Thursday, April 26, 2012

MUUNGANO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Haraiki ya  wanafunzi wapatao  1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani  wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika  leo katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo

No comments: