Field Marshal Tantawi.
Nchini Misri Waandamanaji wamerejea
katika mitaa ya mji mkuu Cairo kuonyesha hasira yao juu ya maisha yaliyotokomea
jana kwenye mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu.
Watu sabini na wanne walipoteza
maisha yao katika uwanja wa mpira ulio katika mji wa kaskazini mashariki wa
Port Said.Mamiya wengine walijeruhiwa.
Kwenye kikao cha dharura cha bunge,
Waziri mkuu wa nchi hio ametangaza kua wanakamati wa Chama cha mpira cha nchi
hio wote wamefutwa kazi na wanachunguzwa. Gavana wa mji wa Port Said
amejiuzulu.
Waziri Mkuu wa Misri Kamal Ganzouri
ametangaza hatua ya kuwafuta kazi wanachama wote wa chama cha mpira cha Misri
na kujizulu kwa baadhi yao kwenye Kikao cha dharura cha Bunge.
Hatua hio hata hivyo huenda isitoshe
kuwaridhisha Wamisri wengi. Kuna dalili la kuongezeka kwa ghadhabu ya wa Misri
juu ya Wizara ya mashauri ya nchini inayosimamia Polisi, ambayo wengi wanahisi
haijabadilika tangu enzi za Hosni Mubarak.
Na ghadhabu hizo zimemuelekea kiongozi wa Misri wa kijeshi Field Marshall
Tantawi. Mashabiki wa klabu ya Al Ahli, ambao wenzao walishambuliwa mjini Port
Said, wameanza safari ya miguu kuelekea medani ya Tahrir na makao ya Wizara ya
masuala ya ndani.
Wabunge kutoka chama cha Muslim Brotherhood wanaongoza katika kuikashifu
serikali bungeni. Kila mmoja anahofia kua huenda haya yakazua duru mpya ya
malumbano ya mitaani. Pamoja na hayo, hali hii inazidi kupunguza matumaini ya
mchakato wa mageuzi ya utawala kutoka mikononi mwa Wanajeshi na kukabidhiwa
raia.

No comments:
Post a Comment