JAN 10, 2012
Serikali imesaini mkataba na shirika la
hifadhi ya jami NSSF kwaajili ya ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini dar es
salaam.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF dakta Ramadhan Dau
amesema ujenzi wa daraja hilo ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi
bilioni mia 2,utakamilika katika kipindi cha miaka mitatu.
Ameongeza kwamba ujenzi huo utatekelezwa kwa
ushirikiano baina ya wakandarasi wa hapa nchini na china.
Kwa upande wake waziri wa ujenzi Dakta JOHN MAGUFULI amewataka wakandarasi hao
kutekeleza ujenzi huo kwa wakati na pia katika kiwango kinachotakiwa........................................................................................................................................
Katibu mkuu wa baraza la mitihani Dr. joyce ndalichako
JAN 10,2012
Wanafunzi elfu tisa waliofutiwa matokeo ya
kuhitimu elimu ya msingi mwishoni mwa mwaka jana wanataraji kurudia mtihani huo
mwaka huu mwezi September.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
PHILIP MULUGO ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri MULUGO amesema hatua hiyo ya
serikali inalenga kuwapa fursa nyingine
wanafunzi ambao wamepoteza nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari mara baada ya kufutiwa matokeo yao.
Katika hatua nyingine MULUGO amesema
utaratibu wa kawaida utatumika kuwahamisha wanafunzi walioathirika na janga la
mafuriko jijini dare s salaam,na kuwapatia nafasi katika shule za jirani na makazi yao mapya
watakayo hamia.
.....................................................................................................................................
Maalim Seif kushotom akiwa na mwenyekiti wa chama cha wana nchi (CUF) Prf.Ibrahim lipumba.
ZANZIBAR: JAN 10, 2012 SAA 1 ASUBUHI
Makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar MAALIM
SEIF HAMAD amesema wakati umefika kwa wazanzibar kuacha utegemezi kwa wahisani katika kupanga na
kutekeleza miradi ya maendeleo.
Maalim Seif ametoa
kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa jengo la Mfuko wa Barabara lililogharimu zaidi
ya shilingi millioni mia 6 Mjini Unguja ambalo limebuniwa na kujengwa na
wataalam wazalendo.
Amesema iwapo kutakuwa na jitihada za
makusudi katika kupanga mipango kwa mujibu wa hali ya kifedha wataweza
kutekeleza miradi ya kimaendeleo kwa uhakika na haraka.
Maalim seif Amesema
ujenzi wa jengo hilo umegharamiwa na Mfuko wenyewe bila ya kutegemea wafadhili
na kujengwa kwa muda wa chini ya mwaka mmoja.

No comments:
Post a Comment