayojitegemea, yenye viongozi na wasemaji na kanuni za kutatua matatizo yao.
Uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa huyo sasa ni diwani katika moja ya kata za Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambako aligombea na kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema ingawa jambo hilo halijaripotiwa kwake na uongozi wa wilaya ya Simanjiro, atafuatilia na kuhakikisha mhusika anachukuliwa hatua kulingana na kanuni za jumuiya hiyo na sheria za nchi bila kujali cheo, umaarufu wala nasaba yake na viongozi.
“Kwanza inawezekana mtuhumiwa ni tapeli mzoefu anayetumia jina la mheshimiwa Rais na familia yake kuwatisha

CHADEMA WAJITOSA ARUMERU
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza
ratiba yake ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha
huku wanachama wake wanne wakiwa tayari wamejitokeza kuomba kuteuliwa.
"Chama cha Chadema kinawahakikishia … kitashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Arumeru Mashariki, kwa lengo la kushinda,” alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika katika taarifa yake jana.
Alisema fomu zilianza kutolewa tangu jana na kwamba mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Februari 25.
Mnyika alisema fomu zinatolewa katika Ofisi ya Chadema ya Wilaya ya Arumeru, Maji ya Chai-USA River na pia katika Ofisi za Chadema za Mkoa wa Arusha.
“Baada ya hapo vikao vya chama vinavyohusika na uteuzi vitafanyika ili kumpata mgombea mmoja,” alisema.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo hilo, Jeremia Sumari.
Mnyika alisema anaamini umakini na uimara ambao kimeendelea kuudhihirisha katika kuwatumikia na kuwawakilisha Watanzania, kitashinda.
Mchakato wa uteuzi ngazi ya jimbo na wilaya utafanyika kati ya Februari 26 na 29, mwaka huu wakati uteuzi ngazi ya taifa utafanyika Machi 3 Machi mpaka 4.
Waliochukua fomu
Wanachama wa Chadema waliojitokeza kutaka kupeperusha bendera ya chama hicho ni Joshua Nasari, Samweli Shami, Francis Tembo na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Arumeru (Bawacha), Anna Mwagirwa.
Kujitokeza kwa wanachama hao wanne wa Chadema, kunafanya idadi ya waliojitokeza kuwania kiti hicho kufikia sita. Juzi, wanachama wawili wa CCM walichukua fomu kupitia chama hicho.
Waliojitokeza ni pamoja na mtoto wa Sumari, , Sioi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, William Ndeoya Sarakikya.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema Mkoa wa Arusha, Ephata Nanyaro alisema wanachama hao wanatarajiwa kuanza kupewa fomu za kugombea leo.
Alisema utaratibu wa kura kumpata mgombea wa chama hicho, unatarajiwa kutangazwa mara baada ya kukamilisha kikao cha sekretarieti ya Chadema, Dar es Salaam.
Sarakikya akana
Katika hatua nyingine, William Sarakikya aliyechukua fomu juzi kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, amesema kwamba si mtoto wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali, Mirisho Sarakikya.
Akizungumza jana mjini Arusha, Sarakikya alisema kwamba wote ni wa ukoo mmoja lakini hajazaliwa na Mkuu huyo wa majeshi wa zamani.
Wakati William akikanusha, Jenerali Sarakikya naye alisema jana kwamba mgombea huyo anatokea katika ukoo wake, lakini siyo mtoto wake wa kumzaa.
“Kimsingi ukoo wote wa Sarakikya ni ndugu lakini William siyo mtoto wangu wa kumzaa, ni mtoto wa jamaa yangu. Mimi nina watoto wanne ambao hawako kabisa kwenye siasa,” alisema Mstaafu huyo wa jeshi na kutaja kazi za wanaye hao kuwa ni udaktari, uhandisi ualimu na taaluma ya benki.

VIGOGO WA SERIKALI KUCHUNGUZWA
TUME ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeanza mchakato wa
kuhakiki mali za viongozi wa umma nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza itaanza
na vigogo 60 akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na
Waziri Samia Suluhu Hassan wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano). Wengine
ni wakuu wa mikoa na wilaya, Meya wa majiji, madiwani, wabunge na wakurugenzi
wa taasisi mbalimbali za Serikali.
Zoezi la uhakiki wa mali za viongozi hao litaanza Februari 20 hadi Machi mosi mwaka huu ambapo linafanyika baada ya kukamilika kwa zoezi la urejeshaji wa fomu za utajaji mali na madeni kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Serikali. Mbali na Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, wabunge wengine watakahakikiwa mali zao katika awamu hiyo ni John Mnyika(Ubungo), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Jerome Bwanansi (Lulindi), Faith Mitambo (Liwale) na Stella Manyanya (Viti Maalum).
Katika orodha hiyo yumo pia Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovock Mwananzila, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Didas Masaburi na Meya wa Jiji la Tanga, Guledi Mohamed. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Charles Nyamrunda, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema kuwa uhakiki huo ni nguzo bora ya kuijenga jamii ya Watanzania, hasa viongozi wa umma katika kuishi kwa kufuata misingi ya uadilifu, iliyowekwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Alisema kwa kuwa idadi ya viongozi ni kubwa na kwamba tume hiyo itaanza na uhakiki wa viongozi 60 wenye nyadhifa mbalimbali.
“Sisi tunachokiomba kutoka kwao ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wetu wakati wa zoezi zima la uhakiki wa mali zao,” alisema Kaganda. Alisema wananchi wanatakiwa kushirikiana na tume hiyo kutoa taarifa zitakazowasaidia kugundua mali zilizofichwa, ambazo zinadhaniwa kuwa ni za viongozi wa umma wanaoguswa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aliwataka viongozi wanaohakikiwa kutokuwa na hofu kwa kuwa zoezi hilo ni la kawaida.
“Hawa hawana tuhuma zozote ni utaratibu wa kawaida tu,”alisema. Jaji mstaafu Kaganda aliliambia gazeti hili kuwa si kosa kwa kiongozi yoyote wa Serikali kuwa na mali na kwamba kosa ni mali hizo kupatikana kinyume na sheria. “Mbunge akiwa mfanyabiashara na biashara yenyewe inafuata sheria hilo sio tatizo ila tukigundua mali hizo au biashara inafanyika kinyume na sheria tunaweza kuwaeleza Takukuru" alisema Kaganda.
Alisema kuwa kwa sasa uadilifu kwa viongozi wa umma umeshuka hivyo zoezi kama hilo kwa kiasi kikubwa linaweza kurudisha uadilifu huo. Katika hatua nyingine, Jaji Kaganda alisema anafanya utafiti wa sheria ya kutenganisha biashara na uongozi. “Nafanya utafiti kuhusu sheria hii ila kwa sasa ni mapema mno kueleza nilipofikia,” alisema Kaganda.

KASHFA MUHIMBILI KUCHUNGUZWA
UONGOZI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), umesema unayafanyia
uchunguzi madai ya mtoto Imrani Iddy kudungwa sindano iliyomsababishia kupoteza
fahamu na kupooza sehemu kubwa ya mwili kwa miezi sita na kuahidi kuwa taarifa
kamili itatolewa kesho.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu, amelazwa katika hospitalini hiyo chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) baada ya kuchomwa sindano hiyo, Julai 28, mwaka jana.
Awali, mtoto huyo alilazwa ICU ya moyo kabla ya kuhamishiwa wodini hapo, Januari 24 mwaka huu.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa MNH, Aminiel Aligaesha alikiri kupata taarifa hizo na kwamba, tayari uchunguzi umeanza na kesho atatoa taarifa.
“Mimi nikipata taarifa sahihi nitakupa Jumatano (kesho) kwa sasa tunalifanyia uchunguzi suala hilo,” alisema Aligaesha.
Hatua hiyo ya uongozi wa Muhimbili kuanza uchunguzi wa tukio hilo, imetokana na habari iliyochapishwa juzi na gazeti hili, ikinukuu vyanzo mbalimbali, ikiwemo mama wa mtoto huyo, Amina Mwerangi kudai kuwa mwanawe alidungwa sindano hiyo na kupooza miezi sita iliyopita.
Ushuhuda wa mama
Amina ambaye aliwahi kuwa mshindi wa mashindano ya ulimbwende Mkoa wa Ruvuma mwaka 2003/04, alisema alimpeleka mwananwe Muhimbili kwa ajili ya upasuaji mdogo wa nyama zilizoota puani.
"Baada ya kuchomwa sindano hiyo, mtoto alipatwa na mshtuko (cardiac arrest) yaliyosababisha mapigo ya moyo wake kusimama. Tatizo hilo sasa limemletea mtindio wa ubongo na kupooza mwili wote," alisema Mwerangi.
Mwerangi alisema jitihada zake kumpata daktari aliyemchoma sindano hiyo, hazikuzaa matunda na daktari mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Edwin aliyekuwa amfanyie upasuaji huo, hataki kujihusisha tena na tatizo hilo.
“Mtoto amekaa ICU kwa miezi sita sasa bila matumaini yoyote ya kupata nafuu, lakini jambo la kushangaza madaktari hawataki kumpa rufaa ili apelekwe nje kwa ajili ya matibabu," alisema Mwerangi.
Akisimulia mkasa huo, Mwerangi alisema alifika Muhimbili Julai 28, 2011 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji mdogo.
Mgonjwa huyo alifunguliwa jalada IP.No.A586301 lililoeleza kuwa alikuwa na tatizo la kuota nyama kwenye njia ya hewa (puani) zilizomfanya zilizomsababishia kupata taabu kupumua.
Alisema mtoto huyo ambaye kabla ya tatizo hilo jipya alikuwa akisoma katika Shule ya Awali ya Mt.Thomas mjini Dodoma, alibainika kuwa na ugonjwa huo wa kuota nyama puani wakati akianza kutambaa.
“Baada ya kumpeleka Muhimbili katika kliniki ya kawaida, walinishauri afanyiwe upasuaji mdogo ili kuondoa nyama hizo. Ndipo Julai 28, mwaka jana nilipofika hospitalini hapo kwa ajili ya huduma hiyo,” alisema na kuongeza:
“Nilipokewa na kesho yake Julai 29 ndipo alipelekwa chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa huduma hiyo, lakini kabla ya hapo, alipigwa sindano ya usingizi iliyomsababisha apate Cardiac arrest.”
Mwerangi, alisema taarifa ya kitabibu baada ya kufanyiwa vipimo vya 'CT Scan', ilibaini mtoto huyo amesababishiwa tatizo la mtindio wa ubongo na kwamba mwili wote umepooza.
“Kila nikiuliza ni daktari gani aliyempiga sindano hiyo sipewi jibu, kila mmoja anasema hajui ila walimkuta tu ndani ya chumba cha upasuaji akiwa hivyo. Badala yake wananiuliza kuwa kwani dereva akisababisha ajali na watu wakafa yeye akapona atasimama?,” alidai Mwerangi
Alisema mbali na kumfichwa daktari aliyemchoma sindano mwanawe, amekuwa akinyimwa ruhusa ya kumpeleka mtoto huyo nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment