KUPELEKA ZIGO LA MIGOGORO YA ARDHI KWA KIKWETE, VIJEMBE KWA CHADEMA VYATAWALA
Waandishi Wetu, Arumeru
MJI wa Usa River katika Wilaya ya Meru jana ulitikiswa na kishindo cha uzinduzi wa kampeni za CCM, ulioongozwa na Mwenyekiti wake Mstaafu, Benjamin Mkapa.Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ngaresero, Mkapa alikanusha kuwa na ubia na kampuni ambazo zimewekeza katika maeneo makubwa ya ardhi ya Meru.Suala la migogoro ya ardhi ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayowakabili wananchi wa wilaya hii na jana Mkapa alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kukanusha kwamba ana ubia na wale aliowaita kuwa ni walowezi katika wilaya hiyo.

“Kwanza
kabisa nataka niweke mambo sawa, nimesikia kwamba ninahusishwa na hawa
wamiliki wa ardhi, eti kina nani hawa… ndiyo Jerome sijui Jerome, huu ni
uzushi na hauna ukweli wowote,” alisema Mkapa alipokuwa akimnadi
mgombea wa CCM, Sioi Sumari na kuongeza:
“Mimi katika nchi hii
sijawahi kumpokonya mwananchi yeyote shamba, wala kumnyanyasa Mtanzania
yeyote kwa kumpokonya ardhi, nimekuwa mtetezi wa kuhakikisha kila watu
wanapata haki ya matumizi yao ya ardhi, haya maneno mengine ni uzushi na
upuuzi wa hali ya juu.”
Alisema amepokea taarifa za kuwapo kwa
migogoro mikubwa ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya wawekezaji
kuhodhi maeneo makubwa na kusema atalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM,
Rais Jakaya Kikwete na kumshauri achukue hatua kwa kuwawajibisha
watendaji wa Serikali ambao wameshindwa kuwajibika na kuchukua hatua kwa
wawekezaji waliokiuka masharti.
“Yapo matatizo kadha wa kadha,
wapo wawekezaji ambao wamehodhi maeneo makubwa wakati hawayatumii, wapo
ambao wamechukua maeneo na kubadilisha matumizi yake na wapo ambao
wamekiuka sheria za uendeshaji wa maeneo waliyopewa,” alisema Mkapa na
kuongeza:
“Yote haya nimeyapokea na nitayafikisha kwa Mwenyekiti
wangu wa CCM ambaye pia ni Rais wangu ili ayashughulikie baada ya
uchaguzi maana tukifanya sasa, hawa wenzetu (wapinzani) watasema
tumewahonga wananchi.”
Aidha, Mkapa alikanusha taarifa kwamba
alitoa masharti baada ya kuombwa kuongoza uzinduzi wa kampeni hizo za
CCM: “Mimi ninamheshimu sana Mwenyekiti wangu wa CCM na uamuzi wa Kamati
Kuu ya chama maana nimezaliwa CCM na kukulia ndani ya CCM. Kwa maana
hiyo siwezi hata siku moja kuhoji au kutoa masharti pale ninapoombwa na
chama kutekeleza jukumu lolote.”
Shamrashamra
Shamrashamra za CCM zilianza asubuhi kwa magari na pikipiki zilizopambwa kwa bendera za kijani na njano kupita katika mitaa mbalimbali ya Usa River, zikiwahamasisha wakazi wa mji huo kuhudhuria uzinduzi huo.
Mapema viongozi kadhaa wa chama hicho walitawanyika katika kata zote 17 za Arumeru Mashariki kulifanya mikutano ya ndani kwa lengo la kuwaweka sawa makada wao ambao wanadaiwa kuchanganywa na taarifa kwamba chama hicho kimegawanyika kuhusu mgombea wao, Sioi Sumari.

Baadaye mchana,
msafara wa mgombea huyo wa CCM ulianza kuelekea katika eneo la mkutano
ukitokea katika Hoteli ya Gateway ukisindikizwa kwa magari na pikipiki.
Kabla
ya msafara huo kuondoka, kulikuwa na kikao cha ndani kilichofanyika
hotelini hapo kikiwahusisha viongozi wa chama hicho na taarifa za ndani
zinadai kwamba kilikuwa kikipanga mikakati ya mkutano huo wa uzinduzi.
Msafara huo ulitoka hotelini hapo saa 9.15 alasiri na kuingia Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, njia ya Leganga na kuelekea moja kwa moja katika Ngarasero.
Wakati msafara huo ukiwa Barabara ya Leganga ukielekea uwanjani, ulipita karibu na kambi waliyofikia viongozi mbalimbali wa Chadema na baadhi ya makada wa chama hicho walijitokeza na kuzomea msafara huo.
Msafara huo uliwasili uwanjani hapo robo saa baadaye na viongozi wake waliungana na wanachama wao waliokuwa uwanjani hapo tayari kwa uzinduzi.
Wapinzani wa Sioi
Katika uzinduzi huo, CCM kiliwapandisha jukwaani baadhi ya wanachama wake waliokuwa wapinzani wa Sioi kwenye kura za maoni. Makada hao ni Elishilia Kaaya, Elirehema Kaaya na William Sarakikya na wote waliuthibitishia umma kumuunga mkono mgombea huyo wa CCM.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa
aliwaomba wana Arumeru Mashariki kulinda mila na desturi iliyojengeka
ndani ya taifa kuwa inapotokea kiti cha uongozi kama ubunge
kinachomilikiwa na CCM inabaki wazi, mrithi atoke ndani ya chama hicho.
“Mila
na desturi zinataka mrithi wa kiti kinachomilikiwa na CCM kirithiwe na
mrithi kutoka CCM. Mchagueni Sioi kutekeleza hilo ili ashirikiane na
wenzake bungeni kutatua matatizo yenu,” alisema.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema tayari chama hicho kimetekeleza ahadi na deni kililokuwa nalo kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremia Sumari ambaye ni baba mzazi wa Sioi kwa kulipa Jimbo la Arumeru Mashariki hadhi ya kuwa wilaya kamili kichama.

Vijembe kwa Chadema
Meneja wa kampeni za CCM Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba aliwapiga vijembe viongozi wa Chadema akimwomba Mkapa kumsihi Rais Kikwete awateue Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ili wasije kulalamika pale mgombea wao atakaposhindwa.

Mwigulu alitumia maneno mengi ya kejeli kwa
Chadema na mgombea wake, Joshua Nassari kwa kumfananisha na vitu kama
shetani, gunzi na vinyamkera huku akiwasihi wapiga kura kutomchagua
mgombea huyo.
Nchemba ambaye pia ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa
CCM, alisema CCM kina uhakika wa ushindi katika jimbo hilo kwani mgombea
wake, anakubalika.
Alisema licha ya kuwepo matatizo kadhaa
Arumeru, hoja si kusema kwa ukali, bali ni kuwa na mipango ya
kukabiliana na matatizo hayo... “Chagueni mtu ambaye atasikilizwa na
Serikali na mtakayeshirikiana naye kutatua matatizo na sio mtu ambaye
anasema kwa ukali ambaye anapotosha jamii.”
Kuhusu uchangishaji wa fedha uliofanywa na Chadema wakati wa uzinduzi wa kampeni, alisema ni kejeli kwa wananchi kuwachangisha Sh50 wakati wanatumia helikopta ambayo kwa saa moja angani gharama zake ni Sh2.5 milioni na Sh15 milioni kwa siku.

Ahadi za baba
Mgombea huyo wa CCM, alisema kipaumbele cha kwanza akichaguliwa ni kutekeleza ahadi zote alizoacha baba yake... “Najua nina deni kwenu, mkinichagua nitahakikisha ninakamilisha ahadi zote za baba kama kukamilisha Barabara ya Ngabobo, ujenzi wa nyumba ya wazee wa mila, kukamilisha ujenzi wa vyoo katika shule na kukamilisha ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Songoto.”
Mgombea huyo pia alisema
ajenda kubwa ambayo atatekeleza baada ya kuchaguliwa itakuwa ni
kushughulikia matatizo ya maji na ajira kwa vijana katika jimbo hilo.Mgombea huyo wa CCM, alisema kipaumbele cha kwanza akichaguliwa ni kutekeleza ahadi zote alizoacha baba yake... “Najua nina deni kwenu, mkinichagua nitahakikisha ninakamilisha ahadi zote za baba kama kukamilisha Barabara ya Ngabobo, ujenzi wa nyumba ya wazee wa mila, kukamilisha ujenzi wa vyoo katika shule na kukamilisha ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Songoto.”

No comments:
Post a Comment