SUMARI AAGA DUNIA.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arushai Mh. JEREMIAH SUMARI amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya Kisukari.
Marehemu SUMARI alizaliwa Machi 2 mwaka 1943 katika kijiji cha AKERI wilayani Arumeru Mkoani Arusha, enzi za uhai wake amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ,ikiwemo Waziri wa kazi Ajira na Maendeleo ya vijana.
Pia aliwahi kuwa Naibu waziri wa Fedha na Uchumi kati ya mwaka 2008 hadi 2010 ambapo mpaka mauti yanamfika usiku wa kuamkia leo alikuwa ni mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki.
Kufariki kwa mbunge huyo kunafanya idadi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania waliopoteza maisha kwa mwaka huu pekee kufikia wawili ,mara baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa morogoro viti maalumu REGIA MTEMA ambaye alifariki wiki iliyopita kwa ajali ya gari.
Radio 5 inawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na wananchi wote wa jimbo la Arumeru Magharibi
Bwana ametoa ,na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina!

No comments:
Post a Comment