Tuesday, January 31, 2012

MGOMO WAENDELEA

Waziri mkuu mh.Mizengo Pinda.

DAR ES SALAAM:      

Madaktari katika baadhi ya maeneo nchini wameendelea na mgomo wao licha ya agizo la waziri mkuu kuwataka kurejea katika vituo vyao vya kazi hapo jana ,na kwamba atakayeshindwa kufanya hivyo atakuwa amejiondoa  mwenyewe katika utumishi wa uma.
Katika hopsitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam  mgomo wa madaktari umeendelea kama kawaida hapo jana ,huku hali ya wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo ikizidi kuwa mbaya na baadhi yao kufariki dunia.
Hata hivyo mgomo huo umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wauguzi katika hospitali hiyo kungana na madakatari katika mogomo huku baadhi yao wakipinga hatua ya kutaka kuletewa madaktari kutoka jeshini.
Katika baadhi ya mikoa ikiwemo Mbeya , Mwanza na Kilimanjaro baadhi ya madaktari wameonekaana kusaini vitabu vya mahudhurio na kuondoka bila ya kuwahudumia wagonjwa.

No comments: