Wiliam Ruto
THE HAGUE
Mahakama ya kimataifa ya jinai ya
ICC imewakuta na kesi ya kujibu Wakenya wanne mashuhuri.
Wakenya hao ni aliyekuwa waziri
William Ruto, mwandishi wa habari Joshua Sang', mkuu wa utumishi wa umma
Francis Muthaura na naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta.
Ushahidi uliowasilishwa na upande wa
mashtaka dhidi ya aliyekuwa waziri Henry Kosgey na mkuu wa zamani wa polisi
Meja Jenerali mstaafu Mohammed Hussein Ali haukutosha kuanzisha kesi dhidi ya
wawili hao.
Akitoa uamuzi huo kwa niaba ya jopo
la majaji, jaji Ekaterina Trendafilova alisema kulikuwa na sababu za kuamini
kwamba washukiwa William Ruto na Joshua Sang' huenda walichangia katika madai
ya kuwatimua watu wa jamii ya Wakikuyu, Wakamba na Wakisii ambao walikuwa na
misimamo tofauti ya kisiasa.
Katika kesi ya pili dhidi ya Uhuru
Kenyatta na Francis Muthaura, mahakama ilisema huenda wakawa na mkono katika
madai ya mateso dhidi ya binadamu na kuwatimua watu kwa nguvu kutoka makaazi
yao.
by Philip Magese

No comments:
Post a Comment