Wednesday, January 25, 2012

KUISAIDIA POLISI SIO KUWEKWA LOCK UP

Thobias Andengenye, Kamanda wa polisi mkoa waArusha



Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye ametolea ufafanuzi suala la kuisaidia polisi na kusema kuwa si kila anayeisaidia polisi analazimika kukaa selo.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio 5 kamanda Andengenye amesema suala lililopo ni aina ya ushahidi unaotafutwa na polisi na kuongeza kuwa watu wengi wanaisaidia polisi na wako nyumbani.
Mkuu huyo wa polisi ameeleza kuwa endapo mtu atatakiwa kuisaidia polisi na ushahidi wake umsaidie kumsafisha au kumtia hatiani mtu huyo huwekwa ndani kulinda taarifa ambazo polisi inakuwa nazo.
Kituo hiki kiliamua kutafuta ufafanuzi wa suala hilo kutokana na maswali ambayo watu wamekuwa wanahoji kuhusu mtu kuisaidia polisi kwanini anawekwa chini ya ulinzi wa  jeshi hilo.

No comments: