Tuesday, March 13, 2012

JK AAGANA NA MABALOZI

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi wanne wapya wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Mabalozi hao waliapishwa hivi karibuni. Mabalozi wapya walioagana na Rais Kikwete ni pamoja na Mhe.Philip Marmo anayekwenda China, Mhe.Grace Mujuma anayekwenda Zambia, Mhe.Mohamed Haji Hamza anayekwenda Misri na Mhe.Dkt.Batilda Burian anayekwenda Kenya. Katika picha juu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini China Mhe.Philip Marmo ikulu jijini Dar es salaam leo aasubuhi





Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Mhe.Dkt.Batilda Burian ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe.Mohamed Haji Hamza ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi

No comments: