Baada ya baadhi ya wadau kupinga vikali nyongeza ya posho za za wabunge,mambo yamezidi kuwa moto baada ya kuibuka mgawanyiko juu ya suala hilo linalotikisa taifa kwa sasa...Mbunge wa kigoma kaskazini Zito Kabwe jana aliandika katika katika mtandao wa kijamii wa face book kuwa hotoogopa kusema ukweli juu ya nyongeza hiyo aliyodai kuwa aistahili na nikuwanyonya wananchi.
Kwa upande
mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la
posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na
mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana
nalo kwasasa. CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa
ya Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya
swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya kuwawakilisha
bungeni. CCM inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala
hili na busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza sauti
za Watanzania kwani huko bungeni wana wawakilisha hawa Watanzania, ni vizuri
kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza kilio cha waliokupa dhamana ya
kuwawakilisha. Msimamo wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika
na mchakato huo ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza, yeye
katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao walitafakari hili
na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.

No comments:
Post a Comment