WENGINE WAWILI WAUAWA, WANAHARAKATI WATAKA RC, DC, IGP WAFUKUZWE KAZI
HALI katika Mji wa Songea, Ruvuma bado ni tete. Baada ya watu wanne kuuawa na polisi Jumatano iliyopita, watu wengine wawili wameuawa kwa kupigwa na wananchi juzi.Watu hao ambao ni wanaume, walishambuliwa kwa marungu, mawe na mapanga na kufariki dunia baadaye wakiwa kwenye matibabu. Wananchi waliwashambulia baada ya kuwatuhumu kuhusika na vitendo vya mauaji mkoani humo.
Juzi, Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma liliwakamata na kuwaweka mahabusu askari wake wanne wanaotuhumiwa kutumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu wanne Jumatano wiki hii, wakati wananchi waliokuwa wakipinga mauaji dhidi ya wenzao tisa kwa imani za kishirikina walipopambana na polisi. Watu 41 kujeruhiwa.
Fujo za juzi zilitokea katika Mtaa wa Mkuzo, Songea mara baada ya wananchi kuwakamata watu hao wawili ambao walishindwa kujieleza wakati wakihojiwa. Mbao ya hao, pia alikuwepo mwanamke mmoja ambaye alifanikiwa kutoroka.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao walijitetea kuwa wao ni mafundi ujenzi na walikuwa wakimtafuta mtu ambaye hata hivyo, walishindwa kumtaja jina ili awauzie kiwanja. Baada ya kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha, wananchi waliwataka waeleze walipotoka na wameshaua watu wangapi.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mkuzo, John Moyo alisema wananchi hao walifanya fujo hizo kwenye ofisi yake baada ya kuwafikisha.
Moyo alisema wananchi walipowahoji na kuona wakishindwa kujieleza walianza kuwashambulia kwa kuwapiga na kuwajeruhi vibaya.
Baada ya kushindwa kuwadhibiti, alisema alipiga simu polisi ambao walipowasili eneo la tukio walilazimika kuwatawanya wananchi hao kwa mabomu ya kutoa machozi na kuwapeleka watu hao hospitali.
Wakiwa hospitalini, watu hao walifanyiwa upekuzi na kukutwa wakiwa na hirizi moja kubwa rangi nyeusi pamoja na karatasi nyeupe iliyoandikwa kwa lugha ambayo haikuwa rahisi kusomeka.
Walipoulizwa majina yao, mmoja alisema anaitwa Juma na mwenzake ni Gervase. Katika hali iliyoashiria kuwa Gervase hakutaka atajwe, alimuashiria mwenzake kwa kumbana na pingu.
Wakati huo Gervase alikuwa amevimba uso na alionekana kuishiwa nguvu na hali yake kuzidi kuwa mbaya.
RPC, hosipitali
Baadaye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk Benedicto Ngaiza alisema Gervase alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu mapokezi na mwenzake Juma pia aliaga dunia saa chache baadaye.
“Haikuwa rahisi kwa watu hao kupona kwani hali zao zilikuwa mbaya sana. Walikuwa wamejeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na vifo vyao vimetokana na kupoteza damu nyingi,” alisema Dk Ngaiza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda amethibitisha kutokea kwa tukio akiwasihi wananchi waache kuchukua sheria mkononi na badala yake watii sheria bila kushurutishwa pindi wanapomuhisi mtu kuwa ni mhalifu.
“Kwa kweli nasikitishwa na kuumizwa sana na matukio yanayoendelea. Naomba wananchi watulie waache kuuana kwani vitendo hivyo ni vya kinyama na ni uvunjifu wa amani. Tunawaomba wasaidiane na polisi ili tuweze kudhibiti au kutokomeza kabisa wimbi hili la mauaji katika mji wetu,” alisema Kamhanda.
Vikao
Kutokana na wasiwasi uliotanda katika Mji wa Songea, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu kwa upande mmoja na Kamanda Kamhanda kwa upande mwingine jana kutwa waliripotiwa kushinda katika vikao tofauti vyenye lengo la kurejesha utulivu.
Mwambungu alikuwa na kikao na waendesha pikipiki maarufu kwa jina la Yeboyebo jana mchana katika Ukumbi wa Klabu ya Songea ambacho kilikuwa kikihamasisha ulinzi shirikishi ili kukomesha mauaji hayo.
“Madreva pikipiki mna mchango mkubwa sana maana abiria wenu walio wengi mnawafahamu vilivyo hivyo ni vyema kama kuna mtu mna wasiwasi naye mkatoa taarifa polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa,” alisema Mwambungu.
Kamhanda kwa upande wake alikuwa na vikao tofauti katika kambi za polisi na mara ya mwisho ilielezwa kwamba alikuwa Ofisi za Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Songea.
Katika hatua nyingine, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Augustine Songea, wamelalamikia milipuko ya mabomu ya juzi jioni kwamba iliwaathiri kwenye mitihani.
Mmoja wa wanafunzi hao, Hofe Seregius alisema milipuko ya mabomu ambayo yalitua jirani na chuo chao na kwamba yaliwafadhaisha kiasi cha kushindwa kuendelea na mitihani ya historia, hivyo wanataka uongozi wa chuo kuwaruhusu kurudia mtihani huo.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Donatus Komba alikiri kuwapo kwa taharuki kwa wanafunzi akisema Polisi walitumia nguvu kubwa dhidi ya wananchi.
Wanaharakati waja juu
Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika (SAHARiNGON) umelaani kitendo cha polisi kuua raia kwa risasi katika maandamano hayo na kumtaka Rais kuwawajibisha Mkuu wa Mkoa Ruvuma na Kamanda wa Polisi wa Mkoa kwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.
Watendaji wengine waliopendekezwa kuwajibishwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Thomas Ole Sabaya na watendaji wakuu wa Manispaa ya Songea.
Akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana, Mratibu wa SAHRiNGON Tawi la Tanzania, Martina Kabisama alisema wahusika hao wameshindwa kutimiza wajibu wao jambo lililosababisha wananchi kuandamana kwa amani na kushambuliwa na polisi.
Alisema taarifa za matukio ya watu kuuawa kwa kile kilichoelezwa ni imani za kishirikina zilianza kujitokeza Novemba mwaka jana na taarifa zilifika polisi na hadi wananchi wanafikia hatua ya kuandamana, wahusika hawakuonekana kuchukua hatua.
“Ni jambo la kushangaza kwa polisi hao kwenda kuvamia maandamano ya amani na kuua raia. Kitendo hicho tunakilaani sababu wananchi waliandamana kwa amani ikiwa ni namna yao ya kupaza sauti baada ya polisi kushindwa kuchukua hatua dhidi ya matukio hayo,” alisema.
Alisema kitendo hicho cha polisi ni kinyume na haki ya kuishi kama ilivyoelekezwa katika Ibara ya 13 ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977.
Alisema kitendo hicho pia kimekiuka haki ya mkusanyiko kama inavyoelezwa katika Ibara ya 21 kifungu cha kwanza, haki ya kusikilizwa na kutoa maoni Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema tukio la maandamano na vurugu zilizotokea ni matokeo ya Serikali kushindwa kuchukua hatua kwa wakati tangu mauaji ya raia yaliyohusishwa na imani za kishirikina yalipoanza kutokea Novemba mwaka jana.
Kabisama alishauri viongozi na watendaji serikalini kujenga utamaduni wa kuchukua hatua dhidi ya matukio mbalimbali yanapotokea kabla ya kusababisha athari.
“Kumejengeka tabia ya Serikali kuchukua hatua baada ya migomo na maandamano kutokea. Tumeshuhudia mgomo wa madaktari watu wamekufa ndipo Serikali inachukua hatua na hili la Songea watu wameandamana na kupoteza maisha ndipo Serikali inachukua hatua. Kitendo hiki cha kushindwa kuchukua hatua kwa wakati ndicho kinacho sababisha wananchi kuchukua sheria mkononi,” alisema.
CCK chapanga kushtaki polisi
Chama cha Kijamii (CCK) kimesema kinatarajia kulishtaki Jeshi la Polisi mara baada ya kukamilika kwa mpango wa ukusanyaji wa taarifa kuhusu mauaji yaliyofanywa na Polisi huko Songea.
Mwenyekiti wa CCK, Constantine Akitanda alisema jana katika taarifa yake: “Hatua ya kulipandisha jeshi la Polisi kizimbani itakuwa ni tukio la kihistoria katika kuitikia wito wa kutetea haki za wananchi wetu.” Hata hivyo, hakusema ni lini hatua hiyo itachukuliwa.
Alisema chama hicho kimependekeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iingilie kati sakata hilo ili kujua ni kwa namna gani wahusika mbalimbali walivyochangia mauaji hayo.
“Pia Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu achunguzwe kuhusu kauli yake kwamba polisi waliwaua wananchi waliokuwa wakiandamana kuelekea kwenye majengo ya Serikali,” alisema Akitanda.
Akitanda alisema chama hicho pia kinapendekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema kuhojiwa kuhusu matukio ya mauaji ya polisi ambayo yamekuwa yakifanywa mara kwa mara hapa nchini.
HALI katika Mji wa Songea, Ruvuma bado ni tete. Baada ya watu wanne kuuawa na polisi Jumatano iliyopita, watu wengine wawili wameuawa kwa kupigwa na wananchi juzi.Watu hao ambao ni wanaume, walishambuliwa kwa marungu, mawe na mapanga na kufariki dunia baadaye wakiwa kwenye matibabu. Wananchi waliwashambulia baada ya kuwatuhumu kuhusika na vitendo vya mauaji mkoani humo.Fujo za juzi zilitokea katika Mtaa wa Mkuzo, Songea mara baada ya wananchi kuwakamata watu hao wawili ambao walishindwa kujieleza wakati wakihojiwa. Mbao ya hao, pia alikuwepo mwanamke mmoja ambaye alifanikiwa kutoroka.

MWISHO WA ANTENA ZA KAWAIDA
2013
LUNINGA au televisheni za teknolojia ya analojia zenye `matumbo’ hazitafanya kazi kuanzia Januari Mosi, 2013 hadi ziunganishwe na ving’amuzi vitakavyonunuliwa kutoka kwa kampuni ambazo ni wakala wa vituo vya televisheni.
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa kutangaza kusitishwa kwa matangazo ya Televisheni kwa kutumia analojia kwenda digitali kuanzia Januari Mosi 2013.
Akizungumza na Mwananchi kuhusu kauli hiyo ya Waziri, mtaalam wa vifaa vya elektroniki, Damas Mligo alisema zile luninga za zamani itabidi ziunganishwe na ving’amuzi ndipo zifanye kazi. Bei ya ving’amuzi katika kampuni mbalimbali zinaanzia Sh70,000.
Alisema kuna baadhi ya luninga za digitali ambazo ving’amuzi vimejengewa ndani hizo zitatumika kama kawaida.
Waziri Mbarawa aliwataka wananchi kujiandaa mapema hasa kununua ving’amuzi kwa luninga ambazo zinatumia teknolojia ya analojia.
Alisema faida ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo na ongezeko la vituo vya televisheni.
Aidha Mbarawa alisema faida nyingine ya kuingia kwa teknolojia ya digitali ni matangazo ya televisheni kupatikana katika wingi zaidi vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti.
“ Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa ifikapo Desemba 31, 2012 saa sita kamili usiku vituo vyote vya utangazaji vinavyotumia teknolojia ya analojia vitazima mitambo yake na kutumia digitali,”
alisema Profesa Mbarawa.

SHELUKINDO HALI BADO TETE
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ametakiwa kuripoti katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ifikapo Machi 7 mwaka huu, ili kusikiliza hukumu ya kesi ya madai inayomkabili.
Shelukindo anadaiwa kushindwa kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwenye benki ya Azania mwaka 2005.
Hakimu wa mahakama hiyo, Joyce Minde alisema hukumu ilishatolewa na mahakama hiyo ambayo ilimamuru Shellukindo kulipa deni analodaiwa na benki hiyo, lakini hadi sasa ameshindwa kutekeleza amri hiyo.
“Hiyo kesi siyo ngeni, ni kesi ya madai namba 92 ya mwaka 2005 na ilishatolewa hukumu. Tunachofanya sasa ni kukazia hukumu tu,” alisema Minde na kuongeza:
“Kuna njia mbalimbali za kukaza hukumu kama vile kukamata mali za mdaiwa, mfano nyumba au kufungwa jela.”
Alisema; “Nitasikiliza utetezi wake na nitatoa hukumu kulingana na uzito wake. Kama hauna uzito mahakama itachukua hatua kali, ili alipe deni hilo.”
Hata hivyo, Minde hakuweka wazi kuwa hukumu ya kwanza ilisomwa lini kwa maelezo kuwa, yeye hakuwapo wakati hukumu hiyo ilipotolewa.
Kwa upande wa Benki ya Azania inayomdai Shellukindo, haikuwa tayari kueleza kiasi cha fedha inachomdai wala mwenendo wa kesi hiyo huku wasemaji wa benki hiyo wakielezwa kuwa kwenye vikao kwa muda mrefu.
“Ni kweli hiyo kesi ipo, lakini mimi siyo msemaji. Kwa sasa wasemaji wa benki wako kwenye kikao cha muda mrefu, labda ufuatilie huko huko mahakamani ” alisema mmoja wa watumishi wa benki hiyo anayefanya kazi katika kitengo cha sheria ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Shellukindo ajibu
Alipotakiwa kuzungumzia kesi yake hiyo, Shellukindo alisema hana taarifa kwamba mahakama imemtaka afike mahakamani hapo Machi 7 kusikiliza kesi hiyo.
"Mimi sina taarifa yoyote kwamba natafutwa," alisema Shellukindo akielezea kushangazwa na jinsi jambo hilo linavyopewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari kwa kile alichosema, "We ni mwandishi wa kumi unanipigia kuniulizia juu ya jambo hilo."
Alikiri kuwa ni kweli ana deni analodaiwa na benki hiyo na kwamba, suala hilo siyo la ajabu kwa sababu ni Watanzania wengi wamekopa benki na wanadaiwa hivyo anashangaa kuona yeye kukopa imekuwa ajabu.
Hata hivyo, alitafsiri suala hilo kuwa ni mchezo unaochezwa na maadui zake kisiasa kwa lengo la kumchafua na kushusha heshima yake mbele ya jamii.
Shellukindo alienda mbali akiwatuhumu baadhi ya waandishi wa habari wanaolifuatilia suala hilo kwamba wamehongwa ili kumchafua."Siyo ajabu sasa watakuja wachunguze mimi na mume wangu tuna ndoa au la," alilalamika Shellukindo
Uamuzi huo imeiweka njia panda Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi ambayo ilishaanza kazi kwa mujuibu wa maelekezo ya Spika wa Bunge, ambyo sasa haina lam kufanya zaidi ya kusubiri maelekezo mapya.
Hadi Masaburi alipoamua kuondoa mashtaka yake dhidi ya wabunge hao, tayari kamati hiyo ilikuwa imewahoji vigogo kadhaa wakiwamo Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hussein Katanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Simon Group (wanunuzi wa UDA), Robert Kisena.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinawataja wengine waliokuwa tayari wamehojiwa kuwa ni wabunge wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (Temeke – CCM), Iddi Azzan (Kinondoni-CCM) Mussa Azan Zungu (Ilala-CCM) pamoja na wabunge waliokuwa wakituhumiwa na Masaburi ambao ni Halima Mdee (Kawe – Chadema), Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki – CCM) na Abdulkarim Shah (Mafia – CCM).
Masaburi alizungumzia kuondoa mashtaka yake alipoitwa mbele ya kamati hiyo mwanzoni mwa wiki hii, hatua ambayo imeifanya kamati hiyo kuendelea na suala hilo ikisubiri maelekezo ya Spika wa Bunge, Anne Makinda.
“Kwa kifupi sisi hatuwezi kuendelea na suala hilo kwani Massaburi alituambia kwamba tayari ameishaiwasilisha kwa Spika barua ya kuondoa malalamiko yake, sasa sisi tunasubiri maelekezo ya Spika maana ndiye aliyetupa sisi kazi hii,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho na kuongeza:
“Hadidu za rejea alizotupa Spika zinatufunga, hatuwezi kwenda nje ya hapo kwani maelekezo ni kufanyia kazi malalamiko ya Masaburi, sasa kama ameondoa mashtaka yake unadhani sisi tutafanyaje, hakuna kinachoendelea kuhusu suala hilo, tunafanya kazi nyingine zilizopo halafu mwenyewe (Spika) akija atatupa maelekezo”.
Habari zaidi kutoka ndani ya kamati hiyo zinasema iwapo Spika ataamua kuachwa kwa suala hilo, basi nguvu kubwa ya wabunge, fedha na muda waliotumia kuwahoji wahusika wengine vitakuwa vimepotea bure
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ni moja ya kamati nne ambazo zilipewa kibali na Spika Makinda kutekeleza majukumu yake baada ya kumalizika kwa mkutano wa sita wa Bunge mjini Dodoma.
Kamati nyingine ni Hesabu za Serikali inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe na Kamati ya mambo ya Ukimwi, inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lediana Mung’ongo.
Mara kadhaa juzi na jana kwa nyakati tofauti, gazeti hili liliwatafuta Spika Makinda, Ngwilizi na Masaburi kupitia simu zao za viganjani bila mafanikio kwani zilikuwa zikiita kwa muda mrefu bila majibu.
Hata hivyo, Katibu Wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema kuwa suala hilo anapaswa kulijibu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
“Yeye (Ngwilizi) anaweza kulielezea vizuri kwa sababu kamati yake ndiyo inayolishughulikia,” alisema Dk Kashililah.
Kiini cha mgogoro
Mgogoro huo ulianzia Bungeni Agosti 3 na 4 mwaka jana, wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Uchukuzi, pale baadhi ya wabunge walipozungumzia kile walichosema kuwa ni uuzwaji kinyemela wa hisa za UDA na kutaka wahusika akiwamo Dk Masaburi wachukuliwe hatua.
Katika mjadala huo, wabunge hao na wengine walitishia kutoipitisha bajeti hiyo na kutaka wote waliohusika katika uuzaji wa UDA wawajibishwe.
Pia walitaka Dk Masaburi ajiuzulu kabla Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hajaingilia kati na kuunda kamati kuchunguza kashfa hiyo.
Siku moja baadaye, Agosti 5, Dk Masaburi akiwa mjini Arusha, aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema kwamba “wabunge wameshindwa kufikiri kwa kutumia akili na badala yake wanatumia makalio yao kufikiri”, kauli ambayo ilichochea mgogoro huo kuendelea
Matamshi ya Masaburi yalimfanya Mbunge wa Kinondoni (CCM), Iddi Azan ambaye Agosti 10, mwaka jana alitumia Kanuni ya 68 (7) ya Kanuni za Bunge toleo la 2007 kuomba mwongozo wa Spika kwa maelezo kwamba kauli ya Meya si kwamba tu ilikuwa imewadhalilisha baadhi ya Wabunge, bali Bunge zima na kwamba inakiuka kinga na haki za Bunge
Naibu Spika, Job Ndugai akitoa mwongozo kwa Azan aliamuru suala hilo kupelekwa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili iweze kulichunguza na kulishauri Bunge ipasavyo
Hata hivyo Kamati hiyo ilipopewa kazi na Spika ilielekezwa kufanyia kazi malalamiko ya Msaburi kwa wabunge na siyo malalamiko ya wabunge dhidi ya Meya huyo ambaye hivi sasa anaomba ridhaa ya wabunge kuchaguliwa tena kuingia katika Bunge la Afrika Mashariki.
Hatua ya Masaburi kuomba kuondoa mashtaka yake inatafsiriwa kuwa ni hatua ya kukwepa mgogoro baina yake wawakilishi hao ambao ni wapigakura wake watakaomua hatma iwapo atarejea katika Bunge la Afrika ya Mashariki au la.
Uchaguzi huo utafanywa katika mkutano wa saba wa Bunge utakaofanyika mwezi April mwaka huu
Source;Mwananchi.

MASABURI vs KAMATI YA BUNGE
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi ameondoa kesi aliyokuwa amefungua dhidi ya wabunge watatu kwa madai kwamba walimshambulia bungeni, hatua inayoonekana kulichanganya Bunge.

No comments:
Post a Comment